NakuliliaTanzania
JF-Expert Member
- Sep 24, 2007
- 555
- 7
Ni kweli kuna watu wengine hatumjui huyu Dr.Mauwa Daftari, Je unaweza kutuelimisha zaidi kuhusu mtu huyu. najua muda ni mali ila kwa kitu kama hiki sidhani kama utakuwa unaupoteza bali utakuwa unautumia ipaswavyo. Kwanza nataka kujua kama ni Dr. wa watu au ni title? Unaweza kutufahamiasha ana sifa gani za kuweza kuongoza wizara nyeti kama hiyo? sio kwamba ninam-grill ila naogopa kurudia makosa. Haitakuwa the same kama la aliyetangulia lakini impact yake ni ile ile...kurudisha maendeleo nyuma au kuwanyima wananchi accessibility previlage. Kama mlivyosema watu wengi wanasoma michango yetu, basi tuwe waangalifu tusiwapotoshe kwenye maamuzi yao.
Kwa kukumegea kidogo tu
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=6401Waziri aomba Mahakama Kuu imfutie kesi
Na Grace Michael
NAIBU Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Maua Daftari ameiomba Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kutupilia mbali kesi ya madai ya sh. milioni 500 iliyofunguliwa dhidi yake na mfanyabiashara, Bi. Fatma Salmin kwa kumkashifu.
Katika utetezi wake uliowasilishwa Mahakamani hapo mwishoni mwa wiki kupitia wakili wake, Bw. Peter Swai, Dkt. Daftari alieleza kuwa kesi hiyo namba 34/2008 haina msingi wowote kwa kuwa mdai hana kigezo cha kusimamia madai hayo.
Dkt. Daftari alidai kuwa madai ya mfanyabiashara huyo hayana msingi wowote kwa kuwa hakuna maneno yoyote yenye kashfa aliyoyatoa yenye lengo la kumkashifu kama ilivyodaiwa kwenye hati ya madai ya mlalamikaji....