MANGI MASTA
Senior Member
- Jul 14, 2011
- 175
- 56
Leo kuanzaia saa 2 had 7 katika viwanja ya mahakama ya kilwa masoko umati wa watu ulikuwa umejaa na FFU wengi wamemwagwa eneohilo,ilikuwa ni katika kusubiri hukumu ya kesi iliyodumu takribani mwaka mmoja ambapo aliyekuwa mgombea wa ccm jimbo la Kilwa kusini wa Bw.Ramadhani Madabida alifungua kesi dhidi ya mbunge mchaguliwa wa CUF.Mh.Suleman Bungara(maarufu kwa jina la *****).Miongoni mwa tuhuma za CCM waliwatuhumu CUF kumchafua mgombea wa CCM na kwamba kunawapigakura 16 wa ccm walinyimwa kupiga kura.Baada ya masaa 4 ya kusomwa hukumu na jaji Fatma kutupilia mashtaka ya ccm dhidi ya CUF viwanja vya mahakama viligeuka ukumbi wa Sherehe kwani wakazi wengi wa jimbo la Kilwa kusini hasa wafuasi wa CUF walikuwa wamejaa mahakamani hapo kujua hatma ya kesi ya Mbunge wao.