Clouds na Matusi ya Lusinde inamaanisha Nini?

Kama uliwasilkiliza vema walikuwa wakishangilia kwa kubeza na kuonyesha ujinga wa Mh. Lusinde. Lo! aibu yake na aibu yao pia.
 
Nimesikia asubuhi hii Clouds FM wakirudia sehemu ya hotuba ya matusi ya Lusinde redioni huku watangazaji wakishangilia. Jee hii inamaanisha nini katika jamii? Maadili ya utangazaji yanasemaje kuhusu kitendo kama hiki?

Kudadadeki zao!!!!!!!
 
Lakini mbona huyu mheshimiwa alikuwa Member - National Executive Board wa Chadema ina maana mlipompa hiyo nafasi hamkujua kama ana matatizo myasemayo?
 
Clouds tusiwaseme wanawafikishia ujumbe watanzania kuwa ni aina gani ya viongozi ambao tumewapa dhamana! Wahuni na washenzi!
Clouds hawana makosa! Wanasikilizwa karibu nchi nzima hivyo wametumia nafasi yao kufikisha ujumbe! Mia nina wasiwasi na aliyekuwa akiukana kama ni mzima au la!

Note: Tuwashukuru clouds, tusiwabeze hata kama wanacheka ila ni kejeli kwa lusinde na waliomtuma
 
Lakini mbona huyu mheshimiwa alikuwa Member - National Executive Board wa Chadema ina maana mlipompa hiyo nafasi hamkujua kama ana matatizo myasemayo?

Tulijua ndo maana tukamnyanganya hiyo nafasi akaamua kurudi chichiem
 
Nadhani wanamdhalilisha Lusinde zaid, kwa sasa watanzania takribani wote wamepata kuyafahamu matusi yake hivyo kupima uwezo wake ki akili
 
si kama walikuwa wanashangilia...walikuwa wanamsanifu/wanashangaa/hawakupendezwa na mbunge kutukana....ukiwachekju ju utasema walkuwa wanashangilia bt not.....

dah mbaba anatukana yule hatar...
Daa ulikuwa wapi Rose jamani wakati tunashangilia jana. hujaonekana siku nyingi humu ndani
 
Nimesikia asubuhi hii Clouds FM wakirudia sehemu ya hotuba ya matusi ya Lusinde redioni huku watangazaji wakishangilia. Jee hii inamaanisha nini katika jamii? Maadili ya utangazaji yanasemaje kuhusu kitendo kama hiki?

Chakaza, Kama CCM hawakumkemea CLOUDS FM ulitaka wafanye nini? Kwa hili Clouds FM nawapa big-up kwani wanatujuvya jinsi viongozi wetu wanavyothubutu kutukana hadharani. Umewahi kuhudhhuria mikutanao ya kampeni na mchanganyiko wa rika ya wahudhuriaje. Kuficha ukweli ... kumwambia mfalme amevaa suti wakati yuko uchi haifai jamani!
 
JF ina wanasheria nguli kibao. Najua kuwa kutukana ni kosa. Naomba elimu, hivi Lusinde hawezi kushitakiwa criminally kwa kosa la kutukana matusi kama ya Dr Slaa kufukuzwa upadre kwa wizi wa sadaka na kuwapa mimba wanakwaya? Sheria za Tanzania zinaruhusu private prosecutors? Au mpaka Feleshi akubali. Yaweza kuwa njia ya kuwafanya watawala wetu kuwajibika.
 
Lakini mbona huyu mheshimiwa alikuwa Member - National Executive Board wa Chadema ina maana mlipompa hiyo nafasi hamkujua kama ana matatizo myasemayo?

Ndo maana hakukawizwa, walipomshtukia tu kuwa amesoma kile chuo cha Matusi.com wakambwaga akarudi kwao CCM.
 
Ukizingatia kuwa matusi yaliyotolewa na huyo mh yalilenga watu binafsi sio vizuri kuendelea kuyarusha hewani. Hasa kwa kuzingatia kuwa Clouds Radio inasikilizwa na watu wa rika zote, kwa hiyo ni aibu kuendelea kurudia matusi hayo. Watangazaji wafuate maadili ya kazi yao. Walioshindwa wameonekana tugange yajayo!
 
Nadhani baadhi ya watangazaji wana mawazo ya kihuni tu, mtu mzima na busara zako hali ya hewa ikichafuliwa kama alivyofanya Lusinde na wewe ukaipaka rangi mi nakuona kama zezeta tu.
 
Back
Top Bottom