Uchafu wa TCU na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yosefu

la fiducia

JF-Expert Member
Mar 13, 2016
212
168
Habari zenu wakuu!? Ukipitia katika website ya tcu utaona habari mpya inayoonesha qualified and non qualified students wanaosoma diploma ya education st Joseph.

Kwanza mwanzoni ile ilikuwa ni program ya miaka mitano ( 5 years degree program) ila baada ya kufutwa kwa Chuo cha mtakatifu yosefu tawi la Arusha tcu ikafuta pia udahili wa wanafunzi wapya katika kozi ile na kuamrisha wanafunzi wanaoendelea watalazimika kumaliza level ya diploma kwanza.

Vigezo vya kuingia kataika kozi ile mwanzo ilikuwa ni div 4 ya pointi 26 ambayo wizara na Chuo walikubaliana pamoja na tcu!

Baadae chuo walitoa tangazo kwenye website yao kwamba kozi hii ili uweze kujiunga unatakiwa uwe na d nne tuu na mbili nikutoka katika masomo ya sayansi!

Sikujua walikubaliana tena kuweka vigezo hivyo ama ni Chuo wenyewe waliamaua! Chuo kikaanza kudahili wanafunzi kwa vigezo hivyo tangu mwaka 2013!

Baadae mwaka elfu mbili na kumi na tano TCU wakapeleka barua chuoni ya kwamba Chuo ina dahili wanafunzi wasio na sifa walikuwa wakichukua hata wanafunzi waliosoma arts na wengine hata kuwa na d moja tuu lakini walikuwa wanachukuliwa kusoma kozi hii ya masomo ya sayansi.

Majina yakatumwa na tcu ya wanafunzi ambao walikuwa hawana vigezo vya kisoma kozi hii, wanafunzi wakataka wabandikiwe hayo majina ili wajue, ila chuo wakataaa wakasema hizo habari hazina ukweli!

Wanafunzi hawakuishia hapo walifuatilia hili swala na kuagundua ni kweli ila chuo kilikuwa kinafanya uhuni tuu na kuwatishia wanafunzi atakae fuatilia anafukuzwa Chuo, na kweli wanafunzi wengi walifukuzwa Chuo kutokana na hili swala,.

Wanafunzi hawakukomea hapo wakaendelea kufuatilia na kuanzisha migomo kipindi hicho waziri wa elimu alikuwa shukuru kawambwa!

Shukuru kawambwa alifika chuoni na kukagua na alikuja asubuhi na kuondoka jioni kabisa! Baada ya pale shukuru kawambwa aksema wanafunzi wote wanasifa na hakuna ambae hana vigezo wote wanavigezo na wataendelea kusoma na hii kozi inatambuliwa na mikopo watapta.

Baadae Tcu nao walikuja kuthibitisha hilo na kusema wanafunzi wote wanasifa na waendelee kusoma!

Kilichokuja kutokea nikwamba baada ya kufutwa kwa hivi vyuo tarehe 14 mwezi 3 wanafunzi hawa wakaamuriwa na tcu wahamie main Campus ambayo ndio ile ya luguruni!

Wanafunzi waliripoti wakaambiwa watapewa maelekezo ya jinsi utaratibu mpya utakavyokuwa,

Baada kama ya wiki kupita wakawa wanalazimishwa kuingia madarasana kusoma! Wanafunzi hao wakawa wanahoji tutaingia vipi darasani wakati TCU hawajatupa utaratibu?
Na kule walikuwa wanasoma miaka mitano degree program huku wameambiwa watalazimika kusoma diploma kwanza he utaratibu upoje?

Vijana hawa kila walivyoendelea kuhoji walikuwa hawapati jibu sahihi wakaamua kwenda kwa waziri wa elimu mama ndalichako, waziri alichukua jukumu la Kuwaita wote wanaohusika pale TCU! wakaambiwa walitolee ufafanuzi wa wazi katika vyombo vya habari mgaya akalipotezea!

Kumbe walikuwa wanashindwa kulitolea maamuzi kwa kuwa kulikuwa na wanafunzi ambao walisema hawana vigozo vya kusoma kozi hiyo!

Na hilo swala wanafunzi walilifatilia mda sana na mgaya ni shahidi wa hilo ila walikaa kimaya na kuacha mabo yaende tuu!

Baadae NACTE wakasema wale walio chini ya dv 26 hawatambuliki na watakuwa wamejiondoa wenyewe.

Vijana wakendelea kukomaa wakasema tushapotezewa mda sana leo hii mnatuakatisha jujuu haiwezekani, wakaenda tena TCU mgaya siku hiyo akataka kuondoka vijana wakamkomalia kikaendeshwa kikao na majibu ya tcu yalikuwa hivi.......

Kama mngekuwa hamna vigezo mbona chuoni mmepokelewa?
Hapa sisi wenyewe tupo kwenye matope wizara ipo kwenye matope nyie wanafunzi mpo kwenye matope na Chuo pia kipo kwenye matope.
Wanafunzi wote ni qualified ila ni wanafunzi ishirina na tatu tuu ndio wanamatatizo!

Vijana wakawaambia sisi tunataka hayo ulioyatamka utupe kwa maandishi, wakagoma tena kuyathibitisha kwa maandishi!

Chuoni wakawapa barua wanafunzi ya makubaliano yao na tcu kuwa vigezo ni d nne!
Nitawaletea attachment ya hiyo barua.

Baada ya kufatilia sana tcu wakaweka majina ya disqualified dk kumi na kuyaondoa baada ya kusumbuliwa sana ndio wakaamua wayaweke sasa!

Mgaya akaambiwa na waziri wa elimu achana na yaliyopita tuangalie tulipo lizungumzie hili swala! Mgaya akapotezea tena akakaa kimya! Huko chuoni nako wahindi wanalazimisha wanafunzi waingie darasani!

Kumbe walikuwa wanacheza mchezo mchafu wanafunzi wakiingia darasan wanapiga picha wanazituma tcu kuwa wanafunzi wamekubali kuingia madarasani ili walizime juu juu.

Wanafunzi walipgundua hayo wakaatumia nguvu kuwafanya wanafunzi wenzao wasiingie madarasani!

Na lengo lao ilikuwa ni kuwapunguza kwa mtindo wa kuwafelisha!

Vijana hao wakaamua kwenda had I kwa Paul makonda mkuu wa mkoa wa dar es salaam mwanzo wa wiki hii bila mafanikio, wazo lao la mwisho ilikuwa ni kumtafuta mwana sheria ili kumwelezea swala lao kama anaweza kuwasaidia

Lakini kuna haja gani ya kutafuta mwanasheria wakati mamlaka zinazohusika zipo!?

Sasa tcu tuwaelewe vipi mwanzo walisema wanfunzi wote ni qualified leo hii mnawaambia wanafunzi hao hao ni disqualified na wengine wako mwaka wa tatu!

Inatia huruma sana watoto wa watu wameteseka sana, wazazi wao wamehangaika kuwalipia ada kwa miaka yote hiyo ada ya muhindi c mchezo,

Je kama ww ingekuwa mwanao amefanyiwa uhuni kama huo kweli utachukua hatua gani?

Wanaohusika plz nendeni pale muwasaidie watoto wa watu wa maskini wanaoteseka katika nchi yao kwa wageni wanaoshirikiana na walafi watanzania wenzetu.

Ebu tushauriane na kuwapa ushauri Hawa vijana wafanyeje, haturusu matusi wala maneno machafu ukishindwa pita kushoto.

Nitajitahidi kupata attachment zote za ushahidi wa wanafunzi ambazo ni officials kati yao, chuo , Tcu na wizara ya elimu.
Na naendelea kupata mengi kuhusu hili swala na ntafikisha kila litakaponifikia,

Source wanafunzi wa st Joseph luguruni Dar es salaam.
 
Unauliza swala gani hapa? Wanafunzi wengi wamepelekwa vyuo vingine. Hao ambao hana sifa, yaani hao wa form 4 lazima tukubali kwamba TZ hatuna digrii ya form 4. Kama ni kuwa serious, ni kuwashitaki TCU pamija na ST joseph kwa kuwaingiza chuoni kiutapeli.

Nina hisia kwamba TCU na wizara ya kawambwa,nwalikuwa na ushirika wa aina fulani na hao ST. Joseph. Bodi ya mikopo pia ilihusika maana waliwezaje kutoa ada za watu wasio na sifa za kusoma digrii?
 
Nahisi kuna ushirika kati ya TCU na baadhi ya vyuo. Sio st. Joseph tu, Kuna vingine Kama Kampala international university, university of bagamoyo. Vyuo havina vigezo, uongozi mbovu,figisu figisu nyingi lakini bado hatua stahiki hazichukuliwi na TCU wamekaa kimya. Nawashauri hao vijana waliofanyiwa utapeli walipeleka swala hili mahakamani, waishtaki TCU na st. Joseph
 
mgaya ni tumour pia tcu na st joseph kuna kitu kizito hapo na cho ni rushwa inayotembea pia HESLB pia wanashirikiana kuwaibia wanafunz
 
Unauliza swala gani hapa? Wanafunzi wengi wamepelekwa vyuo vingine. Hao ambao hana sifa, yaani hao wa form 4 lazima tukubali kwamba TZ hatuna digrii ya form 4. Kama ni kuwa serious, ni kuwashitaki TCU pamija na ST joseph kwa kuwaingiza chuoni kiutapeli.

Nina hisia kwamba TCU na wizara ya kawambwa,nwalikuwa na ushirika wa aina fulani na hao ST. Joseph. Bodi ya mikopo pia ilihusika maana waliwezaje kutoa ada za watu wasio na sifa za kusoma digrii?
Bodi ya mikopo pia nao walikuwa pamoja na TCU,Wizara pamoja na chuo! Kwa saba karibia nusu ya hao wanafunzi walikuwa wanapata mikopo! Na swala la wanafunzi hawa kutopelekwa vyuo vingine ni kwamba kozi ya miaka mitano ilikuwa inatolewa pale tuu!

Kwa hiyo TCU waliwahamishiwa pale na kuwaambia kuwa tunataka kuona utaratibu na jinsi mnavyofundishwa kwa kuwa mpo karibu Arusha mlikuwa mbali ndio maana tulikuwa tunashindwa kufatilia!!

Sasa ata hawaeleweki!
 
Habari zenu wakuu!? Ukipitia katika website ya tcu utaona habari mpya inayoonesha qualified and non qualified students wanaosoma diploma ya education st Joseph.

Kwanza mwanzoni ile ilikuwa ni program ya miaka mitano ( 5 years degree program) ila baada ya kufutwa kwa Chuo cha mtakatifu yosefu tawi la Arusha tcu ikafuta pia udahili wa wanafunzi wapya katika kozi ile na kuamrisha wanafunzi wanaoendelea watalazimika kumaliza level ya diploma kwanza.

Vigezo vya kuingia kataika kozi ile mwanzo ilikuwa ni div 4 ya pointi 26 ambayo wizara na Chuo walikubaliana pamoja na tcu!

Baadae chuo walitoa tangazo kwenye website yao kwamba kozi hii ili uweze kujiunga unatakiwa uwe na d nne tuu na mbili nikutoka katika masomo ya sayansi!

Sikujua walikubaliana tena kuweka vigezo hivyo ama ni Chuo wenyewe waliamaua! Chuo kikaanza kudahili wanafunzi kwa vigezo hivyo tangu mwaka 2013!

Baadae mwaka elfu mbili na kumi na tano TCU wakapeleka barua chuoni ya kwamba Chuo ina dahili wanafunzi wasio na sifa walikuwa wakichukua hata wanafunzi waliosoma arts na wengine hata kuwa na d moja tuu lakini walikuwa wanachukuliwa kusoma kozi hii ya masomo ya sayansi.

Majina yakatumwa na tcu ya wanafunzi ambao walikuwa hawana vigezo vya kisoma kozi hii, wanafunzi wakataka wabandikiwe hayo majina ili wajue, ila chuo wakataaa wakasema hizo habari hazina ukweli!

Wanafunzi hawakuishia hapo walifuatilia hili swala na kuagundua ni kweli ila chuo kilikuwa kinafanya uhuni tuu na kuwatishia wanafunzi atakae fuatilia anafukuzwa Chuo, na kweli wanafunzi wengi walifukuzwa Chuo kutokana na hili swala,.

Wanafunzi hawakukomea hapo wakaendelea kufuatilia na kuanzisha migomo kipindi hicho waziri wa elimu alikuwa shukuru kawambwa!

Shukuru kawambwa alifika chuoni na kukagua na alikuja asubuhi na kuondoka jioni kabisa! Baada ya pale shukuru kawambwa aksema wanafunzi wote wanasifa na hakuna ambae hana vigezo wote wanavigezo na wataendelea kusoma na hii kozi inatambuliwa na mikopo watapta.

Baadae Tcu nao walikuja kuthibitisha hilo na kusema wanafunzi wote wanasifa na waendelee kusoma!

Kilichokuja kutokea nikwamba baada ya kufutwa kwa hivi vyuo tarehe 14 mwezi 3 wanafunzi hawa wakaamuriwa na tcu wahamie main Campus ambayo ndio ile ya luguruni!

Wanafunzi waliripoti wakaambiwa watapewa maelekezo ya jinsi utaratibu mpya utakavyokuwa,

Baada kama ya wiki kupita wakawa wanalazimishwa kuingia madarasana kusoma! Wanafunzi hao wakawa wanahoji tutaingia vipi darasani wakati TCU hawajatupa utaratibu?
Na kule walikuwa wanasoma miaka mitano degree program huku wameambiwa watalazimika kusoma diploma kwanza he utaratibu upoje?

Vijana hawa kila walivyoendelea kuhoji walikuwa hawapati jibu sahihi wakaamua kwenda kwa waziri wa elimu mama ndalichako, waziri alichukua jukumu la Kuwaita wote wanaohusika pale TCU! wakaambiwa walitolee ufafanuzi wa wazi katika vyombo vya habari mgaya akalipotezea!

Kumbe walikuwa wanashindwa kulitolea maamuzi kwa kuwa kulikuwa na wanafunzi ambao walisema hawana vigozo vya kusoma kozi hiyo!

Na hilo swala wanafunzi walilifatilia mda sana na mgaya ni shahidi wa hilo ila walikaa kimaya na kuacha mabo yaende tuu!

Baadae NACTE wakasema wale walio chini ya dv 26 hawatambuliki na watakuwa wamejiondoa wenyewe.

Vijana wakendelea kukomaa wakasema tushapotezewa mda sana leo hii mnatuakatisha jujuu haiwezekani, wakaenda tena TCU mgaya siku hiyo akataka kuondoka vijana wakamkomalia kikaendeshwa kikao na majibu ya tcu yalikuwa hivi.......

Kama mngekuwa hamna vigezo mbona chuoni mmepokelewa?
Hapa sisi wenyewe tupo kwenye matope wizara ipo kwenye matope nyie wanafunzi mpo kwenye matope na Chuo pia kipo kwenye matope.
Wanafunzi wote ni qualified ila ni wanafunzi ishirina na tatu tuu ndio wanamatatizo!

Vijana wakawaambia sisi tunataka hayo ulioyatamka utupe kwa maandishi, wakagoma tena kuyathibitisha kwa maandishi!

Chuoni wakawapa barua wanafunzi ya makubaliano yao na tcu kuwa vigezo ni d nne!
Nitawaletea attachment ya hiyo barua.

Baada ya kufatilia sana tcu wakaweka majina ya disqualified dk kumi na kuyaondoa baada ya kusumbuliwa sana ndio wakaamua wayaweke sasa!

Mgaya akaambiwa na waziri wa elimu achana na yaliyopita tuangalie tulipo lizungumzie hili swala! Mgaya akapotezea tena akakaa kimya! Huko chuoni nako wahindi wanalazimisha wanafunzi waingie darasani!

Kumbe walikuwa wanacheza mchezo mchafu wanafunzi wakiingia darasan wanapiga picha wanazituma tcu kuwa wanafunzi wamekubali kuingia madarasani ili walizime juu juu.

Wanafunzi walipgundua hayo wakaatumia nguvu kuwafanya wanafunzi wenzao wasiingie madarasani!

Na lengo lao ilikuwa ni kuwapunguza kwa mtindo wa kuwafelisha!

Vijana hao wakaamua kwenda had I kwa Paul makonda mkuu wa mkoa wa dar es salaam mwanzo wa wiki hii bila mafanikio, wazo lao la mwisho ilikuwa ni kumtafuta mwana sheria ili kumwelezea swala lao kama anaweza kuwasaidia

Lakini kuna haja gani ya kutafuta mwanasheria wakati mamlaka zinazohusika zipo!?

Sasa tcu tuwaelewe vipi mwanzo walisema wanfunzi wote ni qualified leo hii mnawaambia wanafunzi hao hao ni disqualified na wengine wako mwaka wa tatu!

Inatia huruma sana watoto wa watu wameteseka sana, wazazi wao wamehangaika kuwalipia ada kwa miaka yote hiyo ada ya muhindi c mchezo,

Je kama ww ingekuwa mwanao amefanyiwa uhuni kama huo kweli utachukua hatua gani?

Wanaohusika plz nendeni pale muwasaidie watoto wa watu wa maskini wanaoteseka katika nchi yao kwa wageni wanaoshirikiana na walafi watanzania wenzetu.

Ebu tushauriane na kuwapa ushauri Hawa vijana wafanyeje, haturusu matusi wala maneno machafu ukishindwa pita kushoto.

Nitajitahidi kupata attachment zote za ushahidi wa wanafunzi ambazo ni officials kati yao, chuo , Tcu na wizara ya elimu.
Na naendelea kupata mengi kuhusu hili swala na ntafikisha kila litakaponifikia,

Source wanafunzi wa st Joseph luguruni Dar es salaam.
Tuache kutafuta njia za mkato katika Elimu. Kama mngelifaulu haya yasingewapata. Baadala ya kusoma mnaendekeza mijadala Na waliomaliza shule zamani
 
daah mgaya ni jipu ambalo limeanza kutoa usaha kama ndalichako hatolitumbua kuna shda
 
Bodi ya mikopo pia nao walikuwa pamoja na TCU,Wizara pamoja na chuo! Kwa saba karibia nusu ya hao wanafunzi walikuwa wanapata mikopo! Na swala la wanafunzi hawa kutopelekwa vyuo vingine ni kwamba kozi ya miaka mitano ilikuwa inatolewa pale tuu!

Kwa hiyo TCU waliwahamishiwa pale na kuwaambia kuwa tunataka kuona utaratibu na jinsi mnavyofundishwa kwa kuwa mpo karibu Arusha mlikuwa mbali ndio maana tulikuwa tunashindwa kufatilia!!

Sasa ata hawaeleweki!
Kwa ufupi ni kwamba ktk nchi hii hakuna utaratibu wa digrii ya miaka 5 kwa form 4. Hiyo iko kenya kwenye mfumo wa 8-4-4 na wiki jana mjadala umeanza huko Kenya wakitilia mashaka juu ya mfumo huo wa elimu.

Inavyoonekana kuna watu serikalini walikuwa na vijana walioshindwa kuingia vyuoni, wakaamua kuunda mfumo usiokuwepo hapa nchini. Ktk hao vijana utakuta kwamba wengine ushindi wao haukuwa unawaruhusu hata kuingia form 5, sasa iweje waingie chuoni kusoma digrii? Hap Dar wamewaweka kuwazubaisha tu na baadaye watapewa diploma na certficates tu.

Hao wahindi wa St Joseph jihadharini nao sana! Hakuna elimu hapo. Vyeti watapata lakini soko hili la ajira lenye interview, watakwama sana!
 
Hili lipelekwe kwa wabunge pia kama J Mbatia (NCCR) na Mama Lyimo (CDM) wanaweza wakalivalia njuga likaenda. TCU na Wizara lazima wawe accountable kwenye hili.
 
Back
Top Bottom