Chama gani mbadala kwa CCM?

UNAJUA MKANDALA ALIKUWA NDO KIONGOZI WA REDET ALIPOFANYA KWA BIDII KAZI WALOMTUMA AKALAMBA U V/CHANCELLOR,NAYA ANAOTA NDOTO YA UVC,huwaga namdharau sana huyu jamaa,na anapoongea sishtuki kuwa mwanazuoni anaongea,mpuuzi-mpuzeni.
 
:juggle:DR.BANNA MOJA YA WASOMI WENGI WATUMWA WA MAGAMBA,HAWAJIAMINI NA ELIMU ZAO KWAMBA WANA AMINI BILA KUTETEA MAGAMBA HADHARANI HAWAPATI VYEO.AIBU WANATUMIWA KURUBUNI UMMA WA WATANZANIA WACHACHE,WALIO USINGIZINI.CCM HAINA MVUTO KWA KUNDI LA VIJANA WENGI NA HASA WASIOTAFUTA AJIRA KWA VIMEMO.
SI YEYE TU TULIMSIKIA PALAMAGAMBA KWENYE ISHU YA KATIBA MPYA ALIVYOTETEA MAGAMBA.NINACHOJUA CCM NI WAATHIRIKA WA UKIMWI HATA WABADILISHE DAMU WAO NI WA KUFA KABLA YA 2015.
 
Ole wao wasio soma alama za nyakati.Jamani watu aina ya akina Bana huwa wapo nao wamo kwenye MSAFARA,ki uhalisia wanajua nini kinaenda kutokea then wanajaribu kupotosha jamii juu ya ukweli wa mambo kama njia ya kujihami. Hakuna asiye jua kama wao ni vibaraka wa CCM
 
Hiyo ndiyo ubaya wa elimu ya kukariri inayokupa cheti na siyo knowledge, pamoja ma elimu yake yote anashindwa kusoma hata alama za nyakati? Au anaongea kuwafurahisha watu fulani?

Hakuna kitu pale amebaki kutema mate tu akiongea Dr. hovyooooooo!!!
 
Huyu jamaa anawaaibisha academicians,usomi wake ni wa makaratasi,hawezi kufikiria nje ya box.
The handsome thing is, anajiaibisha mwenyewe, his researches produce the most embarrassing results and to his name lays the shame, ati watanzania asilimia ngapi sijui wanamkubali JK, it is a vivid lie! But to his name and only him, wengine kina Mkumbo wanaenda perfect, fact is fact, very ambiguous, it never changes. It is so unfortunate ma-Prof wengi wanagombea kwa tiketi ya magamba,cuz they think it an easy way, cha ajabu wakichemsha wanarudi kufundisha, hawa jamaa ni legelege mno, they are terrified by people of Mkumbos nature!
 
Dr. Bana, kwa hilo namuona ana muono wa upeo mkubwa sana.

Hivi uchukulie mfano wa magwanda, si watasusia nchi hawa mambo yakienda kombo kidogo. Mzee wa kiraracha nachama chake wamesha salim amri, NCCR ndio hoi bin Taaban, CUF ndio tayari na kushinda kwao uchaguzi wa visiwani lakini wamejijuwa kuwa chama chao hakiwezi kuongoza na wameridhia kuongozwa na CCM.

Bana kwa hili uko juu. Wengi sana wanafikiria kupiga kelele na kushinikiza maandamano na kususa ndio kuongoza? hapana. Wangeona mfano Egypt, huko sasa tunaona hata washabiki wa mpira wanauana hovyo.

Nadhani viongozi wa magwanda wameliona hilo na sasa wamebadilika, nilipowaona wanakwenda Ikulu na kunywa juisi kwa kashata nikajuwa, sasa hawa ndio wanaanza siasa, wakiendelea hivyo, baada ya miaka 20, wajukuu wa waasisi wa hiyo kampuni wanaweza kuongea mengine.
Mnafanana sana na Bana, whats really your point here, cha msingi ni nchi kutawaliwa na yields tuzione, it is somebody not some party, CCM mbona hakukaliki 2015! Kila mtu anataka urais, halafu, mind you that tutakuwa na wagombea binafsi, do't limit your thinking by closing yourself in that small dark box!
 
Mtanzania anekaa kila siku analalamika badala ya kuwacha uvivu na kufabya kazi kwa bidii, huyo hata ashushiwe malaika hatoacha kulalamika.

Fursa alizokuwa nazo Mtanzania leo hii, nchi nyingi sana duniani hawana. Lakini asiye na macho hawezi kuziona, asiye na masikio hawezi kuzisikia.
Fursa ziko vipi? Mpaka uhonge, upendelewe kwa sabababu mbalimbali, kisiasa, kidini etc! Mtu anapewa kwa mfano eneo kubwa la msikiti ajenge hotel, kwa sababu kesha honga, sijui km unaliona hilo ndugu! Corruption is the problem, CCM is too corrupted na n wazi kabisa tumeona watu wanapitisha mahawala zao kugomea nafasi mbalimbali na uwezo hawana, wanaharibu tu, wanakingiwa vifua wasiwajibishwe, what are you thinking, mabadiliko tena kuanzia na ninyi wanawake, start thinking independently, be emancipated, ma'ke wengi mnafikirai kuuza utu ili muishi maisha bora, halafu mnataka pia haki sawa;hakuna fursa sawa, na ndo maana mageuzi hayaepukiki, see for yourself 2015 msiwe na njozi tu ati Mungu atawasaidia!
 
...Dr Bana ...umeaibisha wasomi na usomi....,jibu ulilotoa lime base ..kwenye matokeo ya uchaguzi wa 2010..,,,

Mimi nilidhani umeongea "sasa",ukiwa na Ripoti ya kiutafiri ya sasa......

Je kwa sasa kwa wimbi la uongozii uliopo Sasa hakuna chama mbadala?
Kwa mfumko mkubwa huu asilimia ishirini wa bei hakuna chama mbadala...
Kwa uwezo wa hoja na kiongozi na hata kwa ushauri wanaoutoa kwa serikali ...hakuna chama mbadala...?
Kwa uchumi huu mbovu?? Kwa migomo hii ??
Unaongelea nguvu ndogo ya upinzania.....kwenye katiba ya sasa? Tume ya uchaguzi ?

Nadhani tuna haja ya kuwa na Shaka na maoni ya daktari Bana,,...

Phd YAKE KAPATIA WAPI HUYU MZEE?ASHABUNGULIWA NA MCHWA, NJAA NA ROHO MBAYA VINAMSUMBUA, MTU KASHINDWA KUWASAIDIA NDUGUZE ATASHAURI NINI NCHI HII YA ALMOST 43M, MUANGALIENI TU NA WEREDI WAKE WA MASHAKA, ANASHINDWA KUJUA UKWELI WA MAMBO NA HALI NZIMA YA KISIASA, KIUCHUMI, KIELIMU NA KIAFYA VIKOJE NA PHD YAKE?NAWEZA NIKAGHAILI KUSOME PHD KAMA PRODUCT NDO HIZI!
 
Kwa uchunguzi wangu wa harakaharaka watanzania wengi wanapenda mageuzi. Shida ni kwamba hawaviamini CHADEMA kwa sababu ya Ukaskazini na waislam wanakiona ni chama cha kikristo ikichagizwa na kufadhiliwa na Christian Demokratic cha Ujerumani. CUF ni chama cha kiislam. Hata wakane vipi lakini ndio vile wakristo hawakiungi mkono.TLP na NCCR ni choka mbaya. Chama pekee chenye usawa ni CCM ambacho kwa hakika wanachi wamekichoka. Ujio wa CCJ ulisubiriwa kwa hamu kabla ya kuja kusalitiwa na Sitta na Nape. Lakini wazee wa zamani wakijiengua CCM na kuungana na damu changa na kuleta chama kipya kwa hakika CHADEMA na CUF vitasambaratika na sasa tutaona mageuzi yenye usawa nchi nzima. Upinzani wa kweli utatoka CCM na rais wa kwanza kutoka upinzani Tanzania atatokana na kugawanyika kwa CCM. Machale yananituma Edwardkarim Ngoyai Lowassa ndiye atakuwa chanzo cha mgawanyiko huu.
 
Siku moja fisi alimuona kijana akitembea akadhani kuwa mikono yake ni mifupa inayokaribia kuanguka. Akamfuata hadi alipoingia ndani ya nyumba bila kupata alichotaka. Subiria ndoto yako hiyo. Huenda ikatokea!
 
Mkuu nilishawahi kusema mbadala wa CCM ni CCM, na CCM haimeguki, tunabadilishana uongozi tu, tunapeana nafasi siku zinakwenda, ukiweza unapewa ukifanya unamaliza, unapisha wengine, ndio maana tumeendelea kuona na kusikia wengi na bado tutaendela kuona na kusikia wengi..
 
Tumekuwa tukipambana na kuleta mabadiliko ya Kisiasa yaani Kuitoa CCM madarakani(kuipumuzisha)ila mimi binafsi sijapata mbadala wa CCM,lengo ni kutoa mtu aliyechoka(CCM)na Timu yetu imeshafungwa nne Bira(awamu za marais wetu),Mashabiki wameshoka kushangilia(Umasikini,maradhi,huduma mbovu za jamii,ufisadi),tunataka kufanya Mabadiliko(Sub)je tuingize SuperSub akabadilishe Matokeo au tufanye Mabadiko tu,bora liende,kama Zambia,Senegal,Kenya,Ghana
Au tubadili mfumo wa Uendesheji wa serikali
"Kiukweli bado sijaona Mbadala wa CCM yaani SuperSub"
Tunahitaji kubadilisha Maisha ya Watanzania ila si ulaghai wa Siasa
***Ni rahisi kwa vyama vya upinzani, kwa mfano, kuyalenga makombora yao ya lawama kwa vyama vinavyotawala kuliko kujichunguza vyenyewe na kuangalia iwapo vina sifa za uwajibikaji au za kujenga demokrasia.
#Heri ya Mwaka Mpya#
 
Back
Top Bottom