Coco Beach siku ya Pasaka (Picha)

Kipimo cha ubaya ni uzuri, kwa waliokulia Dar, kwao Dar ni safi hadi pale watakapokwenda Moshi ndipo watagundua wanaishi mji mchafu na upo msafi hapa Tanzania. Dhana ya walio nje warudi kupambana na wasitoe mawazo ni hafifu kwani wao wameona nini tofauti na wanajaribu kuchangia.Kuchangia si lazima iwe pesa mawazo ni mchango mzuri sana. Lakini pia wamewahi kuchangia kwa hali na mali mambo mengi tusiyoyajua wengine kwa upungufu wa kutambua au habari.

Mavazi na matumizi ya beach ni jambo la mtu binafsi, mimi napenda sana beach lakini ukiniweka ndani ya karai la maji naweza kufa ninavyoogopa maji. Hii hainuzuii kubeba gazeti au kitabu changu na kwenda mahali tulivu na upepo mwanana kuburudika.
Napenda kwenda muziki lakini sipendi kucheza muziki zaidi ya kuangalia,kusikiliza na kuchanganyika na jamaa, je hizo ni sababu za kusema sijui matumizi ya kumbi za muziki au beach!. Muhimu ni mtu anajisikiaje akiwa katika eneo analolitaka na lililoandaliwa vema.

Maeneo ya burudani ni muhimu sana, katika miji yote mizuri dunia kila kata ina Park na sehemu za kuchezea wakubwa na wadogo, si siku za sikukuu bali kila siku. Dar es Salaam, park ya mnazi mmoja ni ya 'jeshi', eneo kama kinondoni na Temeke hakuna, angalia vurumai sinza hadi mwenge n.k. Wakati wa siku kuu japo basi nimtoe kijana akale 'shkrimu' kwa hiyo siku moja, dah! sijui ni wapi kama si kusimama dukani na baada ya hapo siku imekwisha. Umasikini hauna maana ya kushindwa kupata raha ya asili, au kufanya kile unachoweza japo kukupa tabasamu.

Uzembe wa beach ya coco ni zao la wananchi kwanza, kwasababu ndio wanachagua viongozi kwa rangi za vyama na si kwa maendeleo. Wakazi wa Dar wangewahoji madiwani waliopita wamefanya nini cha kuinua au kuboresha maisha yao miaka 5 iliyopita? na wakati wa kampeni walitakiwa waulize sera za diwani kuhusu mambo kama elimu, afya, burdani n.k.
Hili la beach ni kazi ya jiji lakini utashangaaa meya kila siku yupo magazetini akizundua vinywaji vya bia. Ujenzi wa beach ni mpango wa jiji kuweka taratibu zitakazomwezesha mwekezaji kutoa huduma na kupata faida bila kuwachaji wananchi(inawezekana) na wakati huo jiji linapata kodi "Quid pro quo"

Kazi ya serikali ni kusimamia sera na mipango ikiwa ni pamoja na halmashauri za miji na majiji. Tatizo la Tanzania si viongozi wasiojua, bali ni viongozi wasio 'innovative'. Kiongozi akiwa ofisini anafanya kazi kama ya yule aliyemkuta bila kubuni mbinu mbadala. Hakuna kiongozi anayetaka kuacha alama'mark', na ni hivyo hata kwa wananchi, kuna wakati kila mtaa una baa, wakati wa saloon. Hatuna innovation kuwa watu wakifuga kuku basi anzisha ka mradi ka chakula cha kuku n.k au tray za mayai n.k ni mifano tu tusivyo innovative.

Tatizo linalojadiliwa la beach ya coco ni muhimu ili ku 'set tone' ya jinsi gani tunaweza isaidia jamii yetu si kwa hili tu hata mengine. Tutavia akili tukidhani kila siku ni siasa tu, na tutakuwa wazembe tukidhani yapo mafanikio yasiyoanza na fikra na kwamba mpiganaji ni yule tu aliye msituni na sio mchora ramani au muongoza rada.
Coco beach ni uzembe wa Wananchi waliochagua madiwani na mameya wazembe wanaolelewa na serikali isiyo na ubunifu. Tutakuwa sehemu ya uzembe huu kama hatutasema, elekeza, pendekeza au kufanya. Hata mbuyu ulianza kama mchicha.
 
mimi mwenzenu ni mmbishi kidogo kuilaumu serikali tuuu wakati saa zingine ni taasisi zake ndizo zinazotuangusha!

Kuna nani ameshawahi kutembelea bwalo la magereza kule ukonga? Wafungwa wametengeneza mazingira poa sana, bwalo zuri sana na magereza taarabu wanatumbuiza kule na siku hizi naona hata video nyingi wanashuti kule. Kwa nini wazee wa jiji wasitumie magereza, yaani wafungwa, kutengeneza some of the mazingira na open parks in dar and elsewhere in tanzania? Tunaambiwa kuna msongamano wa petty thieves in our jails - why not start chain gangs and put these petty offenders to work in cleaning up or karabatiing open spaces and parks, neighborhoods, roads, schools etc? Nimekulia oysterbay and kwa haraka haraka tu kuna parks tatu in dire needs to be create excellent rehabilitation - at the end of karume road coming from oysterbay beach as if going to ali bin said; at the end of msasani road pale tulikokuwa tunaosha mbwa, na mbele yake kidogo on kenyatta drive. I think these can be turned into jogging paths, put a couple of miniature football goalposts, and a couple of basketball, volleyball and even tennis courts, contract one of the portable toilet companies for their service-for-a-fee and if it allows have a couple of parking spots for a fee - these fees will then be used to pay for the lights and piped water. All this kimbisa can get from our vast prison population labor.

You can also build a jogging and bicycle from the lighthouse on one end of toure drive all the way to coco beach and then from golden tulip all the way to see cliff hotel - better yet: From golden tulip to sea cliff you can build a skateboard/rollerblade path and/or park, put some benches facing the ocean and try and preserve the natural vegetation.

Sorry, just wondering aloud...........
mkuu ni pm bado atujachelewa
 
Mie ssioni haja ya serikali kupoteza pesa, eti kuweka mazingira safi beach! Sasa hiyo beach unamtengenezea nani? Cheki hao walioko hapo, haaaa bichi wanafanya nini..... wapi ulishaona watu beach na mijigwanda michafuu, kandambili rangi tofauti. halfu mwisho wa siku kaangalie... uchafuu umetapakaa kila kona hapo. Tatizo raia bado sana wako nyuma. Labda ndo umasikini unachangia.

Lakini laazima sote tukiri kuwa Watanzania sote bado hatujawa na utamaduni wa usafi. Nakumbuka kunakuwapo na mapipa ya takataka mitaani, lakini hayakai hata siku mbili, watu wanayapiga teke. Watu wanaptupa taka nje ya pipa. na wengine wanayapeleka makwao. Badala ya kutupa taka kwenye sehemu mmoja watu wanatuma kwenye mtaro wa maji taka. Mwisho wa siku kero ikizidi tunailaumu CCM.

nakubaliana na wewe... but sio kwenye RED!.. watanzania waliowengi ni maskini.. ni haki yao kwenda maeneo yalio wazi. au mkuu ulitaka uone watu walishusha suruali.. wamevaa chupi... wamegeuza kofia nyuma mbele mbele nyuma...
 
SILVER SAND PIC.jpg







Inasikitisha sana, kwa wale ambao wamebahatika kupitai huku ufukwe wa SILVER SAND wanaweza kujonea jinsi ambavyo Serikai yao ilivyoamua kutelekeza rasilimali muhimu za nchi hii. Silver Sand Hotel ambayo ipo kati ufukwe mpana na mzuri kabisa imekuwa ni gofu, ufukwe mchafu japo kuwa wamiliki wake ni shirika la umma lenye ruzuku lukuki.
SILVER SAND PIC.jpg SILVER SAND PIC.jpg
 
Ushamba ni kazi, wabongo wamekariri upuuzi wa wanasiasa mpaka hawajui nguo za beach ni zipi na madhumuni ya kwenda beach ni yapi! Wengi utafikiri wako uwanjani wana angalia tamasha la michezo kumbe wako beach. Beach yenyewe chafu na concrete sijui za nini!
 
Kwa mfano huku kwa jaluo,katika miji mingi kuna adopt a highway programme.Yaani,shule,makampuni,vyama na institutions mbali mbali zina-adopt a pice of land arruond that highway na kuzisafisha!..bure!! hapo dar manzese kuna daraja la watu kupitiza barbara lakini bado watu wanakufa kwa kugongwa na magari!!
Hapo CDM lazima watampiga madongo JK!!...
 
Wakishazungushia uzio tukiingia tunapigwa kiberiti na bado wenye hela zao wanaendelea kupeta tu kwa madaha mtaani! Siku moja tutaamka tu na i swear wenye viti vyao ofisi zitakua chungu!
 
hali hii huwa inajirudia wakati wa siku kuu zozote kubwa za kidini. Picha hizi ni kutoka kwa Mroki za siku ya ya Pasaka iliyopita. Wakati wa Dar ambao wamezoea kinyaa wanaendelea kuwachagua watu wale wale ambao wameshindwa kutafuta suluhisho la ukosefu wa maeneo ya kupumzika lakini maeneo ya mahoteli ya kitalii yanapatikana kwa urahisi!

Nimechambua hili katika makala yangu mojawapo ya kesho nadhani iko Tanzania Daima au MwanaHalisi.

cocobeach.jpg


cocobeach2.jpg

Du beach za bongo bwana jamaa walivyokaa utadhani wavuvi wa samaki wanasubri kwenda kutega
 
hapo beach ni pasafi sana ukiringanisha na sehemu wanazoishi wananchi wengi unaowaona hapo. ukizungukia DSM katika mitaa mingi utangundua hilo.
suala la uchafu na mazingira lazima litizamwe katika pande zote mbili. wananchi na wanaowaongoza.

kwa DSM na mikoa mingine ya pwani contribution ya uchafu inayotokana na negligence ya wenyeji ni kubwa sana. huwa naona kama mikoa ya bara ina nafuu kidogo in terms of wenyeji kujiweka katika mazingira safi.
kupambana na uchafu ni tatizo kubwa kuliko watu wanavyofikiria sie tunaoishi uswahilini tunalijua hilo. ni kero kubwa sana
katika mazingira haya lazima Wananchi ndiyo waisukume serikali ndiyo mambo yataenda otherwise everybody is comfortable kwenye mazingira hayo. sidhani kama ukifanya utafiti hapo utapata mtu atakayesema ni pachafu
 
Kama hata majengo ya Ikulu na makazi ya maafisa wa kuu wa Serikali tulirithi kwa Mkoloni, mnadhani kunaweza kuwa na akili yeyeote ya kuendeleza fukwe?...
 
Back
Top Bottom