CUF ya upande wa Lipumba huenda kumvua uanachama Mtatiro

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,020
MWENYEKITI wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif, Julius Mtatiro na wenzake huenda wakavuliwa uanachama baada ya kudaiwa kukaidi wito wa kamati ya utendaji ya chama hicho.

Wanachama hao waliitwa na Kamati ya Utendaji ya CUF Wilaya ya Ubungo kujibu tuhuma kwanini wasifukuzwe kutokana na mienendo yao ndani ya chama hicho.

Mbali ya Mtatiro wengine ni Khalid Singano, Kassim Choga, Mawano Yusuf Kilemi, Jumanne Ally, Mwinyi Khamis na Twaha Rashid.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katibu wa CUF Wilaya ya Ubungo, Ali Makwilo, alisema kikao hicho kilifanyika jana lakini waliotikia wito huo ni wanachama wawili tu.

Aliwataja wanachama walioitikia wito huo kuwa ni Katibu wa Tawi la Kimara Stop Over, Yahaya Muhsin na Katibu wa Tawi la Matangini, Patrick Mwakasege.

“Ni kweli tumewaita na wapo waliokuja lakini Mtatiro na wenzake hawakuja, maana yake wamedharau wito. Kisheria ukituhumiwa halafu hukwenda unaruhusu mamlaka ikuadhibu.

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA
 
So sad,
Itakuwa ndio mwisho wa siasa za uchochoroni za Lipumba...... 2020 sio mbali.... aibu kubwa yaja nyuma yake....
wenzie washaanza kutimkia CCM .

BTW kina Mtatiro na wengine, they have lots of options..
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi kwanni kina mtatiro na seif wasijitoe wakaunda chama kimoja na hao chadema na kina zitto ili CCM isitugawanye maana ikifika 2020 alafu CUF bado imegawanyika ni wazi kabisa kanda ya pwani nzima itarudi ccm
 
Msitutoe kwenye reli ya baba askofu Zakary Kakobe. Habari ya mjini kwa sasa ni askofu Zakary Kakobe, aliyemtaka Magufuli atubu haraka iwezekanavyo kwa UOVU mkubwa aliyoufanya.

Magufuli anainajisi katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea kwa kuvikandamiza vyama vya siasa na kuifanya nchi hii kuwa kama ya chama kimoja. Hii ndiyo habari ya mjini.

Kusema kwamba Mtatiro na wenzake wanaoweza kuvuliwa uanachama na genge la wahuni linaloongozwa na prof Lipumba ni ndoto za mchana.
 
Kuna ruzuku yao kama sikosei 500 millions, jambazi Lipumba anainyemelea hii lakini mahakama imempiga stop.

Hivi kwanni kina mtatiro na seif wasijitoe wakaunda chama kimoja na hao chadema na kina zitto ili CCM isitugawanye maana ikifika 2020 alafu CUF bado imegawanyika ni wazi kabisa kanda ya pwani nzima itarudi ccm
 
Uko sawa kabisa Mkuu. Mimi huiita CUF haramu maana huwezi ukajiuzulu ukafukuzwa uanachama halafu bado ukarudi kwenye chama kinyemela na kurudia wadhifa wako. Huu ni uhuni wa hali ya juu unaoungwa mkono na MACCM.
Mkuu hapo kwenye jina CUF "HARAMU" ndio umepatia haswaa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi kwanni kina mtatiro na seif wasijitoe wakaunda chama kimoja na hao chadema na kina zitto ili CCM isitugawanye maana ikifika 2020 alafu CUF bado imegawanyika ni wazi kabisa kanda ya pwani nzima itarudi ccm
Tatizo ni uroho wa madaraka.Kila mmoja wao atataka yeye ndo awe Mwenyekiti au mgombea Urais 2020.
Hoja ni nzuri lakini ni ngumu kutekelezeka.
 
Tatizo ni uroho wa madaraka.Kila mmoja wao atataka yeye ndo awe Mwenyekiti au mgombea Urais 2020.
Hoja ni nzuri lakini ni ngumu kutekelezeka.
Mbona 2015 iliwezekana Cuf na nccr na NLD walimpisha mgomba urais wa chadema ..... Naamini ni maridhiano tu yanaweza leta suluhu lasihivyo ikifika 2020 wakiwa bado wanaendekeza kina lipumba wataanguka vibaya sana
 
Back
Top Bottom