Hollo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2008
- 827
- 165
Na wanaosema ni Fisadi wana hakika na hilo?Wanaosema sio FISADI wanahakika na hilo?
Na wanaosema ni Fisadi wana hakika na hilo?Wanaosema sio FISADI wanahakika na hilo?
Na wanaosema ni Fisadi wana hakika na hilo?
...na ninamuomba aelewe kuwa jina langu la FMES ni pamoja na biashara behind it sasa sio jina tu ni signature kubwa sana na I have worked so hard kulifikisha lilipo, hapa JF huwa ninajitolea bure, lakini sio nje ya hapa, nilitaka tu hilo lieleweke wazi kwa wakuu wote hapa maana naona ndio kwanza ana post moja, ni vyema kufahamishana mapema, na ninamtakia mafankio mema hapa ndani ya JF!
Ahsante Wakuu!
mkuu natumai utakuwa umeliorodhesha (register) jina hilo brela na nchi nyingine ilipo na mawasiliano ya kibiashara. vinginevyo mkuu utakuta wenzio wamekuwahi na utapata tabu sana kufaidika nalo kibiashara. ni maoni tu mkuu
Uchawi, Unga, Leso - weka chochote - watu wasife moyo. Kazi bado ipo kubwa na huu ni mtapakanyo tuu - yaani ni pumba tupu kama hizi taarifa ni za kweli.
Alafu huyo ndio alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali yetu?? Kazi kweli tunayo
Angalau sasa watu watakoma kidogo kumfuata fuata Chenge. Kila siku makelele tu ambayo hayana msingi wowote. Tulieni tujenge nchi ndugu zangu na kuacha majungu. CCM hakuna mafisadi wowote na huyu Chenge anasingiziwa tu.
MASAKA...Are you serious or simply playing the devil's advocate with a light touch?
Makelele yasiyo na msingi indeed..ina maana vita vya wazalendo dhidi ya ufisadi wewe havikuhusu..au wewe ni mmoja wao? YOU DESERVE TO BE STONED TO.........................................
womenofsubstanc
Sintoshangaa nikija ambiwa kwamba huyu ndugu yetu alikuwa mmojawapo wa waandamaji na wapiga makofi kule Kiteto - (kwa Lowassa), kijijini kwa Chenge, na kule Ntwara alikopigiwa makofi Nkapa.
It makes no sense kwa mtu mzima mwenye uwezo wa kubonyeza keyboard ya computer akasema maneno haya. Nisingeshangaa kama ningeyasikia maneno haya kwa mtu wa kijijini ambaye hata pesa ya kununua kandambili hana.
Binadamu ni tofauti na wanyama. Tumepewa "utashi" ambao kama tunautumia vyema hatuwezi kuwa na fikra za dizaini hizo.
Alijiuzuru kupisha uchunguzi!na matokeo ya uchunguzi bado!iweje mtu ahukumiwe na kiutwa fisadi wakati ni uchunguzi tu?Alijiuzuru REMEMBER!!!!!!
mhh yatasemwa mengi tutumie akili kama ukumbi ulikuwa ushafungwa ina maana hata hao StarTV walikuwa nje na kamera zao.Zilitegwa vipi au zilikuwa nyuma yake zikimfata Andrea??
haya makubwa kama tv nazo zinaamini mambo ya ushirikina ambao unapigwa vita tanzania na afrika nzima.
UDAKU......
muda mfupi kabla ya mafundi wa StarTV kuondoka; haikutokea usiku wa manane. Na anayedhania ni udaku akalaghe bao.... hivi sasa kuna uchunguzi mkali unaendelea hapa. Kwenye kichwa cha habari sikusema utaalamu wa jadi a.k.a ushirikina. Mimi ni nzi sina imani za kishirikina, nafuata uchafu popote ulipo, naishi kwenye uchafu, nakula uchafu.. lakini mwenyewe nina afya. Hili ni kubwa mno hasa mkitoa imani za kishirikina pembeni.
ina maana hata huko bungeni, hawana wasaidizi ?? hii kitu nashindwa kuielewa, story nzima imekuwa badly staged, hivyo kuamini kwangu itakuwa vigumu ! Maelezo ya mtoa mada yanachanginyi !
Kiungani,
Bandiko linasema ukumbi ulishafungwa how comes waandishi wa Startv wabaki ndani ya ukumbi uliofungwa? ina maana walifungiwa ndani? Kwani hata Mh Chenge "aliposahau" kitu ilibidi "afunguliwe"
i cant afford to agree with this, cha msingi weka tapes ambazo zinadaiwa kuwepo ! other wise, this will be another ball rolling, huku watu wasidiscuss alichosema zitto ! maelezo yooote haya is nothing compared to a five second movie clio, tuonyesheni hata kidogo na tujudge wenyewe, lakini kujudge kutokana na maneno yanayotungwa, is like playing with our heads !
Polonium (pronounced /pəˈloʊniəm/) is a chemical element that has the symbol Po and atomic number 84. A rare and highly radioactive metalloid,[1] polonium is chemically similar to tellurium and bismuth, and it occurs in uranium ores. Polonium has been studied for possible use in heating spacecraft. It is unstable; all isotopes of polonium are radioactive.
Wewe Kitila, utakuwa kiongozi wa Tanzania bila ya kwenda Bagamoyo? Vipi mkuu unafikiri ni bure? Wakuu kina Zitto wanahitaji kukufunda mkuu,
Yaani bila sangoma na songi songi itakuwaje huwezi kuwa hata katibu tarafa vipi mkuu chi yako unakuwa kama mgeni?
Yule ni kama Muungwana anaingia pale au? Na mzungu mbele ya Muungwana nani yule ,au ni shemeji yake, Mrs. Sinclair? Jim aangalie!
Halafu hivi kwa nini Wangwana wa Bongo wanatembea na wa-Mura badala ya makachero wa kiraia?
Hamna kibaya sana, isipokuwa ila tu nadhani Vasco anapoenda sehemu sehemu kazungukwa na wa-Mura, anapoteza image of a civilian president.
Huyo mbele ya Muungana na Mama Sinclair, Kwi kwi kwi...
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kapteni John Chiligati, jana alimtaja mbele ya waandishi wa habari mbunge ambaye aliingia katika ukumbi wa Bunge jioni ya Jumatatu.
Tukio hilo linahusishwa na ushirikina kwa mujibu wa taarifa zisizo rasmi, ambazo zimekuwa zikisambaa kwa muda wa siku tatu zilizopita.
Ingawa hakumtaja kwa jina, Chiligati alisema kuwa mbunge huyo alikuwa waziri lakini sasa hana tena wadhifa huo.
Akifafanua, Chiligati alikiri kuwa mbunge huyo aliomba na kupewa ruhusa kuingia ndani ya ukumbi huo wa Bunge, ili kukagua na kuangalia nafasi atakayokuwa anaketi.
Alisema kuwa mbunge huyo alilazimika kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na kiti maalumu cha kukalia ndani ya Bunge kutokana na kuondoka kwake kutoka katika wadhifa wa uwaziri.
Chiligati alisema kwamba, kwa kuwa Bunge lilikuwa linaanza vikao vyake siku inayofuata, mbunge huyo aliona ni busara kutafuta mahali pa kukaa jioni hiyo, ili asisumbuke asubuhi.
Alikiri kuwa ni kweli aliingia ndani ya ukumbi wa Bunge na kupita katika kila kiti, akiangalia majina kwa lengo la kutafuta kiti kilichokuwa wazi.
Alisema wakati akifanya hivyo, hakuweka uchawi wowote kama ambavyo inadaiwa na watu hivi sasa.
Kwa taratibu za Bunge, kila kundi ndani ya Bunge hilo lina mahali pake maalumu pa kukaa kwa mpangilio unaoeleweka. Makundi hayo ni pamoja na mawaziri, ambao huketi upande wa kuume kwa Spika, wapinzani, ambao huketi upande wa kushoto wa Spika na wabunge wengine ambao hukaa katika nafasi zilizosalia.
Chini ya utaratibu huo, mpangilio wa kukaa hupangwa mwanzoni mwa Bunge, ambapo kila mbunge hupangiwa kiti chake cha kukaa. Hata hivyo, wabunge wanaruhusiwa kuhama kwa muda kwenda eneo jingine na wanapomaliza dharura hiyo hurejea kwenye viti vyao.
Spika Samuel Sitta, naye alishathibitisha kuwa, zipo picha zinazomuonyesha mbunge huyo akiwa ameandamana na mtumishi mmoja wa Bunge, akipita katika viti kadhaa ndani ya ukumbi huo wakati ukiwa umefungwa.
Ingawa Sitta na Chiligati waliepuka kumtaja mbunge huyo kwa jina, lakini kiongozi ambaye alikuwa waziri na kujiuzulu katika siku za hivi karibuni ni Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge.
Chenge alijiuzulu kutokana na kuhusishwa kwake kwenye uchunguzi unaoendeshwa na Taasisi ya Kuchunguza makosa ya rushwa ya Uingereza (SFO).
Makachero wa SFO walivutika kumchunguza Chenge katika uchunguzi wao dhidi ya Kampuni ya Bae Systems ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania rada kwa bei ya juu.
Licha ya kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati mkataba wa mauzo hayo unafikiwa, makachero wa SFO walimkuta Chenge akiwa na akiba ya takriban dola za Marekani milioni moja kwenye akaunti iliyo katika benki moja katika visiwa vya Jersey.
Tangu ajiuzulu nafasi hiyo, Chenge hajawahi kuhudhuria vikao vya Bunge, na ni kweli hivi sasa anawajibika kutafuta nafasi ya kukaa kwa kuwa hataweza tena kukaa katika nafasi ya mawaziri aliyokuwa akikaa zamani.
Tukio hilo limewaweka wabunge roho juu, hasa baada ya Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, kuugua ghafla katikati ya wiki iliyopita na kulazimika kukimbizwa katika kliniki ya Bunge ili kupata huduma za kiafya.
Wabunge kadhaa sasa wanaonekana kuogopa kuusogelea ukumbi wa Bunge, kutokana na taarifa hizo za kuwepo kwa vitendo vya kishirikina.
"Hili tukio limetutia hofu, tunadhani kuna kila sababu ya kukamilisha uchunguzi wa tukio hili mapema. Spika ameeleza kuwa tukio hili linachunguzwa, tunaomba lichunguzwe kweli, tena kwa haraka, ili kutuondolea hofu tuliyonayo sasa," alisema mmoja wa wabunge kutoka Mkoa wa Mwanza.
Mbunge mwingine ambaye pia hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alilieleza gazeti hili kuwa Spika anapaswa kutoa taarifa ya tukio hili bungeni na kulitolea ufafanuzi badala ya kuendelea kulizungumza kwenye vyombo vya habari.
"Hizi taarifa zipo, wabunge wengi wanazijua, lakini Spika analizungumzia kwenye vyombo vya habari. Mimi nadhani suala hili linagusa maisha yetu, ni bora akalieleza Bunge nini kilitokea," alisema mbunge huyo.
Akizungumza na waandishi juzi, Sitta alisema kuwa, ofisi yake imekabidhi picha za video zilizomnasa mbunge huyo akiwa ameambatana na Ofisa Mwandamizi wa Bunge kwa siri, waliokuwa wakiweka vitu vinavyoaminika kuwa vya kishirikina au aina fulani ya sumu kwenye kila kiti cha mbunge.
Kwa mujibu wa Sitta, picha za mkanda huo zilizonaswa na kamera za usalama zilizomo ndani ya jengo hilo la kisasa, zimefifia kiasi cha kushindwa kubaini kwa haraka watu wanaoonekana ndani ya mkanda huo.
Kutokana na hali hiyo, Sitta alisema ofisi yake imeamua kuukabidhi mkanda wa picha hizo kwa maofisa usalama wa taifa na kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, kwa ajili ya kuzifanyia uchunguzi zaidi.