Rostam Aziz ameiweka serikali ya Tanzania mfukoni? Kwanini hakemewi kwa kuleta nadharia ya chuki na kudharau hadharani mhimili muhimu wa nchi?

Misozwe

Member
Dec 23, 2022
21
26


Kwa nafasi yake katika jamii kama kiongozi mwandamizi mstaafu wa CCM na pia mfanyabiashara mkubwa mwenye ushawishi bila shaka Rostam Aziz anatakiwa awe makini sana na kauli zake kwenye public kwa sababu tulio wengi tunayapa uzito unaostahili maneno yoyote atakayosema.

Kwenye mkutano wa kujadili Tanzania uliofanyika hoteli ya Serena alisema watu wanapinga mradi wa uendeshaji bandari kwa sababu ya udini, jambo ambalo si kweli kwa sababu asilimia kubwa sana wanaoukosoa mkataba huo, wanakosoa tu vifungu vya mkataba, na nimesoma ule mkataba zaidi ya mara tatu sijaona sehemu yoyote inayotaja dini yoyote.

Pia akumbuke kuwa:

  • Mradi wa bwawa la Nyerere unatekelezwa na Arab Contractors ya Misri, taratibu zilifuatwa, hakuna aliyewahi kuhoji kipengele chochote.
  • Mradi wa SGR unaendeshwa na Waturuki, hawa walishinda kwa tenda, hakuna anayehoji.

Pamoja na kuhoji vifungu vilivyopo kwenye mkataba, jambo lingine la msingi linalokosolewa ni kwanini taratibu za manunuzi zilizowekwa kwa mujibu wa sheria hazikufuatwa. Watanzania wanahoji mambo ya msingi.

Kauli nyingine ni ile ya kudharau mahakama kwa kusema serikali inaweza kumpigia simu Jaji yoyote na kumwambia atoe hukumu ya aina gani. Hii ni dharau kubwa kwa mahakama ukiwa ni mhimili unaojitegemea.

Wiki na zaidi imepita sasa toka Rostam Aziz atoe kauli hizi na hakuna kiongozi yoyote wa serikali au CCM au mahakama aliyejotokea hadharani kumkemea mtu huyu kwa kauli zake hizi za hatari. Je, Rostam Aziz ameiweka serikali mfukoni mwake hakuna anayeweza kumkemea kwa chochote atakachosema? Hii ni aibu kwa taifa machoni mwa jamii zinazozingatia utawala bora.

Rostam anatakiwa atoke hadharani atutake radhi wananchi na mahakama.

Kauli kama hizi ni hatari kwa usalama na amani ya nchi. Kama alivyosema Mh Waziri Mkuu kwenye baraza la Iddi, tusichukulie poa amani iliyopo tukaona ni jambo jepesi, likitokea la kutokea tutatafutana. Nakumbuka kilichotokea Gongo la Mboto wakati wa ajali ya mabomu kwenye kambi ya jeshi, familia zilipotezana karibu wiki nzima, wazazi hawajui watoto wako wapi, wazee wasiojiweza walipata shida, walemavu ndio usiseme. Kitu kidogo tu kinaweza leta mtafaruku mkubwa

Kauli kama hizi sio za kuzichekea hata kidogo.
 
R.jpeg
 
Mkuu

Usijali,ngoma ikilia sana hupasuka!!

Ogopa sana unapopiga kelele wenzio wanakaa kimya wanakucheki tu!

Ni hatari sana!!
Hebu tuijadili hoja yake, alichokisema kinafanyika au hakifanyiki? Tuliwahi kuambiwa hadharani kwamba kuna Mhimili mmoja una mizizi mireeefu kuliko mingine au mmesahau?
 
Back
Top Bottom