Julius Mtatiro
Member
- Jun 20, 2009
- 45
- 225
mkuu mtatiro,ukweli ni kwamba nchi yetu inapitia mabadiliko,na sis vijana ndo engine ya mabadiliko haya,bahati nzuri kipindi upo chuoni nami nilikuwepo!kuna hoja ya kwamba upo cuf kama ajira,kwani kam,a ni mwana harakati wa kweli ungetizama uelekeo sahii!umeijibu kiujanjaujanja!kwamba we ni mjariamali,we umetaja mali zako!kabla ujakubali hicho cheo!unakiri kwamba cuf ulijipeleka,unakiri kwaba at the time unajiunga cuf,chadema ilikuwa vibrant!sasa kwa hili hukubaliani nami kuwa uliona hajira unayotafuta cuf ni muafaka zaid kwani kwingine kuna ugumu kidogo,walaji ni wengi?na kwa nini kama si ajira mbona hujaonyesha ni kiasi gani unapata kutokana na unaibu katibu mkuu!then tukachambua na kujua ukweli?
Ndugu yangu Luka,
Idea yako ni nzuri, lakini utambue kuwa sikufika chuo kikuu kutafuna fedha za walipa kodi ili baada ya hapo niwe mshabiki wa vyama vya siasa. Siku zote nimejifunza umuhimu wa kufanyia kila jambo utafiti. Sielewi Idea ya kugeuza wadhifa wa chama cha siasa kuwa ajira, sielewi hii kaka. Wakati napewa wadhifa wa ukurugenzi CUF, mkurugenzi alikuwa anapewa posho ya shs 280,000/- hii ina maana kuwa kwa CUF hatuajiri mtu, kila mtu anajitolea na kuna mikataba ya kujitolea. Kabla sijawa naibu katibu mkuu aliyekuwepo(mhe. Bashange) alijitolea kwa mwaka mzima na baadaye akakiomba chama akapumzike ajenge maisha ya familia yake ambayo ilianza kuyumba kiuchumi. Katika CUF naibu katibu mkuu huna access na pesa, pesa wanasimamia kurugenzi ya fedha tu. Wewe naibu katibu mkuu unakagua nini wamelipa na kama imekuwa sahihi baada ya makubaliano ya vikao. Kwa hiyo hakuna loophole ya kula hela ndani ya CUF na ndiyo maana hadi leo CUF ina rekodi nzuri ya masuala ya pesa, so siku rafiki yangu ukipewa unaibu ukadhani utakula pesa za CUF umeula wa chuya.
Jambo lingine ni kuwa, baada ya kumaliza chuo ningeweza kupata ajira nzuri katika makampuni kadhaa kama ningetaka, lakini niliona nikienda kufanya kazi ofisini sitakuwa na muda wa kufanya advocacy na kuifikia jamii pana zaidi, niliona malengo yangu ya kuelimisha wananchi wengi na kuwatetea yatapotea.
Mwisho napenda kukujulisha kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF kwa viwango vya sasa anapokea POSHO ya tzs 525,000 kwa mwezi. Kwa hiyo unaposema nilijiunga CUF ili kupata ajira that mean 525,000/- kwangu ndiyo fadhila. Hapa nilipo nina digrii moja, nina advanced diploma moja na ninasoma shahada ya pili.