Mngendalyasota
Senior Member
- Jan 22, 2011
- 171
- 48
SAUT ni miongoni mwa vyuo ambavyo management style yake ni customer-centred (Student-centred), wanachuo wanasikilizwa sana na Ofisi ya VC na DVCAA katika maswala yao ya kitaaluma. Ndiyo maana maktaba ya SAUT, pale inapotokea upungufu wa vitabu Management ya Maktaba chini ya Dr Safari wapo radhi hata kutoa photocopies ili wanachuo wapate nakala za kutosha. Kupunguza uhaba huo wa vitabu chuo kimeweka computers za kutosha kwenye maktaba (MGULUNDE RESOURCE CENTRE) ambazo zimeunganishwa kwenye mtandao. Lakini hata wireless internet inapatikana pia kuzunguka maktaba. Sasa hebu tuje UDSM maktaba (CHAGULLA) yake not updated for some years now kutokana na serikali kupuuza elimu hapa Tanzania kwa kisingizio cha ufinyu wa bajeti. Kwa taarifa zisizorasmi ni kwamba ubora wa vyuo vya umma umeporomoka sana ila historia ndiyo inayoendelea kuwabeba hasa UDSM (sleeping giant). Pili udikteta wa serikali kupitia maVCs kwenye vyuo hivyo vya umma umepunguza sana kufichuliwa kwa mapungufu mengi ya msingi ya kitaaluma yanayowasibu wanavyuo. Nenda UDOM, kwa mfano, utaona maajabu, huko Tutorial Assistants wamepewa vipindi na wanafundisha undergraduates(BA) na Assistant Lecturers wanawafundisha wanafunzi wa masters (MA na MSC) kinyume kabisa na sheria za TCU. Lakini kwenye vyuo binafsi kama SAUT, kwa mfano, TAs hawaruhusiwi hata kusimamia seminars tu. Mhadhiri mchovu hukataliwa na wanchuo if he does not deliver well in class jambo ambalo si kawaida kwa public universities.Vyuo binafsi ndiko mahala pekee ambapo OPRAS zinafanyiwa kazi na kuwa na mrejesho kwa wahusika tofauti kabisa na Public Universities.