Uchaguzi 2020 Chonde chonde Watanzania,msisahau mwenendo wa wabunge wa CCM wawapo Bungeni na hatari ya kuwarudisha tena Bungeni kwa wingi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,048
144,454
Nawakumbusha watanzania kuwa ni wabunge wa CCM ndio waliopitisha sheria zote katili na kandamiza kama zile za makato ya Bodi ya Mikopo,Sheria ya kuunganisha Mifuko ya Hifadhi za Jamii na Sheria ya kikokotoo kipya kilichozua malalamiko makubwa kutoka kwa umma.

Nilisema jana katika mada yangu hapa JF kuwa wapinzani na wadau wengine tuna wajibu wa kuukumbusha umma wa watanzania juu ya athari za wabunge wa CCM wawapo Bungeni ili kesho wasianze tena kulia kwa watayoyafanya Bungeni.

Watanzania wakumbushwe: Mbunge wa CCM hata akiwa Doctor,Professor,Msanii maarufu,Mchungaji maarufu,n.k, awapo Bungeni huwa hana msaada kwa wananchi zaidi ya kupitisha tu miswaada ya inayoletwa na serikali na zaidi kutetea serikali Bungeni.

Pia,watanzania wajue tu Bunge likitawaliwa na wana-CCM,basi wasishangae Katiba ikabadilishwa na muda wa Uraisi ukaongezwa kama walivyoanza kupiga kampeni katika Bunge lililopita.

Media kwa sasa naona zitajikita zaidi kupamba wabunge wa CCM bila kuwakumbusha perfomance yao; hivyo, na wapinzani mkilalala na watanzania wakasahau yaliyopita,tutakuja kujuta huko mbele.

Ni aheri kuchagua mbunge mwenye kipato cha kawaida wa upinzani, kuliko mbunge tajiri wa CCM ;ni aheria kuchagua mbunge asie msomi wa upinzani, kuliko mbunge msomi wa kiwango cha udokta au uprofesa ambae ni CCM.

Kuna kila dalili media kutumika na kusahaulisha kabisa watanzania juu ya hayo niliyoyasema na mengine ambayo sikuyasema;kwahiyo, ni wajibu wetu kuyasema kupitia mitandao,mkikutano ya kampeni,n.k.

Kuna hatari naiona, ingawa kwa sasa wengi hamtaweza kunielewa, ila wakati utafika, mtakuja kunielewa ingawa teyari tunaweza kuwa tumechelewa.
 
Kweli kabisa, asilimia kubwa ya wabunge wa ccm bungeni ni mizigo, hawana msaada wowote kwa nchi!
Watanzania wanapaswa kujadili hili na sio kujadili misururu mirefu ya watia nia wa CCM au umaarufu wa watia nia wa CCM,n.k.
 
Tunashukuru kwa kutukumbusha lakini pia usisahau kutukumbusha na wale wabunge wanaopinga Kila kitu hata kama kina maslahi kwa jamii mfano wale walioandika barua majuu ili tunyimwe mkopo wa elimu na wale waliokuwa wanatutishia MIGA.
 
Yaani wabunge wa ccm hawana faida yoyote kwa taifa Ila wanafaida kwa kupitisha mauchafu yote ya serikali na hawahoji chochote wkt katiba na sheria za nchi zinavunjwa.......m

Hii ni ccm ya kishetani ni lazima tuhakikishe hawarudi tena madarakani
 
Una hoja nzuri sana Salary slip.

Ila kwa bahati mbaya sana ni wachache watakuelewa...wananchi wengi watachagua wabunge kwa kumwangalia Magufuli bila kujua kwamba ubunge na uraisi ni vitu viwili tofauti kabisa kiutendeji.
Ni sawa na mbingu na ardhi.
 
Una hoja nzuri sana Salary slip.

Ila kwa bahati mbaya sana ni wachache watakuelewa...wananchi wengi watachagua wabunge kwa kumwangalia Magufuli bila kujua kwamba ubunge na uraisi ni sawa na mbingu na ardhi.
CCM ni wazuri sana katika propaganda na pia media ziko upande wao; hivyo, sisi tusipojiongeza kwa kuyasema haya sasa,watanzania wanaweza kusahaulishwa na wakaami Dr.Kimei au Abbas Tarimba akiingia Bungeni, atakuwa tofauti na wabunge waliopita wa CCM na atakaokuwa nao Bungeni.
 
Back
Top Bottom