Chongolo, tunaomba Katibu wa CCM kata ya Wazo achunguzwe kwa kusajili eneo la chama kwa jina lake

MNIACHEEE

New Member
Jul 9, 2022
2
0
- AMESAJILI ENEO LA CHAMA KWA JINA LAKE

Mheshimiwa Katibu Mkuu wetu mpendwa Daniel Chongolo, sisi wanachama cha Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Wazo tunaomba uunde timu maalumu ya kuchunguza ubadhilifu mkubwa au matumizi mabaya ya madaraka ‘Ufisadi’ unaofanywa na Katibu wetu wa CCM Kata ya Wazo, ndugu Dennis Modest Liheta ambaye hivi karibuni amejinufaisha kwa kujipatia Kiwanja kilichopo katika Mtaa wa Salasala eneo maarufu la JKT KWA BABA YALO, Mashimoni.

CCM Kata ya Wazo, ililiomba eneo hilo kwa Manispaa ya Kinondoni kwaajili ya kujenga ofisi za chama kwa kufuata taratibu zote ikiwa ni pamoja na kupitia ngazi ya chama wilaya na kubarikiwa na Katibu wetu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Cde Jacob Siay.

Sasa kwa kuwa Katibu wa CCM kata ndio mtendaji, ilibidi apewe jukumu la kufuatilia kiwanja hicho Manispaa, ndipo Katibu Kata Dennis Modest Liheta alitumia mwanya huo ku ‘take advantage’ ya kujinufaisha na kulisajili eneo hilo kwa jina lake binafsi badala ya CCM KATA YA WAZO.

Hadi sasa kiwanja hicho kinasomeka kwa jina la Dennis Liheta licha kuwa documents na process za uombaji zilikuwa cha chama cha mapinduzi kata ya Wazo.

Katibu Kata huyo, amekuwa kiongozi mwenye kufanya maamuzi ayatakayo akionyesha jeuri kwa viongozi wenzake, huku akijinasibu kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kumfanya chochote kwasababu, Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Cde Adam Ngalawa, amemweka kwenye kiganja.

Mara kadhaa amekuwa akilitumia jina la Mheshimiwa Ngalawa kuwatisha wanaCCM na viongozi wenzake wanaojaribu kuhoji masuala mbalimbali yenye ukakasi kwenye chama kata.

Habari za chini ya kapeti zinasema kuwa Katibu Kata wa Wazo anapata jeuri kupitia kwa Mzee Adam Ngalawa kwa kuwa Mzee analipa fadhila kwani mwaka 2022 alipewa zawadi ya kiwanja katika eneo la Mtaa wa Msigani na uongozi wa kata uliopita huku Denis Liheta akiwemo kwenye nafasi yake hiyohiyo ya Ukatibu.

Ndg. Dennis Modest Liheta amekuwa ni kiongozi mwenye kujali maslahi yake binafsi kwa Mwamvuli wa upole, huku akikitafuna chama kwa kupoteza Mali za chama.

Katibu Dennis Liheta amekigawa chama katika Kata ya Wazo kwa kuendeleza makundi ya uchaguzi, lakini pia kufikia hatua ya kutoa siri za maamuzi ya vikao vya kamati za maadili na siasa za kata, kitendo linachohatarisha usalama wa maisha ya wajumbe wa kamati hizo.

Mfano halisi: Hivi karibuni viongozi watatu wa matawi ya Wazo, Mivumoni na Kawawa walisimamishwa… wawili miezi sita na mmoja miezi mitatu kwa makosa ya kimaadili, lakini Katibu Dennis ameweza kutoa siri kwa waliosimamiswa kuwa mjumbe Fulani na Fulani ndio walioshinikiza mpewe adhabu…. Kitendo kilipelekea mmoja wa wajumbe kutumiwa meseji za kutishiwa maisha.

Mheshimiwa Katibu Mkuu Chongolo, situation kama hii inadhoofisha chama hasa ukizingatia tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwakani… Sisi wanaCCM Kata ya Wazo tunakuomba uingilie kati hilo ili kuokoa jahazi.

XXX KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI XXX
 

Attachments

  • Dennis Liheta.jpg
    Dennis Liheta.jpg
    57.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom