CUF yaendelea kumeguka ambapo Vijana zaidi ya 300 wajiunga na CCM Mtwara

Weston Songoro

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
2,793
1,083
Chama cha Wananchi, CUF kimeendelea kusambaratishwa Tanzania Bara. Maelfu kwa maelfu ya wafuasi wake wameendelea kukikimbia chama hicho na kujiunga na chama kubwa, CCM. Safari hii ni zamu ya vijana zaidi ya 300 walioachana na CUF na kujiunga na CCM ambapo kwa sasa wameamua kuchapa kazi kupitia kikundi chao za ujasiriamali kinachojishughulisha na kilimo cha mbogamboga.

Wanachama hao wamepokelewa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Anastazia Wambura alipofanya ziara ya kikazi mkoani humo.

Vijana hao wamesema kuwa wakati wanajiunga na CUF walishawishiwa kipindi ambacho kulikuwa na vuguvugu la gesi. Kwa sasa ukweli wameuona na wameamua kuachana na vyama vya kitapeli na kilaghai.

Chanzo: TBC1 Habari
 
Wakati wa kampeni siku mgombea urasi wa CCM alipozuru Mtwara kuna vijana walihama Chadema wakahamia CCM na mmoja wao aliongea live,,,ajabu lile jimbo likaenda upinzani na umati wote ule pale Ntwara mjini.Julai 23 tumeshuhudia wanasiasa wengi wakirudi CCM kutoka upinzani, na ikumbukwe hata Kingunge and Co walikuwa CCM wakaenda upinzani.So suala la watu kuhama vyama hapa Tanzania sio issue kwa sasa wala big news mdau labda kwako hasa kwa msimu huu ambao hauna uchaguzi wala nini.Msimu wa kusaka pesa ya kula tu
 
.........Vijana hao wamesema kuwa wakati wanajiunga na CUF walishawishiwa kipindi ambacho kulikuwa na vuguvugu la gesi. Kwa sasa ukweli wameuona na wameamua kuachana na vyama vya kitapeli na kilaghai.[/QUOTE]
Wameuona ukwel gani?
 
Wakati wa kampeni siku mgombea urasi wa CCM alipozuru Mtwara kuna vijana walihama Chadema wakahamia CCM na mmoja wao aliongea live,,,ajabu lile jimbo likaenda upinzani na umati wote ule pale Ntwara mjini.Julai 23 tumeshuhudia wanasiasa wengi wakirudi CCM kutoka upinzani, na ikumbukwe hata Kingunge and Co walikuwa CCM wakaenda upinzani.So suala la watu kuhama vyama hapa Tanzania sio issue kwa sasa wala big news mdau labda kwako hasa kwa msimu huu ambao hauna uchaguzi wala nini.Msimu wa kusaka pesa ya kula tu
Mkuu, watu wakihama kwenye vyama vyenu na kujiunga na CCM mnasema si big news ila wakihama CCM na kujiunga na magenge yenu mnaitisha Press tena inarushwa live. Kichekesho
 
.........Vijana hao wamesema kuwa wakati wanajiunga na CUF walishawishiwa kipindi ambacho kulikuwa na vuguvugu la gesi. Kwa sasa ukweli wameuona na wameamua kuachana na vyama vya kitapeli na kilaghai.
Wameuona ukwel gani?[/QUOTE]
Nadhani wamebaini kuwa gesi ina manufaa makubwa kwa taifa na Mtwara sasa inapiga kasi kubwa kimaendeleo tofauti na walivyoaminishwa kuwa kila kitu kutajengwa Dar na Bagamoyo
 
Mkuu, watu wakihama kwenye vyama vyenu na kujiunga na CCM mnasema si big news ila wakihama CCM na kujiunga na magenge yenu mnaitisha Press tena inarushwa live. Kichekesho
Nikusaidie tu kuwa mimi sina chama,napenda kuyaangalia mambo kwa uhuru zaidi,ndo maana nimebalance kwa kumtaja mzee Kingunge and Co.Ila kwakua una ASHKI MAJINUNI umejikuta unajibu tu pasina tafakuri.Mi siwez kushtuliwa na habar za kuama vyama kwa kua si habar tena kwa sasa.Habar za kuama vyama zilianza kabla wewe hujajua siasa enzi za kina mrema kwenda NCCR akina Oska Kambona na UMD,sijui kama unakijua hiko chama
 
Mkuu, watu wakihama kwenye vyama vyenu na kujiunga na CCM mnasema si big news ila wakihama CCM na kujiunga na magenge yenu mnaitisha Press tena inarushwa live. Kichekesho
Unategemea isemwe ni big news? Atakayesema hivyo atakuwa na mtindio wa ubongo, unamkumbuka,Al sahaf(sina uhakika wa jina linavyoandikwa) wakati Iraq inapokea kipigo?
 
Kwani kuhama chama au kuacha kushiriki maswala ya siasa ndio kawaida wala si jambo la kushangaza, kitu cha kushangaza ni kukataza kufanya watu wengine kufanya siasa mkizunguuka tanzania nzima na wengine kuzuiwa acheni muone mtakavyomeguka kama biskuti kwenye maji maana mnachosema kingine na uhalisia tofouti maana mmesema elimu bure huku wanafunzi wanachangishwa mlinz na maji hapa mwananchi atawafurahieni au mkamtoa kwenye sukari 2000 mpaka 3500 mtaeleweka au mtu alikuwa anapata huduma ya upasuaji kwa 80000/: leo huduma hiyohiyo anaipata laki hasini mtaeleweka mjane alikuwa na kijumba chake cha vyumba vinne ambavyo ndio anavitegemea leo mnamwambia alipie kodi mtaeleweka nk ndio maana mnaogopa kuacha na wengine waseme ili tujue ukweli na uhalisia tunapokwenda
 
CUF ni miongoni kwa vyama vichache Tanzania chenye wanachama wa damu kabisa, yaani hao wanachama wa CUF kanda ya Kusini wana sababu zao za kuwa CUF ambazo CCM wala Chadema hazipo
Wameenda kupiga hela tu hao kwenye mioyo yao bado ni CUF
 
Ngoja niulize kwanza.. hivi UKAWA bado ipo?maana Mbatia kapotea gafla
Gauni la bibi harusi huvaliwa mara moja tu. Ukawa ni sawa na gauni la bibi harusi, baada ya harusi bibi harusi anavaa kanga moja kumfurahisha mumewe.
 
Back
Top Bottom