Vesper-valens
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 5,287
- 7,388
Wakuu kwema?
Ebhana leo nimeona niongelee hii issue, Kuna Kundi jipya limezinduliwa siku za hivi karibuni (TNC)
TNC inaundwa na member wa tatu kutoka TMK wanaume family ambayo baadaye ilikuja kuvunjika na kuzaliwa makundi mawili yani TMK halisi na TMK family
Wazo la kuanzisha TNC naamini mwenye idea aliangalia vichwa vitatu katika kundi la TMK family wakapatikana Juma nature, Mh temba na Chege chigunda
Hivi vichwa vyote vilishawai kufanya vizuri sana kwenye muziki wa bongo fleva miaka ya nyuma lakini sio wote walioweza ku maintain mpaka sasa coz muziki wa sasa umebadilika kidogo kutokana na wakati
Tukiongelea ukweli kwenye TNC, Chege pekee ndio mpaka sasa anaweza akasimama mwenyewe na kutengeza Hit song, Lakini Mh temba na Juma nature ni kama muziki ushawaacha sana, yani hawana uwezo tena wa kutengeneza muziki utakao pendwa na kizazi cha sasa tofauti na Chege
Kuanzia kwenye branding chege ameweza kukimbizana na mahitaji ya soko la sasa, ukija kwa influence Chege ana mashabiki wengi kuliko wenzake ushahidi upo hata kwenye page yake ya instagram, kwenye interviews chege yuko smart sana kwenye kujibu, ukilinganisha na hawa wengine hususani juma nature
Haya yote chege ameweza kuwaacha sana nyuma wenzake kutokana na ukweli.jamaa alishaanza kujichanganya tangu zamani sana, licha ya kuwa member wa TMK hakua anaishi temeke kama hawa wenzake ambao miaka nenda rudi swaga zao ni zile zile hawataki kubadilika.
Ukija kwa juma nature licha ya kua na talent kubwa sana ila amepotea kutokana na ukweli watu walio nyuma yake sio sahihi, hawana cha maana wanacho mshauri zaidi ya kushinda bar kunywa pombe,
Mh temba naye hana kipaji kikubwa sana cha kuweza kufanya muziki pekee yake, combination yake yeye na chege ilimsaidia sana kukua kimuziki.
Ukiyangalia haya yote unaona kabisa kuwa Chege alivyokubali kurudi kuungana na hawa ndugu zake ni wazi amekubali kujirudisha nyuma kimuziki
Au nyie mnaonaje wadau?