Chuo Kikuu Yohana wagoma.....ni aibu kwa uongozi

Magezi

JF-Expert Member
Oct 26, 2008
3,359
692
na Danson Kaijage, Dodoma


JINAMIZI la wanafunzi wa vyuo vikuu kugoma limekikumba Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana mkoani hapa ambapo wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu wamegoma kuingia madarasani kwa zaidi ya saa nane wakishinikiza uongozi wa chuo hicho kuwapatia fedha kwa ajili ya kununulia vifaa muhimu kulingana na kozi zao.

Mgomo huo ulitokana na wanafunzi kupata taarifa kuwa fedha zao zimeishafika chuoni hapo kupitia akaunti ya chuo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, lakini uongozi wa chuo umekaa kimya bila kutoa taarifa yoyote.

Akizungumza na Tanzania Daima, Rais mstaafu katika serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, Lengai ole Sabaya alisema wanafunzi wametumia njia zote za kidemokrasia, lakini imeshindikana hivyo wameamua kutumia mgomo ili kushinikiza uongozi kutenda haki.
Alidai kuwa uongozi huo wa chuo umeona fedha hizo ni nyingi, hivyo ulitaka kuchukua uamuzi wa kutaka kuwanunulia wanafunzi vifaa jambo ambalo hawana imani nalo.

Mwanafunzi mwingine, Venance Kamuhanga alisema yeye ndiye aliyepewa jukumu la kufuatilia fedha hizo, Bodi ya Mikopo na kusisitiza kiasi cha sh milioni 91 zimekwishafikishwa chuoni hapo.

"Kwa nini miaka iliyopita walikuwa wanatuingizia kwenye akaunti zetu, lakini mwaka huu wagome? Au kwa kuwa miaka iliyopita fedha hizo zilikuwa ni kidogo ambapo mtu mmoja alipata sh 17,000 hadi 15,000?" alihoji Kamuhanga.

Kwa mujibu wa Kamuhanga kwa mwaka huu, alidai kuwa mtu anayekopeshwa asilimia 100 atapata sh 180,000 wakati yule wa asilimia 40 atapata sh 121,000 hadi 126,000.

Hata hivyo, wanafunzi hao walisitisha mgomo huo baada ya Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Minoris Meshack kuzungumza nao na kuwaahidi kuwapatia fedha zao.

Makamu huyo alisema uongozi wa chuo uliona ni busara kuwanunulia vitu hivyo ili wanafunzi hao waweze kusoma kwa ufanisi kwa kuwa wakipewa fedha hizo wengi hawanunui.

My Take:

Angalia wasomi wetu wananvyo endesha mambo utadhani wako karne ya 17. Mwanafunzi wa chuo kikuu anachukuliwa kama mtoto wa shule ya msingi eti akipewa hela hata nunua vifaa vya kusomea??

Hii inaonyesha uongozi wa chuo kikuu hicho walivyo na uroho wa fedha sasa wanataka wachukue chajuu kwenye pesa ya wanafunzi ili hali ni mikopo na wanafunzi wenyewe ndo watawajibika kuilipa.

Kwa mwendo huu na maprofesa hawa.......kazi tunayo.
 
Nchi hii hata watu wa mungu na mashirika yao nao ni mafisadi, sasa wanataka kufisadi mikopo ya wanafunzi
 
Nadhani mgomo ni tangazo la biashara kwa vyuo vikuu vingi hapa Tanzania ambalo wamiliki hawana gharama ya kulipa kwa media.!
 
Back
Top Bottom