Leo ni kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa P-Funk Majani, unakumbuka ngoma gani kali aliyoitayarisha?

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
1680210917069.png
Leo Machi 30, ni Kumbukumbu ya Siku ya Kuzaliwa kwa Paul Matthysse a.k.a P-Funk Majani, Mtayarishaji Mkubwa na Bora wa Muziki Tanzania.

Alianza kujihusisha na Muziki mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati akisoma International School of Tanganyika. Majani amehusika kwa kiasi kikubwa kujenga heshima ya Muziki wa Bongo Flava ndani na nje ya Nchi.

Kati ya nyimbo alizotayarisha ni Zeze ya TID, Mwanza Mwanza ya FID-Q, Zali la Mentali ya Prof. Jay, Hili Game ya Juma Nature, Kimya Kimya ya Jay Moe, Machoni Kama Watu ya AY, Bye Bye ya Inspekta Haroun, Nampenda Yeye ya Mh. Temba, Bijou ya Dully Sykes na nyingine ongezea hapo.
====

Paul Matthysse ndio jina alilopewa na wazazi wake, ila anafahamika kwa jina la P'Funk Majani, ni mtanzania mwenye mchanganyiko wa asili ya kidatchi.

Amezaliwa tarehe 30, mwezi March, mwaka 1976.

Wengi wanajiuliza kuhusu neno Majani katika jina lake limetokana na nini! huwa aneleza suala hili huku akiwa anacheka sana, tofauti na fikra za wengi, jina la Majani limetokana na tabia yake ya kupenda kula mboga za majani, anajulikana kama P 'Funk Majani

ELIMU

Amesoma katika shule ya IST (International School of Tanganyika), kisha alikwenda kujinoa zaidi katika chuo kikuu cha Netherland akichukua masomo ya Sound Engineering.

Kwenye Miaka 1991-92 wakati yupo bado shule IST (International School Of Tanganyika, Majani alikuwa mtundu kwenye studio za pale shule kwa kupiga- piga midundo mbali mbali ya hapa na pale na kufoka-foka na pia alikuwa mbele kwa kupiga muziki kwenye party mbalimbali.

P-Funk alikwenda kimasomo ya (sound) engineering kwa miezi 18 mjini Amsterdam, Netherland kabla hajaingia kwenye kutayarisha muziki. Maisha ya huko hayakuwa rahisi kwakuwa alikumbana na ubaguzi wa rangi wa hatari.

SAFARI YA MUZIKI Alianza kupenda muziki tangu akiwa shule ya msingi IST, inaelezwa kuwa alipendelea sana kupiga midundo mbali mbali ya muzki katika chumba maalumu cha muziki shuleni hapo. Mwaka 1992 huku akiwa ameunda kikundi cha muziki kilichokuwa kinajulikana kwa jina la 'Street Wisdom' kwa kipindi hicho alitumia muda wake mwingi kufanya muziki kwani ndio kitu alichokuwa akikipenda.

Mwaka 1995 akiwa na vifaa vyake vichache alianzisha kampuni yake ya kurekodi muziki nyumbani kwake. Na ni katika kipindi hicho hicho neno ’Bongo’lilipokuwa linatawala katika misemo ya kiswahili cha mitaani na lilikuwa linaelezea hali halisi ya maisha ya Dar es Salaam na ndio kipindi hicho album ya Bongo ilipozinduliwa.

Akiwa bado ni mtayarishaji muziki mdogo, amefanikiwa kupata umaarufu mkubwa katika fani ya muziki na hasa katika milipuko ya nyimbo zenye ladha ya Bongo. Anakubali kuwa amepata sana utaalam na mbinu kutokana na kufanya kazi watayarishaji wengine wa muziki wa Kitanzania kama Master J, Bonny Love na Rico. Mawazo yake na namna ya kuyaoainisha na muziki ndio hasa ambacho kinafanya muziki wake ufanikiwe.

Majani ana orodha kubwa ya wasanii nchini aliowatoa wakiwemo Juma Nature, Jay MO, TID, Solo Thang, Ngwair, Fid Q, Zay B, Sister P, Rah P, Daz Baba, Ferooz, Man Dojo na Domo Kaya, Mike T na bila kusahau kazi nyingi za Profesa alizozifanya yeye.

Ni ukweli usiopingika kuwa, P Funk aka Khalfan ama Mkono wa Mungu ndiye producer wa Tanzania aliyetengeneza hits nyingi zaidi kuliko mwingine yeyote. Bongo5 inamtakia Happy Birthday producer huyu machachari. Bado ana mchango mkubwa tu kwenye maendeleo ya muziki wa Tanzania.

Alikuwa anapenda kuimba muziki wa Hip Hop kwa kipindi hicho cha miaka ya 90, ingawa kwa sasa ni produza anamiliki studio ya Bongo Records, huku akibainisha kuwa studio hiyo imewatoa mastaa wengi.

Hakuwa nyuma kwa kuwa na mikakati ya kuufanya muziki utambulike kwani alikuwa ni mtu ambaye anaweza kuandaa 'concert' za uzinduzi wa albamu mbalimbali za wasanii waliokuwa chini ya lebo yake na aliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani kwa wakati huo hakuna msanii aliyeweza kuipita rekodi ya Juma Nature wakati wa uzinduzi wa albamu yake ya Ugali alipoweza kujaza mashabiki katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Mikakati hiyo bado anaendelea nayo kwa kuwaomba wadau wa muziki wajitokeze kudhamini shoo hizo kwani wananchi na mashabiki bado wanahitaji kuona wasanii wao wanafanya uzinduzi wa aina hiyo, hali hiyo itasababisha kuepusha wasanii kufanya uzinduzi wa single zao katika club huku idadi ya mashabiki wakizidi kupungua siku hadi siku.

Kwa sababu ya kupenda kuimba muziki wa Hip Hop mwaka jana prodyuza Pfunk aliamua kufufua kundi la muziki linaloundwa na watayarishaji wakali wa muziki wa bongo fleva akiwemo John Mahundi, Lamar huku wakiwa wameachia single yao inayojulikana kwa jina la 'No Name'

Mwaka 2019, alimtambulisha msanii mwingine Rapcha, anaefanya vizuri katika game ya mziki, hasa kwa kibao chake cha Lisa, kimemtambulisha vizuri, mashairi pamoja na biti kali za Majani zimenogesha kibao hicho.

TUZO Mwaka 2003 alipata tuzo ya Muundaaji bora wa Muziki 'Producer', wakati huo Tuzo za Muziki zilikuwa zikitolewa chini ya kampuni ya Bia ya Kilimanjaro zilijulikana ka Kili Music Awards. alibeba mfululizo tuzo hizo hadi mwaka 2006.
 
Jina la majani sio kwa ajili ya kula mbogamboga, alipewa hilo jina kwasababu ya mibangi.
Bila bangi huwezi tengeneza midundo kama Ile for sure....

Bila bangi majani asinge weza kuvumbua rhymes na midundo.....

Bangi hufanya kuamsha yule mtu wa ndani yako(dude la ndani😎).....
Bangi hufanya uwe na uwezo Bora wa kutengeneza kitu kuzuri...

Una vuta kidogo tena ukiwa umeshiba na hauna stress...🤓
Hata waheshimiwa wengi mbona wanapiga mjani....

Case closed
 
Kwa kipindi chote hakuna kazi mbaya ambayo aliwahi kufanya... zote ukizisikiliza zinaishi na kufariji mpaka kesho!

Beat kali, mashairi mazuri yaliyopangiliwa na ngoma zinafundisha, au hata zisipofundisha unapata burdan. Huyu na MJ respect sana kwao ingawa walikuwa wakali sana kwa vijana kipindi kile, ila faida ilionekana.
 
Back
Top Bottom