Chuo Kikuu bora TZ ni kipi kwa kusomea Uhasibu au Biashara? - ni UDSM, Mzumbe au IFM?

Ha ha ha ha ha ha ha nilijua ipo cku watu watatukanana humu ndani kisa majigambo na kuponda vyuo vya wengine ha ha ha ha sisi kimya na chuo kikuu chetu

• Thanks
Reactions: fox

ila we dogo ni ****** kweli, kila ck kweny topic za vyuo nakuona unakashifu vyuo hii katika vyuo tunaangalia output quality o input quality, kwa sababu c kila m2 mweny div 1 form six ameipata kwa uhalali, chunga kauli zako kwa kukandia vyuo vya wa2 ukimaanisha we ndo bora. Mara aia, tia, ifm, udom, muccobs, saut, tumaini unaviona sio vyuo, nmekufuatilia sana kama vile unasoma havard university, ****** sana, au we ndo wa kwanza kufika chuo nin acha usenge, kazi hawalipi mishahara kulingana na vyuo. Usenge huo .
pole sana, huijui vizuri UDSM nadhan. Nashukuru sina tabia hizo. UDBS iko poa kwa biashara, ila kukomaa kwa sana kwani complications nyingi sana pale.

Mzumbe>uhasibu na utawala

Udsm>sheria

Saut>commnction

Udom>kila takataka

SUA=Kilimo,ila mkuu hapo kwenye UDOM umeniacha hoi nacheka mpaka mbavu zinauma ha ha ha ha ha ha ha ha ha

Mwambie uncle wako ampeleka mtoto wake akarudie kidato cha kwanza shule za kata ndo atakomaa akili vizuri!

Kwa namna nilivyoona comments za wadau, wengi wanaitaja IFM, kwa kigezo hicho nakushauri mpeleke IFM kijana wako.
Shukrani jazeera!

IAA hamna chabo wala kupanga timu, siku ya pepa unakuta namba yako kwenye dawati unakufa mwenyewe.. tofauti na vyuo vingine wanafunzi wanajipanga jinsi ya kukaa watakavyo

Mbona unachanganya maada,kwani vyuo vikuu viko vingapi ?chuo kikuu kipo kimoja tu udsm na sasa udom hivyo vingine sio vyuo vikuu.wewe nenda mlimani kasome acha kujichanganya.

Mie naomba nikupatie ushauri wa kitaaluma zaidi ya habari za kusikia. Vyuo vyote ulivyotaja hapo juu vina faida na hasara zake. Pia inategemea unataka kijana wako asomee kitu gani kama ni economics, accounting , finance, econometrics, business management, management etc.

Mzumbe - kiukweli sio chuo kinachofaa kwani hakina waalimu na kinachukua walimu wake wengi IFM , na UDSM. Na sababu kubwa ni baada ya scandal ile ya vyeti feki wengi wametimka au wameamua kurudi tena shule wakasome vizuri. Ila faida yake ni kwamba gharama za ada yao ni chini kidogo kulinganisha na vyuo vyengine kama kijana wako unamlipia ada. Pia admission competition ni ndogo kulinganisha na IFM na UDSM hivyo basi unaweza kuwa na uhakika wa kupata admission.

IFM - hiki ni tertiary university ijapokuwa miaka ya karibuni wameanza kuwa wanatoa degree. IFM ni tertiary university but wameexcell vizuri sana katika sekta ya Accounting, Finance na Banking. Hivyo kijana wako ukitaka asomee sekta hizo ni bora nakushauri aende IFM kulinganisha vyuo vyote hapo hasa kwasababu sasa hivi wataalamu wengi wa finance, accounting wako IFM. Tatizo la IFM ni ada yake aghali sana kulinganisha na mzumbe sijui UDSM? Pia IFM vijana wanakuwa hawakai darasani hasa akina dada kutwa wako mitaani. Vile vile waalimu wa pale IFM kutwa wapo kwenye consultancy, research na masemina wana muda mchache wa kufundisha hilo linachangia kuleta mapungufu kwenye ufundishaji.

UDSM - Ni chuo kizuri sana kwa mtu anayekusudia kusomea Economics, Econometrics kwani kuna wataalamu waliobobea pale. Hata hivyo nao wanatatizo sawa na IFM waalimu kutwa wapo katika consultancy, research na masemina. Hivyo kijana wako kama ni kilaza anaweza kusumbuka .

SUA - Kama alivyosema mtu mmoja wazuri sana katika research na economics. Ila wanapungufu katika sekta ya decision making, accounting, finance. Kwahiyo kama unataka kijana wako awe mchumi SUA kuzuri, kama UDSM.

Zanzibar University- Ni kweli hichi ni chuo kizuri ila hakina jina. Na wanafundisha vizuri sana na wanafunzi wengi wanaenjoy pale na ada sio kubwa sana. Tatizo lake liko katika cheti (kwasababu ni chuo cha kiislamu), pia kuna tatizo la kimazingira maana kipo zanzibar, vilevile waalimu wake wengi ni kutoka nje ya nchi sasa sielewi ufanisi wao but overall vijana wamesoma pale wamemaliza na wamepata ajira.

Ndugu Analysis yako haijazingatia protocal, Huo ushauri wako umekua Bias na kutoa kipaumbele katika chuo cha IFM. Kwa ufupi UDSM ni wazuri kwa Biashara thats y wanaajiriwa pamoja na perfomance zao za chini yani lower 2nd compared to other universites I mean Mzumbe and IFM ambao inabidi wawe na upper second kucompete na mwanafunzi wa UDSM.

Pili Mzumbe pia ni chuo Kizuri kwenye Commerce especially Bachelor ya Account and Finance imewapa reputation kubwa as well as long period of practical training which covers the whole semister thus giving them an added advantage in Job Market.

Nakushauri huyo Mtu mpeleke UDSM au Mzumbe pia IFM kama jamaa anavyodai but hayo masomo aliyoyataja pia vyuo vingine viko poa tu.
Bila kusahau Mzumbe ina exemption katika Mitihani ya ACCA kama atachukua Acc Finance. Atatakiwa kufanya mitihani 7. Kwa UDSM na IFM mitihani 10.

Ok. ni wazi kwamba kuna vigezo vingi. Hivyo tabia ya mtoto inaweza kuamua mzazi ampeleke chuo gani ili kupata matokeo mazuri.
Mfano - kwa mtoto wa kike bright lakini ambaye hajatulia: usimpeleke IFM?
Hapa napata ranking kama ifuatavyo:

A: FACULTY (Wingi na Ubora wa walimu - Experienced Professors, Doctors, Masters, etc.)
1. UDSM
2. SUA
3. Mzumbe
4. IFM

B: LEARNING ENVIRONMENT (Mazingira ya kusomea - kwa wastani vyuo vya mjini vina distractions nyingi kwa wanafunzi na walimu)
1. Mzumbe
2. SUA
3. UDSM
4. IFM

C: SOCIAL ENVIRONMENT (Mahusiano ya kijamii YANAYOJENGA kati ya wanafunzi, walimu, wananchi wanaozunguka chuo)
1. UDSM
2. SUA
3. Mzumbe
4.
5. IFM

Je, ranking hii inakubalika? Tunweza kupata mwongozo kwa vijana wetu wanaotarajia kuanza elimu ya juu.

Kwa migomo yote hyo hamna kitu..,.hapo

Poor analysis!! Crap!!!

Toa basi analysis yako kabla hujasema yangu mie. Sababu zilizonifanya nitoe analysis hiyo ni hivi:-

a. Ubora wa waalimu wake katika sekta aliyoulizia. Kama husadiki chukua curicullum au jina lengine prospectus ya IFM, UDSM, Mzumbe na Sokoine pima walimu wake na taaluma walizonazo na vyuo walivyosomea utaamini kwanini nimekuja na analysis hiyo.

b. Ubora wa kozi wanazozitoa, kachukue course contents za IFM, UDSM, Mzumbe na Sokoine linganisha utajua kozi gani zinaendana na wakati uliopo.

c. Performance katika utafiti (Uchapishaji) Walimu wa IFM, UDSM wengi wamechapisha utafiti wao katika viwango vya kimataifa kulinganisha na vyuo vyengine. Kwa maana nyengine wanakubalika kimataifa na sio Tanzania pekee yake.

d. Quality ya wanafunzi wake na wanakofanya kazi, zunguka kwenye maofisi wanafunzi wengi wanaomaliza vyuo vya IFM na UDSM wamepata kazi na wanafanya kazi kulinganisha na wanafunzi wa vyuo vyengine.

Chuo kizuri kinajengwa na mambo matatu mosi ubora wa waalimu wake (kwani ndio uti wa mgongo wa chuo), Elimu wanayotoa na uwezo wa wanafunzi kuajiriwa kwani mwanafunzi haendi chuoni kutazama majengo bali anaenda kupata elimu aajirike (value for money). Bila ya hivyo hakuna mtu atakuja kusoma kwako.

Mie sipendi kulumbana kiushabiki bali nakupa maoni yangu unaweza kuyachukua au ukayaacha muamuzi ni wewe.

kwani hata Chenge mzee wa vijisenti si amesoma Havard...tunataka matolkeo ya elimu sio vyuo au vyeti...

Vyuo vinatofautiana kulingana na Kozi ungefafanua unahitaji kozi gani ili upate msaada mzuri.

Chenge - udsm
karamagi- udsm
Kikwete- Udsm
Lowasa-Udsm
6- Udsm
Idi Simba-Udsm
Mkono- udsm
Mchango wao kwa taifa ?
Nakushauri uangalie na Mambo mengine.

mambo ya biashara na uhasibu atahangaika sana kusaka ajira make vyuo vingi vina offer kozi hzo,kwanin asijoin pale Ardhi university make ndio chuo pekee tz kinachotoa kozi za kipekee,Kozi zifuatazo zinapatikana pale tu nchi nzima na ndo maana wahitimu pale hawakai mtaani hata miezi mi3,
1.BSc.in Geomatics(land surveying)
2.BSc.in Geoinformatics(GIS)
3.BS.in Land Management and Valuation
4.Bsc.in Building Economy
5.Bsc.in Finance and investment
6.Bachelor of Archtecture
Na nyingine kibao,tembelea website ya chuo hicho,Ardhi University - Tanzania: Welcome

Mbona unachanganya maada,kwani vyuo vikuu viko vingapi ?chuo kikuu kipo kimoja tu udsm na sasa udom hivyo vingine sio vyuo vikuu.wewe nenda mlimani kasome acha kujichanganya.

nna mashaka na akili yako mkuu huwezi kuwa mzima wewe, eti chuo kikuu kipo kimoja!Mzumbe? St.Augustine?Muslim? SUA?Tumaini?ni nini zote hivyo?acha dharau na kuongea upupu unaonyesha wazi ulifaulu kwa nguvu ya DESA na vijiji,usikute ulimaliza na GPA ya 2,fool

SUA=Kilimo,ila mkuu hapo kwenye UDOM umeniacha hoi nacheka mpaka mbavu zinauma ha ha ha ha ha ha ha ha ha

sua- agriculture economics and agri busines

Back
Top Bottom