CUF nao wamshukia Nnauye

lini utalivua gamba la lowassa na chenge?anaropokaropoka kila siku ili kuwasahaulisha watu kwamba kaufyata mkia kwa lowassa...poor creature
 
Alisema njia sahihi ya kulinda rasilimali zilizopo na zinazoendelea kugunduliwa nchini Serikali ya Umoja wa Kitafa ambayo itashirikisha vyama vyote vyenye wabunge.

Aliongeza kuwa, kwa kuzingatia utaratibu huo hakuna chama ambacho kitakuwa na maamuzi yake katika matumizi ya rasilimali na Maliasili za nchi.}
Huu ni uroho wa madaraka tu, Mkishaungana hakuna atakayemtetea mwanchi wa kawaida, mtaishia kugawana mnachopata kama mnavyofanya huko zanzibar sasa hivi, wananchi tunachotaka chama tawala kiwe na asilimia 60% ya wabunge na upinzani uwe na 40%. Hapo hakutakuwepo na kulala wala kuiba, lakini mkikubaliana mkaunda huo mchanyato wenu, duuu! tumeliwa.
 
Nape ni jembe la CCM. Mimi naona anachofanikiwa mara zote anapotoa matamko ni kuwafanya wapinzani wake wamjadili yeye badala ya kujikita kwenye adui yao mkuu ambaye ni chama anachokiwakilisha.
 
Nape ni jembe la CCM. Mimi naona anachofanikiwa mara zote anapotoa matamko ni kuwafanya wapinzani wake wamjadili yeye badala ya kujikita kwenye adui yao mkuu ambaye ni chama anachokiwakilisha.

Anajadiliwa yeye au utumbo wa ccm ambao yeye ndo katumwa autoe..?

Sent from Tora Bora..
 
Siamini katika serikali ya umoja wa kitaifa...kama vyama vyote vikiunda serikali ni nani atakayeikosoa? ni nani atakayeibua skendo kama za deep green, kagoda,meremeta n.k?nani atahoji uozo serikalini?
 
nchi hii wakichukua wachagga watauza kila kitu. na hilo halitatokea hata watembee uch. na mik.nd. juu.
 
Nape pole sana , kumbe huna habari kuwa bajeti ya Tz asilimia arobaini inategemea wafadhili .
 
Hata jk nae mchaga ndo mana anajua sana fedha.Wewe nawe eti ndo gamba mbona mtupu hivi !Hueleweki nini waandika?ubaguzi utakusaidia nini kijana zaidi ya kujaza pumba kichwa.Ee Mchungaji Msigwa maneno yako yatakumbukwa daima yaani akili ndogo kuongoza akili kubwa.
 
16 AUGUST 2012

Na Grace Ndossa

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimedai kushangazwa na kauli iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye kwa vyombo vya habari kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeingia mikataba ya kifisadi na wafadhili wa nje ili kupora rasilimali za nchi.

Taarifa iliyotolewa Dar es Salaama jana na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Bw. Abdul Kambaya, alisema Bw. Nnauye hakupaswa kuishtaki CHADEMA kwa wananchi bali kupitia Serikali yao walipaswa kuzuia fedha hizo na kuwataja wafadhili hao.

“CUF kimeshangazwa na kauli hii ambayo imetolewa na msemaji wa CCM, ambacho ndio chama kinachoongoza nchi, tulitarajia Bw. Nnauye angewataja hao wafadhili wa CHADEMA ambao dhamira yao ni kupora rasilimali za nchi,” alisema Bw. Kambaya.

Aliongeza kuwa,
chama hicho kinaamini CCM na CHADEMA ni watoto wa familia moja ambapo wafadhili wao ndani na nje ya nchi pia wa aina moja.

“Kama
CHADEMA imeingia mikataba ya kupewa mabilioni ili baadae wataposhika madaraka waweze kulipa mabilioni hayo kupitia rasilimali za nchi basi watakuwa wanaendeleza utaratibu wa CCM kuingia mikataba mibovu isiyo na tija kwa Watanzania,” alisema.

Alisema CUF inaamini kuwa,
tatizo lililopo nchini ni mifumo mibovu inayoendesha Serikali, nchi, kukithiri kwa wizi, matumizi mabaya ya fedha za umma na ukiukwaji wa haki za binaadamu.

Bw. Kambaya alisema, sababu ya Watanzania wengi kuwa maskini wa kutupwa, ukosefu wa huduma bora kwa jamii, kudumaa kwa maendeleo ya nchi na ukosefu wa ajira ni matokeo ya muda mrefu yanayosababishwa na mfumo mbovu uliopo.

Alisema njia sahihi ya kulinda rasilimali zilizopo na zinazoendelea kugunduliwa nchini Serikali ya Umoja wa Kitafa ambayo itashirikisha vyama vyote vyenye wabunge.

Aliongeza kuwa, kwa kuzingatia utaratibu huo hakuna chama ambacho kitakuwa na maamuzi yake katika matumizi ya rasilimali na Maliasili za nchi.

“Sisi tunataka Watanzania waelewe kuwa, mazingira yanaonesha CHADEMA kimeizidi kete chama tawala kwa kuwa na wafadhili wa nje ndio maana CCM Inapiga kelele,” alisema.



Sikubaliani na msemaji hapo kwenye RED kwakuwa hapo kwenye YELLOW sisi tunapapiga vita sana. Hofu yangu kwa msemaji huyu ni kuwa"ANAONEKANA KUENDELEZA PUMBA ZA NAPE KWA NJIA MBADALA"
 
Sikubaliani na msemaji hapo kwenye RED kwakuwa hapo kwenye YELLOW sisi tunapapiga vita sana. Hofu yangu kwa msemaji huyu ni kuwa"ANAONEKANA KUENDELEZA PUMBA ZA NAPE KWA NJIA MBADALA"

Kwanza Wajaribu kuchabadilisha hao viongozi wao wamekuwa Mwenyekiti na Katibu Mkuu tokea Chama hicho cha CUF

Kilipoanzishwa, hajuna Viumbe wengine? Wamegombea Urais Miaka nenda rudi huo sio Udiktekta? Yaani hakuna

Mwanadamu Mwingine atakaye iongoza CUF zaidi ya WAO?
 
Back
Top Bottom