CPA siku hizi bado ina advantage?

Ni bora mara mia uwe nayo kuliko kutokuwa nayo! You never know, kuna siku inaweza kukusaidia!
Ila kwa hii curriculum mpya utaenda kuchukua kweli au utachukuliwa wewe?
 

Attachments

  • Revised Syllabus June 2012.pdf
    451.3 KB · Views: 1,060
Napenda kuuliza wakuu cpa bado ina advantage siku hizi, maana nataka nikachukue lakini nasikia wanaziponda


CPA sio ya kuchukua mkuu ni ya kuitafuta, wapo watu wanaitafuta mwaka wa 6 huu, hawajaipata. Sahau swala la kuchukua, inahitaji kujipanga.

Hata hivyo ili uwe mhasibu unayetambulika kwa maana umeiva kitaaluma ni lazima uwe na CPA hasa kwenye soko la ajira, hizo za kuponda ni story za vijiweni temana nazo, ukweli ndo huo!
 
Kuna mtu nilimkuta ana vyeti kama hv huyu anaweza kuwa marketable wapi au kachanganya madesa ? Ana degree ya law, ana postgraduate ya HR, na master ya MRA(Revenue Administration) na mwisho ana CPB, wekeni mawazo yenu wadau
 
n vzur kuisaka hiyo CPA...nadhani mtoa maada alikuwa akiuliza kwa vzur na hakuwa na maana hiyo ya eti nikaichukue ama nikaiokote...maadam mmemwelewa basi n vzur mkamjibu kama inavyostahili na cyo kumjb kwa kumkebehi...by the way, kama kwako CPA kuipata n ishu basi kwa wengine n rahisi tu mbona, maana kama 4m4 alipata div. 1 pts 7 na 4m6 div. 1 pts 3 then chuo GPA ya 4.8, almost anaenda tu kuiokota au kuichukua tu iyo CPA...sasa ww kama ni kilaza basi usiseme wote n vilaza pia bali utambue kuwa kuna wapo wanaoenda kuchukua na kuna wanaoenda kuiokota na kuna wanaoenda kuisotea kwa kuipigania miaka nenda rudi n.k....
 
Acha mawazo ya kizamani wewe...... Kumbe pamoja na usomi wooote huo bado unamawazo ya enzi za kuajiriwa!!!!! Unasoma ili ukaajiriwe na "wahindi......." Wakunyonye mshahara ndo utachekelea? Badala ya kusoma ili uelewe mambo kisha ukajiajiri wewe unataka CPA ili ukaajiriwe..... Ili upate mshahara wa nusu milioni kwa mwezi....wakati kumbe unao uwezo wa kupata milioni 20 kwa mwezi!!!! Acha unyonge wewe.....
Sasa nakupa ushauri:
1). Soma digrii yako ya accounting and finance
2). Kisha soma CPA
Halafu baada ya kuhitimu USIAJIRIWE KABISA!!! Tena hata ile ajira ya "kujishikiza usijaribu, acha....
Nenda Mamlaka ya Mapato Tanzania ukajisajili kama Tax Consultant. Kwa mujibu wa maelezo yako, wewe uko elligible kusajiliwa kama tax consultant chini ya kifungu cha 134 na regulation 37 ya sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004. Fanya kazi kama tax consultant miaka mitatu kisha nenda NBAA (assuming tayari una CPA) wao watakusajili kama certified public accountant. Utakuwa unatengeneza mahesabu ya watu na pia kuwafanyia ushauri wa masuala ya kodi.
Nakuhakikishia hutatamani tena kuajiriwa..... Pesa utakayoipata kwa kipindi cha miaka ya mwanzo (miaka mitano mpaka kumi hivi) ni pesa ambayo hutakuja uipate kwa kuajiriwa hata kama utafanya kazi miaka sabini!!!! Amini nikuambiayo mimi.
Kama haitoshi naomba uni PM nikuelekeze zaidi....
Mkuu, naheshimu mchango wako ingawa kidogo unapotosha. Huwezi kusajiliwa kuwa tax consultant kama huna uzoefu unaotakikana. Na uzoefu ataupata kirahisi kupitia kuajiriwa au kufanya kazi na consultant ambaye ni mzoefu!
 
Mkuu, naheshimu mchango wako ingawa kidogo unapotosha. Huwezi kusajiliwa kuwa tax consultant kama huna uzoefu unaotakikana. Na uzoefu ataupata kirahisi kupitia kuajiriwa au kufanya kazi na consultant ambaye ni mzoefu!

Sipotoshi kaka nakuelimisha (maana mimi mwenyewe ni mtaalamu wa kile ninachokisema). Haijaandikwa popote kwenye sheria ama regulation kwamba ni lazima mtu awe na uzoefu ndipo awe tax consultant.... Hakuna andiko hilo kumuhusu tax consultant. Nadhani una miss interprete tu. Na wala hakuna andiko linalosema ili upate uzoefu ni lazima uajiriwe... Kitu kama hicho hakuna!!
Hebu soma Hapa:
Section 134 of the Income Tax Act, 2004

134.-(1) A person shall not (other than as an employee) in return for a payment practice or hold out to be an income tax consultant unless the person is an approved tax consultant.
(2) Approved tax consultants shall be those persons as approved by the Commissioner on such terms and conditions as may be prescribed in the Regulations.
(3) An approved Tax Consultant who knowingly or recklessly, aids, abets, conceals or induces a taxpayer to file a misleading or fraudulent statement commits an offence under this Act".

Hebu soma na regulation yake:
Regulation 37 to the Income Tax Act, 2004
37(1) Individuals meeting the following conditions may apply to the Commissioner in prescibed form and attaching the prescribed fee for approval as Tax Consultant for the purposes of this Act.
(a) an individual holding one of the following academic qualifications-
(i) a degree in Accountancy, Fianance, Financial Management, Commerce, Economics or Laws awarded by any University or other recognised Institution of higher learning; or
(ii) a postgraduate diploma in Tax Management or equivalent qualification as may be recognized by the Commissioner for the purposes ofthis paragraph; o
(b) a practitioner who is duly registered under the auditors and Accountants (Registration) Act, 1972

37(2) Subject to paragraph (4) the Commissioner shall assess applications made under paragraph (1) of this regulation and, if satisfied that the person is of good character and has sufficient knowledge and experience with respect to matters arising under the Act, may approve and register the person as Tax Consultant for the purposes of this act and issue the person with a certificate to that effect.
37(3) For the purpose of assessing a person under paragraph (2) of this regulation the Commissioner may require the applicant to take an examination or other form of assessment.
37(4) The Commissioner shall not approve an individual as a Tax Consultant if the indidual has convicted of (a) a criminal offence carrying a maximum penalty of a fine of not less than shillings 500,000 or imprisonment, or (b) gross misconduct
Unaona mkuu..... Uzoefu haujatajwa kwenye sheria wala regulation. Kama uzoefu ungetakiwa wangetaja idadi ya miaka ya uzoefu. Sheria imetaja kiwango cha elimu tu na imesisitiza hapo. Na ndo maana sheria imetaka watu wanaoomba kuwa Tax Consultants wafanye mtihani na wakifaulu ndo wnapewa certificate ya kuwakubalia kufanya kazi hiyo. Great thinking!!!! Hebu jiulize swali ikiwa unauzoefu kwa nini wanataka ufanye mitihani??? Na je ikiwa kama una uzoefu wa miaka mingi sana kisha ukapewa mtihani na ukafeli inakuwaje hapo????
Jioni njema kama una swali zaidi ni-PM.

 
Mkuu Malyenge asante kwa kutuwekea nukuu ya sheria husika. Je hiyo regulation 37(2) ina maana gani?

37(2) Subject to paragraph (4) the Commissioner shall assess applications made under paragraph (1) of this regulation and, if satisfied that the person is of good character and has sufficient knowledge and experience with respect to matters arising under the Act, mayapprove and register the person as Tax Consultant for the purposes of this act and issue the person with a certificate to that effect.

Btw, unaweza kutuwekea application form pia inayotumika kuomba kusajiliwa kama tax consultant?

Aidha, nakubaliana na wewe kuwa si lazima kuajiriwa au kufanya kazi chini ya mzoefu ili kupata uzoefu. Lakini naamini hiyo ni njia rahisi zaidi hasa kwa kazi za kitaaluma kama hiyo ya tax consultant (otherwise you end up trying to "re-invent the wheel").
 
Safi sana,vijana mmesoma na mmeelimika inapendeza sn,hoja zina mashiko na zinatolewa na rejea za kutosha!
 
Mkuu Malyenge asante kwa kutuwekea nukuu ya sheria husika. Je hiyo regulation 37(2) ina maana gani?



Btw, unaweza kutuwekea application form pia inayotumika kuomba kusajiliwa kama tax consultant?

Aidha, nakubaliana na wewe kuwa si lazima kuajiriwa au kufanya kazi chini ya mzoefu ili kupata uzoefu. Lakini naamini hiyo ni njia rahisi zaidi hasa kwa kazi za kitaaluma kama hiyo ya tax consultant (otherwise you end up trying to "re-invent the wheel").

Simama kwa miguu yako mwenyewe usiogope.... Hao wazee unaotaka kufanya nao kazi ili upate uzoefu wataku-frustrate mpaka ujisikie vibaya. Kitu muhimu ni kuwa na marketing skills, professionalism na customer care ya nguvu. Uta take off tu mkuu. Usipite njia tulizopitia sisi maana kutoka itakuchukuwa muda na gharama kubwa. Thank you for taking my advice. Form nita download kisha nitazitundika leo jion.
 
Mkuu Malyenge asante kwa kutuwekea nukuu ya sheria husika. Je hiyo regulation 37(2) ina maana gani?



Btw, unaweza kutuwekea application form pia inayotumika kuomba kusajiliwa kama tax consultant?

Aidha, nakubaliana na wewe kuwa si lazima kuajiriwa au kufanya kazi chini ya mzoefu ili kupata uzoefu. Lakini naamini hiyo ni njia rahisi zaidi hasa kwa kazi za kitaaluma kama hiyo ya tax consultant (otherwise you end up trying to "re-invent the wheel").

Form hizi hapa.
 

Attachments

  • APPICATION FORMS TO BE TAX CONSULTANT.doc
    63 KB · Views: 439
Mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili nachukua accounting and finance, nawza sana kuhusu ajira baada ya kumaliza chuo mwakani, ningependa mnisaidie kunijulisha hivi siku hizi mtu ukiwa na cpa bado inasaidia au ni useless maana nataka nikishamaliza masomo yangu nikachukue na cpa lakini nasikia watu wanaziponda hadi naanza kua na wasiwasi kwamba ni bure tu siku hizi, naomba majibu wadau

Wewe lazima utakuwa mwanafunzi wa UDOM
 
Mimi nilikuwa mpita njia hapa, nashukuru nimefaidika na ushauri wenu
 
nashukuru mkuu kwa syllabus,academic materials vp unaweza ukanisaidia kwa namna yoyote
 
<style>.ig-b- { display: inline-block; }
.ig-b- img { visibility: hidden; }
.ig-b-:hover { background-position: 0 -60px; } .ig-b-:active { background-position: 0 -120px; }
.ig-b-32 { width: 32px; height: 32px; background: url(//badges.instagram.com/static/images/ig-badge-sprite-32.png) no-repeat 0 0; } MEDIa only screen and (-webkit-min-device-pixel-ratio: 2), only screen and (min--moz-device-pixel-ratio: 2), only screen and (-o-min-device-pixel-ratio: 2 / 1), only screen and (min-device-pixel-ratio: 2), only screen and (min-resolution: 192dpi), only screen and (min-resolution: 2dppx) {
.ig-b-32 { background-image: url(//badges.instagram.com/static/images/ig-badge-sprite-32@2x.png); background-size: 60px 178px; } }</style>
<a href="http://instagram.com/vycaltellem?ref=badge" class="ig-b- ig-b-32"><img src="//badges.instagram.com/static/images/ig-badge-32.png" alt="Instagram" /></a>
 
Last edited by a moderator:
Kaichukue tu kwa faida yako ya baadae, Tena uwahi kabla hazijaisha. Wanagawa paleee NBAA karibu na Library ya Taifa.
Wahi mdau zipo chache utakosa ohooooooooooooooooooooo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom