Chenge ajiuzulu!

Ningemshauri sasa JK awe karibu na JF na asikilize USHAURU unotolewa hapa kulikokukutana na aibu hii


You can only be taken serious kama JF ilichangia pesa za uharamia wa kuiba kura na kutukana watu ili JK aukwae urais if not basi daima atakuwa na washikaji wake akina Kapuya etc.
 
Developing news....lakini nimeambiwa sasa hivi na mtu ambaye ni credible

It is true;He had resigned!!Amefungua mlango sasa!!Si utamaduni wa kwaida kwa viongozi wa Tanzania waliolewa madaraka kujiuzulu kupisha uchunguzi dhidi yao.Chenge kaona ngoma nzito!!Sasa atueleze what goes beyond Vijisenti??Atuambie ni kiasi gani anacho!Amepataje?Kama ni biashara,ni kodi kiasi gani amewalipa watanzania kupitia serikali yao?Kuna maswali mengi sana ambayo anaakiwa kuyajibu na yumkini yakawakumba akina Mkapa(Raisi wa Jamhuri hii aliyewahi kuwa na Kiburi kisichoelezeka!!!Nina imani sasa wanaJF watamuweka kitimoto na atasalimu amri kama alivyofanya kamaradi mwenzake chenge!!mjadala uendelee!!
 
There's nothing to jubilate here! Bado chenge ni mbunge, mnec and mCC wa ccm! Kwan nafasi hizo sio uongozi?? Ths s fucken business! We will jubilate resignation zao kama wataachia ngazi kwenye nafas zote! Including za chama! Wote lowasa,chenge, msabaha,karamagi. Vinginevyo bd hatujafanya kitu!
 
Hili linchi linatuumiza tu roho na kutia uvivu, Tumuuzie mmarekani afanye Dampo la Nyuklia tugawane pesa kila mtu akatafute maisha kwingine.

Imefikia sehemu nimekata tamaa.
 
Ila wakuu with all that said,, mtakumbuka kuwa alipoteuliwa mara ya pili mwezi February kinyume na matarajio ya wengi, alisema kuwa kwa wale wanaoshangaa wakamuulize aliyemteua (Mh Rais) ...sasa mi naona kama amemdalilisha sana JK katika hili!

Na pia najiulize je, kama JK alikuwa anayajua haya, assuming kuwa lishahabarishwa na RO, je alimwacha kwa makusudi aanguke mwenyewe na yeye akabaki kunawa mikono kama pilato?

Na huu msalaba ataubeba chenge peke yake au kutakuwepo na wa kumsaidia kama ilivokuwa kwa EL?


Narudia kwa mara nyingine tena, Mheshimiwa JK ni mtu mzuri na ana ubinadamu. Shida na maswali yetu ni kuhusu Uwezo wake wa kupambanua baya na jema tu.

Kwenye ile thread ya baraza jpya la mawaziri nilijiuliza sana kuhusu "competency ya mkuu wetu wa kaya" linapokuja suala la kuamua Nani awe waziri katika nchi ya Tanzania yenye watu takribani 38,000,000!! Niliijihoji sana vigezo gani mkuu anatumia kuamua watu wa kumsaidia kazi za kujenga nchi na kulinda watanzania.

Mheshimiwa Chenge (napata shida sana kumuita mheshimiwa, I wish na ubunge aachie)ni mtu ailiye katika FIRST ELEVEN ya Mkuu wa kaya sababu Baada ya mheshimiwa kupata 2nd chance ya kusafisha baraza aliona kuwa Katika hao raia 38M hakuna mchezaji kama Chenge. Piga ua jamaa hakukosa namba. Matokeo ya mechi kwa dakika hizi 10 za mwanzo yananifanya nihisi kuwa Mkuu wa kaya kaishiwa wachezaje. Sioni kama atakuwa na mtu wa kufaa kwenye cabinet hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba.

Well, asikate tamaa, hii ni nafasi yake nyingine kusafisha baraza. nafasi ya dhahabu kuepuka fedheha zaidi kama hizi. Heri lawama kuliko fedheha. hatakiwi kuangalia watu usoni katika kuamua nani awe waziri. Watu wa kuangalia usoni ni watanzania wanaoumia kwa dhambi za kina Chenge, Lowasa, Karamagi, Rostam Aziz, Mkapa, Yona, na kadhalika wengi.

UShauri wangu ni kuwa aweke watu ambao hatawaogopa kuwafuta kazi wakiharibu
 
Ningemshauri sasa JK awe karibu na JF na asikilize USHAURU unotolewa hapa kulikokukutana na aibu hii

unajua marais wetu hapo ndipo wanapokosea
JK naye angejiuzulu tu,hapo angepata sifa za ajabu na kuwa mfano wa kuigwa duniani kote.
 
Nilisema huyu atakuwa 'mbuzi wa kafara' kwa kushindwa kuficha 'vijisenti' vyake hadi vikaonekana. Litakalofuata sasa ni mahakamani na wale mafisadi wengine ambao hatuna ushahidi wanaendelea kupeta.

Ukisikia usanii wa kisiasa ndio huu!
 
....rais hawezi kujiweka mbali na kashfa za watu wake wa karibu wa mtandao..hatuwezi kuwa na prof mukandara"s principle eti....rais wetu ni mzuri ila watendaji wabovu......ubovu wa watendaji wa kisiasa hasa mawaziri unamaanisha ubovu wa principle wao...ningeweza kukubaliana na hii principle kama rais angekuwa safi,mawaziri safi alafu watumishi wa umma ndio wawaangushe...hapa tusingemlaumu sana rais kwa kuwa watumishi ni proffessionals ambao reform yao ni process......lakini la hasha watumishi wa umma kwa kiasi kikubwa wamebadilika sana ukilinganisha na mawaziri [wanasiasa]

hii serekali itaendelea kuwa ya kuumbuana na hatua ya mwisho msalabani asulubiwe mwenyewe rais jakaya kikwete...kwa spidi hii ya kudondoka msalabani wateule wake ...ipo siku matope yatamrukia na wananchi watataka asulubiwe.....hadidhi ya mbwa mwitu ...wakila nyama atakayebakiwa na madowa ya damu...nyama ikiisha basi naye hugeuzwa kitoweo.....
 
Truevoter,
There's nothing to jubilate here! Bado chenge ni mbunge, mnec and mCC wa ccm! Kwan nafasi hizo sio uongozi?? Ths s fucken business! We will jubilate resignation zao kama wataachia ngazi kwenye nafas zote! Including za chama! Wote lowasa,chenge, msabaha,karamagi. Vinginevyo bd hatujafanya kitu
Maneno mazito haya mkuu!..
We have to think again kwani walifanya kitu hadi sasa ni wao wenyewe kujiuzuru kwa faida yao.
 
Mimi naamini kabisa kama Mh.Kikwete ni msafi tena msafi wa uhakika.kama kuna wachafu basi hao walidandia basi la Mh.Kikwete na kutaka kumsaidia wakiweka matumaini kuwa atawapatia lifti ,mara nyingi wanaosaidia kusukuma gari nao hutaka msaada wa kufikishwa wendapo.
Kwa ufupi Mh.Kikwete hakuwa mwizi wa fadhila aliwapa msaada na kuwafikisha waendapo ,kama walikula dawa ili wapate nguvu za kumsaidia hilo litakuwa tatizo lao ,Mh.Kikwete hakutaka kujua jamaa walipata wapi nguvu za kulisukuma gurudumu lake la kupanda kilima cha Uraisi kwa kishindo ,yeye aliona tu kuwa gari limeshika kasi na kuondoka hivyo aliowapakia aliwasaidia kwa kuwalipa shukurani.Sasa kusema Kikwete alishinda kwa sababu wasukumaji wake walikula vidonge vya kuongezea nguvu ili waweze kulisukuma gurudumu na wao wapatiwe lifti ,hilo litawagusa hao waliotumia vidonge si kwa msukumwaji.Kawafikisha safari yao ,sasa kama waliiba fedha za kupata nguvu au hapo walipofikishwa ndipo walipokusudia kuiba ,that will be another case ,fagio la chuma likipitishwa inavyotakiwa Mh.Kikwete asiukumbuke ule wema aliotendewa kwani alikwisha walipa wema ,atimize majukumu ya Uraisi na kuangalia mbele awache sheria ichukue mkondo wake huku yeye akiwa msimamizi na kuwaeleza wasaidizi waliomsaidia kusukuma gurudumu kuwa kama angelijua ni majambazi asingeliwafikisha safari yao.

Msafi angechukua milioni ishirini za Wa-Iran ku finance uchaguzi kama ilivyoripotiwa na "Africa Confidential"?

Msafi angewachagua watu incompetent na wenye fraudulent degrees kama kina Mkulo,Nchimbi na kina Chenge weneye corruption allegations?

Give me a break.
 
...ni vigumu sana kumtenganisha kikwete na uchafu kwa kuwa ni rais aliyetokana na mbinu chafu...kwa hiyo simply ni mchafu....ni rais mfujaji wa pesa zetu walipa kodi kwa starehe..hata kama hachukui kama wenzake ...ni rais mwenye kiwango kidogo cha uelewa na usimamizi wa serikali yake...hafai!!!!
 
Hivi
JK anajisikia je? kila anayemteua ni fisadi na anajiuzuru.

Kama mimi ningekua Rais na mimi nigebwaga manyanga ,harafu ngoma inakua droo tunaona nani mjanja.

Ama naye anasubiri kale ka usemi katimie- siku ya mbwa kufa pua zote huziba

Hili sio tatizo la JK!!! Ni tatizo la kitafa...

  1. Nani alimchagua Chenge kuwa Mbunge ambayo ndiyo sifa no.1 ya kuchaguliwa kuwa waziri?
  2. Nani alimchagua Chenge kuwa mjumbe wa NEC ya CCM? JK au wanaCCM?
Kuwa makini kidogo, Sio kila kitu ni cha Rais vingine ni vya jamii nzima tuliyonanyo!!! sasa imebadilika... lazima tuelewe hivyo... Na JK anatuongoza vyema kwenye mabadiliko haya kwa kukubali wanaojiuzulu wajiuzulu...
 
Hutuwezi kumtofautisha JK na ufisadi hata kidogo, hatuwezi kusema Usalama wa Taifa hawakumwambia JK matatizo ya AC, JK anausika moja kwa moja na ufisadi wa mawaziri wake, atueleze ukweli tuendelee kumwamini kwa lipi.
 
Phillemon Mikael, wewe umemkazania JK, JK hawezi kutoka mpaka 2010.

In the meantime, since yeye ndio kashika mpini, ni vizuri kudeal na mafisadi ambao JK anaweza kuwabwaga au hata kuwashitaki mahakamani akiamua.

Ikifika 2010, then ndio uanze lawama nzito ili labda akose.

EM
 
Jmushi1,

Asante kwa kutohoa na kuchambua mustakabali wa Sirikali ya Mhishimiwa JK. Naunga mkono mawazo yako.

Wajumbe JF jamani kuweni na subira, watu kweli wana mengi moyoni kuhusu mwelekeo wa nchi yetu, hata kusahau mambo ya vituo sijui aya pale moyo unapoanza kumwaga "radhi" za dukuduku!

Unajua kwa jinsi serikali yetu ilivyo kwa sasa, ni aibu. Kila anayechaguliwa "kaoza", hivi hii nchi tunaiweka rehani hadi lini? Ukiangalia mbele huoni matumaini.

Walioko madarakani wanatunyia usanii wa hali ya juu. Tanzania inastahili kilicho bora zaidi. Tuko katika wakati mgumu sana Kitaifa, miaka mitano itapita kwa serikali watu wakijiuzuru na kupakana matope bila ya chembe ya maendeleo.

Sasa sijui nyimbo gani inaandaliwa. Ama kweli "pipa" hili liko "auto-pilot". Ni aibu. Wadanganyika ndio tunaoumia.

Hivi, nchi hii hakuna kabisa watu wengine wa kuongozaa?

Watu tulikuwa na imani sana na Kikwete. Waona mbali walisema, tukadghani, aah, hawa nao wana wivu wa kike (kama wasemavyo baadhi), sasa tunajionea wenyewe... Tunakwishaaa..

Rais anasimamia maslahi ya nani? Kwani ni lazima haohao ndio warudi? Je analipa fadhila? Watu hawabebeki.

Watu husema ukitaka kujua tabia ya fulani, angalia marafiki zake. Wote tunajionea. Hivi polisi wakikukuta kwenye kijiwe cha wavuta bangi, wao wakivuta, wewe huvuti, unadhani watakuacha? Utakwenda kuisaidia polisi.

Najaribu kuangalia mbele. Sioni. Kuna ukungu mzito.

Nchi imetekwa na wabadhirifu.
 
Hutuwezi kumtofautisha JK na ufisadi hata kidogo, hatuwezi kusema Usalama wa Taifa hawakumwambia JK matatizo ya AC, JK anausika moja kwa moja na ufisadi wa mawaziri wake, atueleze ukweli tuendelee kumwamini kwa lipi.

Kwa mantiki yako huwezi kumtofautisha mwanachi alimchagua Chenge na Ufisadi... nadhani hutendi haki... unless JK is not a human being!!!
 
Hutuwezi kumtofautisha JK na ufisadi hata kidogo, hatuwezi kusema Usalama wa Taifa hawakumwambia JK matatizo ya AC, JK anausika moja kwa moja na ufisadi wa mawaziri wake, atueleze ukweli tuendelee kumwamini kwa lipi.

are you serious????? hivi kelele zote hizi kuhusu usalama wa taifa kuwa mafisadi na kulinda maslahi yao hizioni????? hivi kweli kabisa unawalaumu usalama wa taifa kwa kutomshauri JK???
 
Kasheshe, kati ya wabunge wote waliochaguliwa na wananchi, kwanini alimchagua Chenge kwenye baraza lake mara mbili.
 
Back
Top Bottom