CUF yaendelea kumeguka ambapo Vijana zaidi ya 300 wajiunga na CCM Mtwara

MAIGIZO TU YA CCM HAYO WALA SIO JAMBO GENI,,,TENA IMETANGAZWA NA TBC CCM,,,HAHAHAHA
 
Huyo anastazia ni Mbunge wa kuchaguliwa wa Mtwara? Au amekiuka agizo la Mtukufu Rais la kufanya siasa ulipochaguliwa tu. Au amejificha kwenye kivuli cha Unaibu Waziri. Jamaaa wanasahu kabisa Matamko yao Kweli cccm ni janga
 
Duh! Umevurugwa wewe

Siyo kuvurugwa, ila taarifa yenyewe inajichanganya. mara vijana 300 wa cuf kuhamia ccm hapohapo kikundi cha ujariamali cha mbogamboga. Sasa huoni kuweka mambo mawili kwa pamoja msomaji anakosa uhondo?
 
Siooowaleee wajamaaaa alishindaaa akashikishwaaa mzigooo matokeo yakajakwao washindiii wananchi wakashtukaa walichana kadiwengitu
 
Mleta thread hii anasema waziri yupo ziara ya kikazi. Sasa hiyo kazi ya kuongeza wanachama wa chama chake ni kazi ya serikali au ya chama? Mi nafikiri hiyo ni ziara ya kichama. La msingi ni kuruhusu na wengine wafanye ziara hizo maeneo hayohayo. Usishangae hao wote aliowapata wakapatwa na mwingine wa chama tofauti. Politics and those who believe in it are dynamic.
 
Muda wa kupitia michango yangu sina ila nna uhakika sijawahi kujinasibu kuwa mimi ni CCM au wa chama cha upinzani,nimejengwa kwenye misingi ya kuhoji,kudadisi,kukosoa na kusifia pale inabpobidi ila si kushabikia chochote bila tafakuri,
ndo maana ya PL 111 na PL 100
Endelea kujidanganya.
 
Mleta thread hii anasema waziri yupo ziara ya kikazi. Sasa hiyo kazi ya kuongeza wanachama wa chama chake ni kazi ya serikali au ya chama? Mi nafikiri hiyo ni ziara ya kichama. La msingi ni kuruhusu na wengine wafanye ziara hizo maeneo hayohayo. Usishangae hao wote aliowapata wakapatwa na mwingine wa chama tofauti. Politics and those who believe in it are dynamic.
Waziri anafanya ziara ya kiserikali
na serikali ni ya chama cha mapinduzi.
Pia ameongozana na mbunge wa jimbo hilo ambae ni wa Ccm

Waziri au naibu waziri ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa hivyo basi ni kiongoz wa CCM wa kitaifa
Kiprotocal alipo lazima uongozi wa mkoa na wilaya husika wa CCM lazima uwepo.

Nia tunayo,
Uwezo tunao
Na Sababu tunayo
kuzuia UKUTA WA WALEVI
 
Wakitibuana huko kwenye mradi wa mbogamboga watarudi tena CUF mana ndo mwanaume anaeshikilia jimbo la Mtwara na viunga vyake
 
Navy boi, mimi sijakataa kwamba waziri ni mwanachama wa CCM. Nahoji kama hiyo ni sahihi kuiita ziara ya kiserikali. Waweza kuwa mwanajeshi lakini ukaenda ziara ya kifamilia. Kwa hiyo si kila ziara ya waziri ambaye ni mwana CCM ni ya kichama. Kwani wewe ndugu kweli hujui hilo? Hujui tofauti ya ziara ya kichama na ziara ya kiserikali?
 
Chama cha Wananchi, CUF kimeendelea kusambaratishwa Tanzania Bara. Maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake wameendelea kukikimbia chama hicho na kujiunga na chama kubwa, CCM. Safari hii ni zamu ya vijana zaidi ya 300 walioachana na CUF na kujiunga na CCM ambapo kwa sasa wameamua kuchapa kazi kupitia kikundi chao za ujasiriamali kinachojishughulisha na kilimo cha mbogamboga.

Wanachama hao wamepokelewa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Vijana hao wamesema kuwa wakati wanajiunga na CUF walishawishiwa kipindi ambacho kulikuwa na vuguvugu la gesi. Kwa sasa ukweli wameuona na wameamua kuachana na vyama vya kitapeli na kilaghai.

Chanzo: TBC1 Habari
Huyo Waziri kaenda kikazi, hayo kupokea wanachama wapya wapi na wapi? Kama alienda kichama (taarifa yenu haisemi hivyo) jee kule ni jimboni kwake? Polisi nao walikuwepo wakimlinda waziri.
 
Mkuu, watu wakihama kwenye vyama vyenu na kujiunga na CCM mnasema si big news ila wakihama CCM na kujiunga na magenge yenu mnaitisha Press tena inarushwa live. Kichekesho
Vipi Lukuvi, Membe na yule DC bado wanamhujumu mkuu wa nchi kama ulivyotuaminisha siku cha zilizopita?
 
Hakuna cha vijana 300 wala nini. Ni uongo uliokubuhu unaoenezwa na CCM. Mtwara ni ngome na itaendelea kuwa ngome imara ya CUF. Hao hawajawahi kuwa wanachama wa CUF bali ni vijana wachache wenye njaa na ambao wanataka kujipatia kipato ili kukidhi njaa waliyonayo. Hadi leo ukipita kwenye mitaa ya Mkana Red, Mangowera, Ligula, Chikongola, Kisutu, Likonde, Magomeni, Mangamba, Mdenga hadi Msanga mkuu ni mitaa ambayo hutakuta bendera ya CCM inapepea isipokuwa kwenye ofisi ya tawi. CCM hapa Mtwara mjini ni kama imekufa.
 
Navy boi, mimi sijakataa kwamba waziri ni mwanachama wa CCM. Nahoji kama hiyo ni sahihi kuiita ziara ya kiserikali. Waweza kuwa mwanajeshi lakini ukaenda ziara ya kifamilia. Kwa hiyo si kila ziara ya waziri ambaye ni mwana CCM ni ya kichama. Kwani wewe ndugu kweli hujui hilo? Hujui tofauti ya ziara ya kichama na ziara ya kiserikali?
Hio ni ziara ya kiserikali
Ila ameambatana na watu wa chama kiprotocal

Usilazimishe mkuu
 
Back
Top Bottom