CUF, CHADEMA kipi kitatufaa?

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,148
CUF, CHADEMA kipi kitatufaa?




amka2.gif

WATANZANIA wenzangu, kama nilivyofafanua wiki mbili zilizopita, kwa kigezo cha kwanza, cha haiba na imani ya wananchi (walio wengi), Chama cha Wananchi (CUF), kimeonekana kuporomoka tangu mwaka 2005.
Kwa kigezo cha ajenda, wiki iliyopita nilianza kugusia kwa muhtasari kile ambacho CUF inaamini na inakusudia kufanya pindi ikipata ridhaa ya kuongoza dola. Sasa tuitathmini ajenda hiyo ili kuona ni kwa kiasi gani chama hicho kina majibu ya msingi na yanayotekelezeka dhidi ya kero na matatizo yanayowakabili wananchi.
Izingatiwe kuwa CUF ni chama cha kiliberali kinachoamini katika ‘haki sawa kwa wote’ kama falsafa yake, utajirisho kama itikadi yake, elimu bora, afya madhubuti, mfumo adilifu wa kodi, Muungano wa haki, siasa kuwa utumishi ulioutukuka kwa umma na fursa sawa katika kujiendeleza kiuchumi, kijamii na kisiasa kama sera zake.
Ajenda ya CUF inaonekana kuwa nzuri katika muktadha wa itikadi, falsafa na sera zake. Ni nzuri kwa sababu tu inazungumzia matatizo na kero ambazo zipo nchini. Mathalan, inazungumzia haki sawa kwa wote dhidi ya unyonyaji, ukandamizaji na ubaguzi katika nyanja mbalimbali; utajirisho na mfumo adilifu wa kodi dhidi ya umaskini uliopo na haja ya kuwa na muundo wa serikali tatu kama msingi wa kutanzua kero nyingi zilizopo kwenye muungano.
Hata hivyo, kiwango cha uzuri wa ajenda hiyo bado hakitoshi kukifanya chama hicho kionekane kuwa mbadala wa CCM, kwani karibu masuala yote inayoyazungumzia, (ukiondoa Muungano wa serikali tatu), yanapatikana pia ndani ya sera kadhaa za CCM na serikali yake.
Maudhui ya ajenda ya CUF hayawezi kumsaidia Mtanzania makini kujua nini hasa tofauti ya msingi kati ya chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Aidha, maudhui hayo bado hayajafanikiwa sana kuonyesha ni kwa kiasi gani serikali ya chama hicho inaweza kuwa bora kuliko serikali ya CCM. Nitoe mifano;
Wakati CUF inazungumzia haki sawa kwa wote, ndani ya sera na maandiko kadhaa ya CCM na serikali yake, dhana ya haki sawa nayo inajitokeza sana, licha ya kuwepo tofauti ndondogo mno za maneno na mantiki (rejea itikadi ya ujamaa na kujitegemea, na sera kadhaa za CCM na serikali yake tangu enzi za Mwalimu hadi sasa).
Wakati CUF inazungumzia kuleta utajirisho, CCM nayo inazungumzia kupunguza umaskini wa kipato na usio wa kipato, pamoja na kuimarisha utawala bora na wenye uwajibikaji ili kuboresha maisha ya watu (maisha bora kwa kila mtanzania), sawa tu na utajirisho huo wa CUF.
Wakati CUF inazungumzia kuleta elimu bora ya msingi na sekondari kwa kila mtanzania bure, CCM nayo inadai kuwa inatoa elimu ya msingi bure na inahakikisha kuwa hakuna mtoto yeyote atakayeshindwa kupata elimu ya sekondari kwa sababu ya ada. Kuna tofauti gani za kimsingi kati ya ajenda ya Cuf na CCM?
Ajenda ya CUF inaonekana kukosa uwezo wa kujiuza yenyewe, kwani matatizo inayoyazungumzia na ufumbuzi inaoutoa, havionekani kuwa na tofauti zozote za kimsingi na kile kilichopo kwenye ajenda au sera za CCM kama nilivyododosa hapo juu.
Kwa kuwa utekelezaji wa sera na ahadi nzuri za CCM umekuwa sio wa kuridhisha, basi ili mtu aunge mkono ajenda au sera za CUF (zinazofanana na za CCM), itampasa awaamini viongozi wa CUF kuwa ni watekelezaji mahiri kuliko viongozi wa serikali ya CCM, vinginevyo ajenda ya CUF pekee haiwezi kumpa ushawishi wa kiutekelezaji kwani inafanana kwa kiasi kikubwa na ile ya CCM.
Mtanzania akimsikiliza kwa makini mwanasiasa mahiri wa CCM akinadi ilani au sera za chama chake na kisha kumsikiliza mwanasiasa mahiri wa CUF akinadi sera za chama hicho, hakuna tofauti za kimsingi ambazo atazipata baina ya vyama hivyo viwili (neno ‘tofauti za kimsingi’ lizingatiwe).
Wanaweza kutofautiana sana kwenye ufundi wa kupigana vijembe na kukashifiana lakini si kwenye kueleza ni nini hasa kifanyike ili kuboresha maisha ya Mtanzania.
Kwa mantiki hiyo, ni kiwango cha imani tu na mvuto wa kisiasa, ambao mtu anaweza kuupata kwa viongozi wa Cuf na CCM, ndiyo utakaoamua aunge mkono chama kipi kati ya hivyo viwili, kwani ajenda za vyama vyote zinafanana kwa kiasi kikubwa.
Kwa maneno mengine, kinachoweza kumfanya mwananchi amchague Profesa Ibrahim Lipumba, wa Cuf na kumwacha Kikwete wa CCM sio tofauti za ubora wa ajenda au sera za Cuf dhidi ya CCM, bali ni imani tu ambayo mwananchi huyo anayo kwa Lipumba pamoja na ushawishi wa haiba yake.
Itiliwe maanan kuwa kwa nchi yenye umaskini uliopitiliza kama Tanzania, ni rahisi sana kwa chama chochote cha siasa kupata ajenda za kufanyia siasa. Matatizo ni mengi mno, kwa hiyo tunaweza kuwa na vyama hata mia moja kila kimoja kikiwa na ajenda au sera yake kuu.
Hata hivyo, chama chenye ajenda bora kitakuwa ni kile tu ambacho ajenda yake kuu imechepukia kwenye chanzo kikuu cha matatizo na kero zote zilizopo, huku ajenda hiyo ikitoa ufumbuzi wa msingi, unaotekelezeka na ulio kipaumbele kuliko masuluhisho yote madogomadogo.
Ili chama husika cha siasa kipate ajenda bora na dira iliyo jibu la msingi dhidi ya kero na matatizo yaliyopo, ni muhimu kizingatie tafiti na kufanya tathmini linganishi juu ya matokeo ya tafiti hizo ili kupata ajenda iliyo nzito zaidi.
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kutoa nasaha nyingi juu ya kuufikia mustakabali bora wa taifa hili. Katika moja ya nasaha zake kuhusu hatma ya maendeleo ya taifa hili, Mwalimu alisema, ili tuendelee tunahitaji ardhi, watu, siasa safi na uongozi bora. Naamini vyote tunavyo isipokuwa uongozi bora.
Udhaifu wa CCM si sera zenye dira nzuri na maneno matamu (ambazo Cuf nayo inazinadi) bali ni kukosa dhamira, fikra na uthubutu wa kujenga serikali yenye uongozi bora na inayowajibika kikamilifu kwa umma (serikali ya wananchi).
Kwa bahati mbaya, ajenda ya Cuf haitusaidii sana katika kutuonyesha udhaifu huo wa CCM wala kutuambia kitu gani hasa mbadala itafanya kuondoa udhaifu huo. Ushawishi wa ajenda, sera na dira ya Cuf, vimejikita katika kutujengea imani tu kwamba, ‘CCM imeshindwa kutekeleza, CUF itatekeleza’. Ajenda ya namna hiyo huwa dhaifu kwani hutegemea kuaminiwa tu badala ya kushawishi yenyewe ni kwa jinsi gani inatoa jibu la msingi dhidi ya kero na matatizo yaliyopo. Itaendelea wiki ijayo.


h.sep3.gif
juu
 
CHADEMA, hii ni taasisi ya Umma yenye malengo kwa UMMA, ilioudwa kwaajili ya kuudumia Umma, katika tafsiri yoyote ya cama mmbadala wa CCM, bila shaka chama hiki ni mbadala, hiki ni chama mama katika kupigania maslahi ya Umma, anaglia muundo wake, malengo yake, dhamira ya waliondani , ajenda zao katika maswala ya kijamii, hakika kuifananisha na CUF ni tusi kubwa.
CUF, NI CHAMA KAMA CHA KIDINI HIVI NA MAANA agebnda zao ni zakificho na mara nyingi hujitoza hadharani kujadili maswala ya kidini yakijitokeza mbele ya jamii. nikielelezo cha watu mufilisi angalia safu zao za uongozi angalia namna mikakati yao ya kisiasa ilivyo , tazama umaarufu wao uko maeneo yapi, kisha waangalie viongozi wao kitaifa....utaelewa hidden Agenda yao.....ukitaka maendeleo CHADEMA ni chama mbadala wa CCM.
 
Last edited:
Chadema ni chama makini na kinajitahidi sana kukuza demokrasia na kuelimisha wananchi umuhimu wa kujiletea maendeleo na kushiriki katika maamuzi ndani ya serikali. Cuf nacho kimejitahidi sana kuleta mapinduzi ya kidemokrasia na nina heshimu sana kazi za akina seif sharif hamadi, duni, na profesa lipumba hawa wote wamekuwa wanamapinduzi wa kweli na wamejitahidi sana kadri wawezavyo kutangaza mapinduzi ya kidemokrasia , ingwawaje CUF imekuwa na mvuto zaidi pemba na zanzibar imechelea kidogo kwenye siasa za bara na vilevile chadema wamepelea pemba na zanzabar na kuwa na mvuto zaidi bara, kama hawa wangeweza sikilizana na kufanya kuwa chama kimoja au kuungana wangeweza kumkoma nyani haraka sana. ila kwa sababu ya uchu wa madaraka na kila mmoja kutaka kuwa kinara inabidi kusubiri kidogo mpaka CCM watakapoacha kutumia ruzuku kama chambo ndipo watakapo sikilizana.

Chadema wapo makini sana bara kama CUF walivyo makini sana Pemba.
 
Back
Top Bottom