Chuo Kikuu bora TZ ni kipi kwa kusomea Uhasibu au Biashara? - ni UDSM, Mzumbe au IFM?

Ok. Kuhusu TAALUMA I can conlude UDSM ndio the best.

Sasa labda kuhusu MAZINGIRA ya kusomea, je ni Mzumbe au? Mazingira manake utulivu wa mandhari, madarasa safi na ya kutosha, CUSTOMER SERVICE bomba, uhusiano wa heshima kati ya mwalimu na mwanafunzi (hasa usalama kwa girls), huduma ya chakula na malazi, recreational facilities, etc.
 
Unachotaka wewe ni chuo ambacho kijana anaweza kusoma masomo ya Uhasibu au Biashara. Kama ni masomo ya uhasibu kigezo kikubwa unachoweza kutumia ni kutafuta mafanikio ya wanafunzi wanaotoka UDSM, Mzumbe, IFM, n.k kwenye mitihani ya CPA kwani uhasibu bila "professinal qualifications" ni kazi bure. Kuhusu masomo mengine ya biashara sina uhakika namna ya kupima. Mwanangu anasoma IFM "and I am not very impressed ". Mimi bado naona UDBS ni chuo kizuri kabisa. Wana mapungufu yao ambayo yapo kwenye vyuo vyote lakini kupita vyuo vingine vyote wana wahadhriri wengi wenye sifa kubwa zaidi.
 
Nimesoma Accounting IFM wakati ule bado kinatoa Advanced Diploma, ni chuo kizuri kuliko vyote kwani tulipokuwa field, tuliotoka IFM tulionekana bora kuliko Mzumbe na UDSM. Naweza kukushauri umpeleke pale lakini kwanza kama unaweza ada yake maana hata kama atapata mkopo hiyo asilimia 40 yake ni nusu ya ada ya mwaka kwa vyou vingine. Pia kuna wengine wameshasema lazima akaze msuli kama ni mzembe kusoma ata-disco semister ya kwanza.
Kuhusu rushwa ni matatizo ya vyuo vyote na hasa mtu binafsi, IFM ukijifanya unajua kuhonga watakufilisi maana wanaweza ficha matokeo ili uwahonge wakutolee lakini hadi ufike huko umeyatafuta mwenyewe.
Mzumbe wanakariri sana na UDSM wako shallow, wanasoma mambo mengi mno kiasi kwamba wanashindwa kuwa co petent hasa kwa wahasibu.
Yangu ni hayo tu mkuu.:frown:
 
Asante kwa ushauri, vigezo ulivyotoa (in red) naona NAAM! ila tatizo kwa SUA ni hiyo 'Agri' tu. Labda nitumie vigezo hivyo kwa kupambanisha Mzumbe, UDSM, IFM na Zanzibar University?
Agric haimaanishi wanasoma kilimo...unajua watu wengi wanafikiri hivyo...watu wa agribusiness and agric economics wanasoma uchumi na biashara kama wengine...principles ni zilezile hilo ni jina tu....ni sawa na mtu asome rural development na community development....hawa kimsingi wanasoma kitu kimoja tu. Ajira ya ndugu yako itakuwa sawa na wa IFM, Mlimani na vyuo vyote wakuu walivyopendekeza...tena atakuwa bora zaidi..SUA hakuna ubishoo wala sharobaro...ni shule tu na kupumzika....kama ana nia ya kuwa mchumi..ama mfanya biashara mzuri ama kuajiriawa katika sekta hizi...asome SUA utanitafuta akimaliza kama tutakuwa hai.Nimewashauri wengi waliotaka kusoma masomo hayo..mwisho wa siku wamekuja nisifu sana.Akisoma SUA....atakuwa ameiva..na hata akiwa graduate school hawezi pata shida ktk research ama dissertation kwani wanasomeshwa na kufanya practicles kwa sana tu.
 
Mie naomba nikupatie ushauri wa kitaaluma zaidi ya habari za kusikia. Vyuo vyote ulivyotaja hapo juu vina faida na hasara zake. Pia inategemea unataka kijana wako asomee kitu gani kama ni economics, accounting , finance, econometrics, business management, management etc.

Mzumbe - kiukweli sio chuo kinachofaa kwani hakina waalimu na kinachukua walimu wake wengi IFM , na UDSM. Na sababu kubwa ni baada ya scandal ile ya vyeti feki wengi wametimka au wameamua kurudi tena shule wakasome vizuri. Ila faida yake ni kwamba gharama za ada yao ni chini kidogo kulinganisha na vyuo vyengine kama kijana wako unamlipia ada. Pia admission competition ni ndogo kulinganisha na IFM na UDSM hivyo basi unaweza kuwa na uhakika wa kupata admission.

IFM - hiki ni tertiary university ijapokuwa miaka ya karibuni wameanza kuwa wanatoa degree. IFM ni tertiary university but wameexcell vizuri sana katika sekta ya Accounting, Finance na Banking. Hivyo kijana wako ukitaka asomee sekta hizo ni bora nakushauri aende IFM kulinganisha vyuo vyote hapo hasa kwasababu sasa hivi wataalamu wengi wa finance, accounting wako IFM. Tatizo la IFM ni ada yake aghali sana kulinganisha na mzumbe sijui UDSM? Pia IFM vijana wanakuwa hawakai darasani hasa akina dada kutwa wako mitaani. Vile vile waalimu wa pale IFM kutwa wapo kwenye consultancy, research na masemina wana muda mchache wa kufundisha hilo linachangia kuleta mapungufu kwenye ufundishaji.

UDSM - Ni chuo kizuri sana kwa mtu anayekusudia kusomea Economics, Econometrics kwani kuna wataalamu waliobobea pale. Hata hivyo nao wanatatizo sawa na IFM waalimu kutwa wapo katika consultancy, research na masemina. Hivyo kijana wako kama ni kilaza anaweza kusumbuka .

SUA - Kama alivyosema mtu mmoja wazuri sana katika research na economics. Ila wanapungufu katika sekta ya decision making, accounting, finance. Kwahiyo kama unataka kijana wako awe mchumi SUA kuzuri, kama UDSM.

Zanzibar University- Ni kweli hichi ni chuo kizuri ila hakina jina. Na wanafundisha vizuri sana na wanafunzi wengi wanaenjoy pale na ada sio kubwa sana. Tatizo lake liko katika cheti (kwasababu ni chuo cha kiislamu), pia kuna tatizo la kimazingira maana kipo zanzibar, vilevile waalimu wake wengi ni kutoka nje ya nchi sasa sielewi ufanisi wao but overall vijana wamesoma pale wamemaliza na wamepata ajira.

Poor analysis!! Crap!!!
 
Usisahau chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kinafunika sana maana huku hamna cha feni wala nini weather yenyewe ni favorable kwa kamuzi.
Mind you mwisho wa siku chuo ni chuo ni yeye mwenyewe tu mwisho wa siku na uwezo wake wa kudeliver popote atakapokuwa hata kama angesoma distance learning!
 
Ok. ni wazi kwamba kuna vigezo vingi. Hivyo tabia ya mtoto inaweza kuamua mzazi ampeleke chuo gani ili kupata matokeo mazuri.
Mfano - kwa mtoto wa kike bright lakini ambaye hajatulia: usimpeleke IFM?
Hapa napata ranking kama ifuatavyo:

A: FACULTY (Wingi na Ubora wa walimu - Experienced Professors, Doctors, Masters, etc.)
1. UDSM
2. SUA
3. Mzumbe
4. IFM

B: LEARNING ENVIRONMENT (Mazingira ya kusomea - kwa wastani vyuo vya mjini vina distractions nyingi kwa wanafunzi na walimu)
1. Mzumbe
2. SUA
3. UDSM
4. IFM

C: SOCIAL ENVIRONMENT (Mahusiano ya kijamii YANAYOJENGA kati ya wanafunzi, walimu, wananchi wanaozunguka chuo)
1. UDSM
2. SUA
3. Mzumbe
4.
5. IFM

Je, ranking hii inakubalika? Tunweza kupata mwongozo kwa vijana wetu wanaotarajia kuanza elimu ya juu.
 
Wadau naomba msaada. Nina uncle wangu anataka kumrejesha mtoto wake aje asomee shahada ya biashara kwenye University/Chuo hapa Tanzania. Ameniomba ushauri kuhusu wapi ampeleke mtoto wake (Chuo bora kwa masomo ya Uhasibu au Biashara). Kwa vigezo rahisi vya popularity x 'quality' nimepata vyuo 3 - UDSM, Mzumbe na IFM. Naomba mwongozo kuhusu kipi bora zaidi (just ranking). Naomba kuwakilisha.

Huyo atakua kaply kama mature age entry coz nijuavo mimi system mpya ya Bongo hairuhusu multiple admission.
Kamasio hivo basi itakua unataka kujua ni chuo gani Bora (comparison)



Prove me wrong!
 
Ok. ni wazi kwamba kuna vigezo vingi. Hivyo tabia ya mtoto inaweza kuamua mzazi ampeleke chuo gani ili kupata matokeo mazuri.
Mfano - kwa mtoto wa kike bright lakini ambaye hajatulia: usimpeleke IFM?
Hapa napata ranking kama ifuatavyo:

A: FACULTY (Wingi na Ubora wa walimu - Experienced Professors, Doctors, Masters, etc.)
1. UDSM
2. Mzumbe
3. SUA
4. IFM

B: LEARNING ENVIRONMENT (Mazingira ya kusomea - kwa wastani vyuo vya mjini vina distractions nyingi kwa wanafunzi na walimu)
1. Mzumbe
2. SUA
3. UDSM
4. IFM

C: SOCIAL ENVIRONMENT (Mahusiano ya kijamii YANAYOJENGA kati ya wanafunzi, walimu, wananchi wanaozunguka chuo)
1. UDSM
2. SUA
3. Mzumbe
4.
5. IFM

Je, ranking hii inakubalika? Tunweza kupata mwongozo kwa vijana wetu wanaotarajia kuanza elimu ya juu.

Sijakuelewa

Unataka kunambia Mzumbe kuna experienced staff (Dr,Prof) Kuliko Sua??, Sikuamini kabisa!,
Umeenda na Maji Kama Gbagbo!
 
Jamaa yangu yuko IFM, nasikia ukishikwa tu, jamaa wanadai ukate laki laki nanusu. mlimani inategemea, maana si kuelewa ni kuafaulu tu, kariri au egesha bora kufaulu. Mzumbe sijasikia baya. Yote niliyosema nimesikia tu. Mwambie jamaa yako mwache aamue mwenyewe.

Kwa nini ushikwe? Na usiposhikwa je!
Poor Tanzanian education
 
Wadau naomba msaada. Nina uncle wangu anataka kumrejesha mtoto wake aje asomee shahada ya biashara kwenye University/Chuo hapa Tanzania. Ameniomba ushauri kuhusu wapi ampeleke mtoto wake (Chuo bora kwa masomo ya Uhasibu au Biashara). Kwa vigezo rahisi vya popularity x 'quality' nimepata vyuo 3 - UDSM, Mzumbe na IFM. Naomba mwongozo kuhusu kipi bora zaidi (just ranking). Naomba kuwakilisha.

mzumbe is the best,mimi nimesoma pale(sio uhasibu lakini) lakini wale jamaa wamasomo ya biashara walikuwa wanapata full dozi ambayo imewafanya kupata ajira haraka sana na wengine kuwa na firms zao,mfano mwingine mtoto wa uncle wangu amemaliza pale mambo ya biashara( BAF) mwaka jana na sasa kapata kazi KENYA COMMERCIAL BANK,so mi nakushauri mpeleke mzumbe,UDSM imebaki jina tuu
 
uh!sa ce wa tumaini,udom,muccobs,mum na sauti tuelewe nin hapo,kwamba vyuo vyetu havina ishu au?
 
Back
Top Bottom