Coco Beach siku ya Pasaka (Picha)

Halmashauri ya jiji wana jua kukamata wamachinga tu kuendeleza fukwe hawataki. Wanatakiwa wawe na mshauri wa biashara aliyeenda shule vizuri. Beach zetu kuna potential kubwa ya kuzigeuza business centres bila kuchafua mazingira. Waamke! nyambafu
 
Wewe bwana,....khaaaa.Lazima ututwangie za kizalendo tu.
Haya basi Zenji mwisho na tutaiga.Meanwhile how do you
say that in English...LOL!!!!!:):):)
Tatizo lingine huko Bara, watu wanakumbuka maeneo kama hayo wakati wa sikukuu tu! Ilhali Zenj kila siku zipo busy na sikukuu ndio kabisa! Mbaya zaidi inatia aibu kwa Jiji hilo kuwa na kabeach kamoja tu kanakovuta watu!
 
Tatizo lingine huko Bara, watu wanakumbuka maeneo kama hayo wakati wa sikukuu tu! Ilhali Zenj kila siku zipo busy na sikukuu ndio kabisa! Mbaya zaidi inatia aibu kwa Jiji hilo kuwa na kabeach kamoja tu kanakovuta watu!

Say that in English....
 
Say that in English....
avatar253_2.gif

:D :D
 
Hao jamaa inakuwa kama wamekaa wanapunga upepo pembeni ya bonge la dimbwi flani la maji! Halafu cheki jamaa walivyochoka...yaani choka mbaya sana. Halafu beach gani hii yenye vichaka...angalia hiyo picha ya kwanza hapo juu juu kwenye picha...hiyo ni miti au vichaka?

Halafu mbona msongamano wa watu ni mkubwa hivyo? Au ni mimi tu macho yangu?

Nadhani mjadala hapa ni namna gani Beach zetu zingeweza kufanywa bora zaidi kwa watu kupumzika na kupunga upepo kuliko kuchoka kwa wanaopunga upepo beach. Nadhani tunawakosea haki watu kuwaambia wamechoka katika hoja hii, kwani kutengeneza beach bora hakutaondoa uchovu wa hawa jamaa, let's not mix the two scenarios.
 
Nadhani mjadala hapa ni namna gani Beach zetu zingeweza kufanywa bora zaidi kwa watu kupumzika na kupunga upepo kuliko kuchoka kwa wanaopunga upepo beach. Nadhani tunawakosea haki watu kuwaambia wamechoka katika hoja hii, kwani kutengeneza beach bora hakutaondoa uchovu wa hawa jamaa, let's not mix the two scenarios.

Mpiga filimbi,shida ni kitu kimbaya sana na madhara yake kisaikolojia pia hayasemeki. Hali ya wananchi kiuchumi ndicho ninachozungumzia pale ninapomention kuchoka kwa wananchi,this time with reference to the picture. Kwasababu kabla mwananchi hajafikiria kwenda beach kupumzika,matatizo na shida wanavyokumbana navyo,mara nyingi hata uwezo wa kupata milo at least miwili kwa siku ni tabu.

Sisi ni wanadamu,na tuna adapt kutokana na mazingira na kama umeshawahi kusafiri mara kwa mara utajua hilo kama wewe ni mtu wa kujifunza.

Kimsingi, kama wananchi hao wangekuwa na hali nzuri ya kiuchumi,basi na ufahamu wao ungekuwa wa tofauti kidogo,tatizo la ku adapt hapa linakuja kwani wengi wamezoea shida na kwasababu upeo wao uko limited,basi ni vigumu kwa wao kutaka mabadiliko.

Ili uweze kufanya biashara ambayo ni sustainable,ni lazima kuwe na consumers,kwetu hapo sisi kwasababu ya umasikini,watu wa biashara huwa wanaprefer watalii foreigners zaidi kwasababu ya foreign currency na uwezo wa watalii hao kuspend.....Na wasipokuja watalii hapo uchumi "Unayumba" Kwani hata Mh Rais atapiga kelele.. Kutokana na hayo,ni vigumu sana kupata viongozi watakaokuwa na uzalendo enough kuwasaidia wananchi hao waliochoka bila ya kuwa na maslahi binafsi.

Mwanakijiji hapo Detroti eneo la Highland park ni mfano halisi wa kile kinachoendelea hapo bongo na kwenye nchi za Africa kwa ujumla. Eneo hilo ambalo community ni predominantly black,wanajamii hao walipoteza kazi zao na hivyo huduma za kijamii zikaanza kupungua,downsizing ikaanza na layoffs kwa mwendo wa mbele. Kuna documentary inayoitwa The water front inayohusiana na tukio hilo,kwani idara ya maji iliathirika na wananchi hao kuanziwa kukatiwa maji mara baada ya kushindwa kullipa bills za maji zilifikia maelfu kwa maelfu kwa mwezi,kwa kawaida hapa USA especially hapa nilipo bills hizo hurange from 20 bucks to 50.

Detroit tunajua imezungukwa na maji,lakini kabla maji hayo hayajatumika ni lazima yawe trated kwenye plant,na hivyo basi maji hayo yalibinafshwa na hivyo kupeleka mgogoro kwenye jamii hiyo,wanajamii hao walikataa ubinafsihswaji wa maji hayo na city council ikabakia na responsibilit hiyo,haijajulikana ni kwanini bills hizo zilipanda lakini habari ndiyo hiyo,kuwa ukibinafsisha watu wanataka kumake profits sometimes beyond means...Wananchi hao walikuja juu,ila hapo ndipo kwenye a thin line between socialism,capitalism and realism....Ukweli ni kwamba socialism inaprevail ila wanazuoni wanataka kuimodify kwani hilo neno ndio tabu, lakini ukweli ni kwamba socialism iko well practiced hapa Marekani. Na mtu asiwadanganye wananchi,serikali bado ina jukumu la kuwaletea wananchi maendeleo in any means necessary na si kuwadanganya kuwa sasa ni capitalism na hivyo kivyao vyao....Na kwasababu matatizo yanayowakabili wananchi ni ya kimsingi kama chakula nk,ni vigumu kufikia levele ya kudai beach nzuri ya kupumzikia, at least huwa wanashiba pilau kubwa wakati wa sikukuu na hivyo kupata fursa ya kupunga upepo.

Kina Kibunango wanadai huko Zenji beach ni all the time,nadhani niliandika something similar to that pale niliposema wananchi hao hawajui matumizi yake na hivyo kuwa shida kwa wao kudai patengenezwe.

Wenzetu wa magharibi walipoanza kusafiri walileta maendeleo kwao,tena watu huwa hata hatujiulizi,walichukua si tu rasilimali,bali pia "Rasilimaliwatu" Sisi ndio tunaondosha kwetu,hapo ndio unapojua kweli maana halisi ya uzalendo,wananchi walio wengi hawafahamu,hawajui correlation ya kile wanachojua viongozi wao vs kile wanachotakiwa kuwafanyia wananchi kwasababu wananchi wenyewe hawana idea ya nini wanataka kifanyike..Na kisaikolojia viongozi ndio wanagandamizia kabisa kwenye fikra za wadanganyika hao kuwa SISI NI MASIKINI, bakuli every now and then whenever wanaposafiri,hakuna kuiga vitendo na mifano ya maendeleo ya kuwanufaisha wananchi,ni bakuli tuu.

Unaona serikali ya Obama inataka sheria ipitishwe kuhusu ujenzi wa nyumba ili zifikie viwango vilivyowekwa ili ziwe more energy efficient na hivyo kupunguza matumizi/gharama za heat,air condition nk.
Serikali ni lazima ibuni mipango ambayo itawasaidia wananchi hata kama wananchi hao hawajui ama hawana habari na manufaa hayo kwani manufaa hayo yatawageuza kisaikolojia na kuwafanya wawe wa wa kupenda maendeleo....Wananchi wakiwezeshwa uvhumi ukiwa mzuri everything else falls on its part.


Mwanakijiji bado tunasubiri makala hiyo na kama imeshatoka tufahamishane.

Mpiga filimbi,huwezi kukwepa kuzungumzia hali halisi ya wananchi hao na kuzungumzia beach peke yake,kuna correlation bila shaka.
 
hali hii huwa inajirudia wakati wa siku kuu zozote kubwa za kidini. Picha hizi ni kutoka kwa Mroki za siku ya ya Pasaka iliyopita. Wakati wa Dar ambao wamezoea kinyaa wanaendelea kuwachagua watu wale wale ambao wameshindwa kutafuta suluhisho la ukosefu wa maeneo ya kupumzika lakini maeneo ya mahoteli ya kitalii yanapatikana kwa urahisi!

Nimechambua hili katika makala yangu mojawapo ya kesho nadhani iko Tanzania Daima au MwanaHalisi.


This is a business opportunity; wawekezaji wa ndani mko wapi? Ngoja niwapigie simu washirika!
 
na nyie watu wa majuu mnaboa.....nyie mnabweteka makalio yenu huko mnataka nani awatengenezee beach zenu?
pesa hamtumi kazi kufanya sherehe kila siku.....tumeni fedha muone kama beach haitakuwa safi sio kukandia kila kitu.....

iteni fundrising za maana sio za sherehe.....mie nashangaa sana
sijawahi kuona hapa walio majuu mnaitisha fundrising ya kusaidia kujenga shule,hospital au other social service....ila naona mnaitishana michango ya madisco....

ionyesheni serikali mfano sio kuandika makala ndeeeeeeeeeeefu JF na kwenye magazeti...tunataka vitendo...ebo

wewe mwanakajiji tumeshachoka na makala zako tunataka vitendo......
 
ionyesheni serikali mfano sio kuandika makala ndeeeeeeeeeeefu JF na kwenye magazeti...tunataka vitendo...ebo

Ebo wewe na familia yako na ukoo wako!

wewe mwanakajiji tumeshachoka na makala zako tunataka vitendo......

ninachofanya mimi wewe hata kukiwaza huwezi! huna mpango!
 
cocobeach2.jpg

Hapa wamendeza kweli kweli ,tatizo wengi wenu mmezoea kuona mkusanyiko wa aina huu wakiwa ni wazungu watupu ndio mnaona hawakupendeza ila ,sijui ile kujianika kama tayari wameanza ingewasaidia hawa wapiga chabo hapa chini.
cocobeach.jpg
 
Mzee Mwanakijiji,

Tusiishie kulalamika tu, tuwe mbele kuchukua hatua na kuonyesha mifano kwa kufanya kweli yale ambayo CCM na serikali yao wanashindwa kufanya. Maeneo ya wazi yanachukuliwa, lakini wasomi, wanasheria wanashindwa hata kwenda mahakamani na kupinga vitu simple kama hivyo. Sisi wengine tunashindwa kuchangia hata harakati kama hizo. Baadaye sisi wenyewe tutakuwa viongozi na kuendeleza ujinga huo huo.
Kwa maneno mengine huu ni wakati muafaka kwa wananchi kusimama kidete na kujipangia maendeleo wanayoyataka badala ya kusubiri kupangiwa na serikali, ni wakati muafaka kwa wananchi kuondoa kero zao wao wenyewe badala ya kusubiri kero hizo zipate kiupambele toka serikalini.

Kwa maneno machache ili kuweza kuwa na mambo endelevu katika jamii yetu, hakuna budi kwa wanajamii hao kushiriki moja kwa moja katika mipango na utekelezaji wake badala ya kusubiri kupangiwa na kutekelezewa na serikali.
 
Kwa maneno mengine huu ni wakati muafaka kwa wananchi kusimama kidete na kujipangia maendeleo wanayoyataka badala ya kusubiri kupangiwa na serikali, ni wakati muafaka kwa wananchi kuondoa kero zao wao wenyewe badala ya kiupambelekusubiri kero hizo zipate toka serikalini.

Kwa maneno machache ili kuweza kuwa na mambo endelevu katika jamii yetu, hakuna budi kwa wanajamii hao kushiriki moja kwa moja katika mipango na utekelezaji wake badala ya kusubiri kupangiwa na kutekelezewa na serikali.
swadakta.......
 
Back
Top Bottom