Changamoto za mwanamume kwenda kukaa nyumbani kwa wazazi wa mkewe

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Feb 18, 2010
4,066
4,085
Mwenzetu alipata misukusuko kazini yapata miezi nane iliyopita.
Ameyumba na sasa amefukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.
Wazazi wa mke wake wapo hapa Dsm na sasa wanamtaka mkwe wao akaishi nao nyumba moja.
Ungekuwa wewe ungefanyeje?
 
Kama ni watulivu na wana moyo wa upendo nitaenda la sivyo bora nikakae kwenye nyumba ya udongo kwa muda!
 
Yakikukuta ndo utatia akili lakini kwa kufikirika kila mtu atakuwa na majibu ya kijasiri
 
Mi naona ni sawa na wazazi wako tu, ila usikae muda mrefu jitahi sana baada ya muda mfupi uhame.
 
Mwenzetu alipata misukusuko kazini yapata miezi nane iliyopita.Ameyumba na sasa amefukuzwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi.Wazazi wa mke wake wapo hapa Dsm na sasa wanamtaka mkwe wao akaishi nao nyumba moja.Ungekuwa wewe ungefanyeje?
Binafsi ningehamisha famili yangu yote kwenda kwa wakwe lakini mimi mwenyewe ningetafuta mshikaji aliye single(rafiki wa kiume) ili anipe hifadhi ili niweke mambo sawa haraka. Wazo la kwenda kuishi kwa wakwe sio baya kama utaishi sio zaidi ya siku3 kinyume na hapo utadharaulika sana.
 
aisee inatisha unaweza kupigishwa dekki mzee mzima
ila inategeme HUYO mkeo na wewe na wakwe zako mna mahusiano makubwa kiasi gani
lool la sihivyo utajuta kuzaliwa wa kiume walahi
 
Back
Top Bottom