Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,047
- 20,411
Watu wanapokwenda beach, wasichana wengi wanapenda kuogelea na wengi wao hawajui, hivyo wale Beach Boys wanaokodisha maboya huingia nao kwenye maji kwa lengo la kuwafundisha.
Kinachofuata sasa, Beach Boys hupeleka boya hadi kwenye kina kirefu, wakifika huko kijana huomba apewe penzi/mzigo {"k"} huku akimtishia mdada kuwa akigoma anamuachia afe.
Mdada akijifanya mbishi anazamishwa, anakunwya maji kidogo kisha anaibuliwa, akishaona mlango wa kuzimu anakubali kiulainii. Kwa staili hii wadada wengi wamepewa mimba na kuambukizwa magonjwa.
Mmoja wa mabinti aliyewahi kufanyiwa mchezo huo aliyeomba hifadhi ya jina lake alidai kuwa, kuna wakati alifika na wenzake kwa lengo la kufundishwa kuogelea lakini kilichompata hatasahau.
“Mimi kila wakati nikienda kule beach natamani sana kuogelea lakini nilikuwa siwezi ndo nikaambiwa wale vijana wanaokodisha yale maboya ukitaka wanakufundisha.
“Siku moja nikaenda pale, nikaongea na kijana mmoja ambaye alikubali kunifundisha kwa malipo ya shilingi elfu tano. Wakati ananifundisha akawa ananipeleka kwenye sehemu yenye maji mengi, tukaenda mbali sana ambako nisingeweza kurudi peke yangu.
“Huko akaanza kunitaka nimpe penzi huku akisema hata nisipomlipa, kwa kweli nilichangayikiwa. Wakati najifikiria alishaanza kunichezea kisha akanibaka,” alidai binti huyo.
Pia soma: Waziri Gwajima: Kuna haja ya kuweka mfumo maalumu wa kuwatambua "Beach Boys" maeneo ya Fukwe