Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuwa anapangisha jumba lake la kifahari kwa takribani Tsh. 25,726,140 kwa mwezi

Mributz

Senior Member
Aug 29, 2022
112
388
Nyota wa klabu ya Alnassr na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuwa anakodisha/pangisha jumba lake la Kifahari lililopo katika jiji la Madrid nchini Unispania kwa euro 10,000 tu (takriban $10,980) sawa na Tsh. 25,726,140/= ( Milioni 25 za Kitanzania ) kwa mwezi!

Jumba hilo lenye ukubwa wa mita za mraba 43,000 linaelezwa kuwa lina vyumba saba vya kulala, bafu tisa, mabwawa mawili ya kuogelea, (Swimming Pool) uwanja wa mpira wa miguu, na kituo cha mazoezi ya viungo vya hali ya juu (Gym) na baadhi ya miongoni mwa maeneo mengine ya kifahari kama chumba cha Cinema na mengine.

Jumba hilo la Kifahari la Ronaldo linaelezwa kuwa ni miongoni mwa majumba ya Kifahari zaidi huku likiwa na paking ya magari ya ndani.

IMG_20230417_234156.jpg
 
Back
Top Bottom