Chenge, Lowassa na Rostam Aziz ni wamiliki wa PCCB?

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Kama CCM imeona Chenge, Lowassa na Rostam Aziz kuwa ni mafisadi, wala rushwa na waliojipatia mali kwa njia za wizi, je Takukuru wanangoja nini kuwaburuza mahakamani watu hawa? Au hawa vinara wa ufisadi ndio wamiliki wenyewe wa Takukuru?
 
Kikwete ndio kinga ya hawa jamaa. Hosea alipo hojiwa na Wikileaks alikiri kuwa Kikwete ndio kikwazo kikubwa cha mafisadi kufikishwa mahakamani.
 
CCM ndio imeshikilia dola. CCM ni chama cha kuwalinda mafisadi, kinafanya kila mbinu na jitihada ili mafisadi wasifikishwe mahakamani.
 
vile vijisenti vya new jersey chenge alisema sio vyake ni vya NGO . Je hiyo NGO iko wapi. Inashangaza kuona story ya vijisenti imesahaulika

Kama sio chenge kuziweka zile pesa za kifisadi kwa niaba ya "CCM" basi aliziweka kwa niaaba ya "wakuu fulani." Kama zingekuwa ni zake binafsi tungeona japo sinema na maigizo kama yaliyowakuta kina mramba.
 
Kama CCM imeona Chenge, Lowassa na Rostam Aziz kuwa ni mafisadi, wala rushwa na waliojipatia mali kwa njia za wizi, je Takukuru wanangoja nini kuwaburuza mahakamani watu hawa? Au hawa vinara wa ufisadi ndio wamiliki wenyewe wa Takukuru?

Nashangaa toka PCCB imeanzishwa hadi leo ina nini cha kujivunia. Hivi hizi taasisi zinafanyiwa evaluation kweli? nini kigezo cha kuzifanya ziendelee kuwepo kama haziperform kwa ufanisi na zinapokuwa zimeshindwa kabisa kufanya kazi zilizokusudiwa?
 
Kuna kitu watu wanaogopa kukisema ila kuna cindicate imeshawekwa mapema sana kulindana serikali....bros wamekaa tayari kusaidia DG PcccB,DCI,DPP wote hao wanalindana maana wamewekwa strategically....ilibakia usalama na mwanasheria mkuu(alitolewa kashfa) nae alikuwa bro......JK analijua hilo pia hawezi kuwagusa!!!
 
Nashangaa toka PCCB imeanzishwa hadi leo ina nini cha kujivunia. Hivi hizi taasisi zinafanyiwa evaluation kweli? nini kigezo cha kuzifanya ziendelee kuwepo kama haziperform kwa ufanisi na zinapokuwa zimeshindwa kabisa kufanya kazi zilizokusudiwa?

Tatizo ni system, hebu mpe Dr Slaa nchi, mwachie TAKUKURU hiyo hiyo a-deal na mafisadi!
 
Back
Top Bottom