unakaribishwa.. Je unathibitisha kushiriki nikuweke kwenye orodha ya washiriki?
Zahoro Salim, ahsante kuthibitisha kushiriki. keep reading this post ili kupata update za mkutano..
waiting to hear from others.. SAA YA VITENDO NI SASA SI KESHO
its my first time to write here but l real like this idea, sijui wageni kabisa tunakaribishwa? kama ndivyo naomba niwepo pia.
Nimemwambia Tito akalipie ukumbi mkubwa kabisa ili tarehe 5february jumamosi saa nane mchana shughuli inaanza. Ni shughuli kweli kweli, mosi; kuhakikisha kama sura ya FL,NM,MJ ni hii iliyopo ktk avatar au sio na wengineo, pili; nini mwisho wa kikao.
ntakuja na samaki wangu mwenye kofia Ya Shark(papa)kama ilivyo kwenye Avatar yangu,mimi nimelipenda Tractor la Kanyagio,siju atakuja nalo from the Farm
Latest news,
Nimeongea na Tito akiwa Lunch Time sasa hivi, anasema amelipia ukumbi wa watu 35, anasema kila mtu akienda pale na Tsh 15,000/ atakuwa amelipia chakula cha mchana, mishikaki miwili,soda moja na ukumbi kabisa. Sasa naomba watu wajisajiri kwa Kanyagio kwa kulipia kupitia M-pesa, Tigo au Airtel. Tufanye hivi ili watu washiriki wakiwa na afya ya akili.
wanajamvi
Nachukua nafasi hii kuwafahamisha kwamba kamati ndogo ya maandalizi ya mkutano wa "CHAI Day:fursa katika Kilimo na ufugaji" inapendekeza kwamba mkutano huu ufanyike JUMAMOSI tarehe 5 Februari 2011 kuanzia saa 8.00 mchana (narudia saa 8.00 kamilI MCHANA). pale Lunch Time Hotel iliyopo Mandela Road karibu na kituo cha Hostel na pia karibu na Ubungo External jijini Dar es salaam. Mwenye mawazo tofauti naomba aseme.
Mkutano utachukua takribani masaa 4. naambatanisha rasimu ya ratiba ili muweze kutoa mapendekezo yenu!!