CHAI Day 5 Feb 2011 Dar: Kujadili fursa katika Kilimo na ufugaji

Nimeongea na Tito juu ya ukumbi wa Lunch Time Hotel, na Tito kampigia mhusika na tumepewa ukumbi ule mkubwa ( Kanyagio anaukumbuka) tuliofanyia chai day ya pili. Amesema kesho anakwenda kulipia advance ya Tsh laki moja ili ukamatwe kabisa. Ukumbi ule ni laki mbili. Kwa sasa anasubiri majibu yetu ili kesho akalipie ukumbi ule. Kama nilivyosema,pana parking kiasi ya kutosha, ulinzi upo, kiyoyozi kipo na choo ndani kwa ndani ukumbini, nyama choma ipo kwa watumiaji, ni patulivu hapa kelele. Ni opposite na Mabibo Hostel Mandela road.

Nasubiri jibu wakuu.
 
AHSANTE SANA Malila kwa update hiii. ukumbi naufahamu ni mzuri. Je kwa bei hii ni siku nzima au masaa machache.. na je umeme ukikatika inakuwaje in terms of upatikanaji wa generator (na kama wakiwasha generator wanapandisha bei). tukumbuke kuwa bei hii ni kwa ajili ya ukumbi tu so tutaongezea hela kidogo kwa ajili ya refreshment). naomba members wengine watoe maoni yao haraka iwezekanavyo ili tuone kama LUNCH time (ubungo external) uchukuliwe huo au utafutwe mwingine kama Rombo View Hotel. tunaoma ushauri wenu wa mwisho kabla kukamilisha suala la ukumbi.

Nakushukuru sana malila kwa update yako. namshukuru sana TITO kwa juhudi zake (inatia moyo jamani)

mpaka sasa watu waliokwisha thibitisha kushiriki ni wafuatao:

  1. KANYAGIO
  2. MALILA
  3. MGOMBEZI
  4. KASOPA
  5. ZAHOR SALIM
  6. NEW MZALENDO
  7. TGS D
  8. REALTOR
  9. MASAKI
  10. STREET SMART
  11. ELNINO
  12. LEN
  13. BABALAO
  14. TITO
NOTE: kuwa watu wachache kama wawili watatu ambao si members wa JF ambao wamethibitisha ushiriki wao (sijaweka majina yao hapa).
naomba wale wote wanaohitaji kushiriki mkutano huu watoe uthibitisho..

katika siku chache zijazo tuta-share timetable/agenda
 
Asante kwa wale wote waliotoa confirmation ya kushiriki katika kikao hiki (CHAI DAY), nimefuatilia hizo confirmation za ushiriki na kuwa na list ifuatayo:

  1. KANYAGIO
  2. MALILA
  3. MGOMBEZI
  4. NEWMZALENDO
  5. KASOPA
  6. ZAHOR SALIM
  7. TGS D
  8. REALTOR
  9. MASAKI
  10. STREET SMART

Samahani kama kuna yeyote ameshatoa confirmation na nimesahau kumweka katika list; vile vile wadau ambao bado hawajatoa confirmation ya ushiriki wao nafasi bado ipo.

Nakubaliana na pendekezo la ukumbi wa Lunch Time Hotel;. Kuhusu confirmation nafikiri tungeweka minimum number of participant ambao watawezesha kukodiwa ukumbi huu kutokana na idadi ya watu inayohitajika katika ukumbi husika. MALILA ukumbi huu unaweza kuchukua watu wangapi kwani baadhi yetu hatukuhudhuria CHAI DAY ya mwaka jana.

Tumekuwa tukitoa confirmation zetu hapa jukwaani; bali ili kuepusha baadhi ya washiriki kuingia mifukoni mwao katika kulipia gharama zitakazojitokeza, napendekeza kuwepo na utaratibu wa kuwa na malipo ya awali ambapo hiyo itaweza kutumika as FULL CONFIRMATION ya kushiriki. Tunaweza kumteua mwandaaji mmojawapo (napendekeza - KANYAGIO) kukusanya michango hiyo kwa njia ya M-PESA au njia nyingine mbadala itakayokuwa rahisi kwa wengi. Kwa tathmini ya awali tulioonyesha nia ya kushiriki kikao hiki tumefikia idadi ya 10, hivyo basi kama ukumbi uliopendekezwa utagharimu Tsh 200,000 itabidi kila mshiriki kuchangia Tsh 20,000. Kadri idadi itakavyoongezeka gharama ya kuchangia kwa kila mtu itapungua, kwa hiyo malipo ya awali tunaweza kuweka minimum Tsh 10,000.

Naomba kuwakilisha.
 
Naomba kesho kanyagio unikumbushe ili tujue suala la umeme inakuwaje. Waalikwa ni wengi mno ambao nina uhakika watakuja. Ukumbi ule unaweza kuchukua watu 50 hivi tukiwa tumekaa.
 
AHSANTE SANA Malila kwa update hiii. ukumbi naufahamu ni mzuri. Je kwa bei hii ni siku nzima au masaa machache.. na je umeme ukikatika inakuwaje in terms of upatikanaji wa generator (na kama wakiwasha generator wanapandisha bei). tukumbuke kuwa bei hii ni kwa ajili ya ukumbi tu so tutaongezea hela kidogo kwa ajili ya refreshment). naomba members wengine watoe maoni yao haraka iwezekanavyo ili tuone kama LUNCH time (ubungo external) uchukuliwe huo au utafutwe mwingine kama Rombo View Hotel. tunaoma ushauri wenu wa mwisho kabla kukamilisha suala la ukumbi.

Nakushukuru sana malila kwa update yako. namshukuru sana TITO kwa juhudi zake (inatia moyo jamani)

mpaka sasa watu waliokwisha thibitisha kushiriki ni wafuatao:

  1. KANYAGIO
  2. MALILA
  3. MGOMBEZI
  4. KASOPA
  5. ZAHOR SALIM
  6. NEW MZALENDO
  7. TGS D
  8. REALTOR
  9. MASAKI
  10. STREET SMART
  11. ELNINO
  12. LEN
  13. BABALAO
  14. TITO
NOTE: kuwa watu wachache kama wawili watatu ambao si members wa JF ambao wamethibitisha ushiriki wao (sijaweka majina yao hapa).
naomba wale wote wanaohitaji kushiriki mkutano huu watoe uthibitisho..

katika siku chache zijazo tuta-share timetable/agenda

Asante Mkuu Kanyagio!

Nafikiri wakati wewe unakusanya hiyo list ya washiriki nami nilikuwa najaribu kufanya hivyohivyo, naona list yako imefikia watu 14. Hata nami kuna mshiriki mmoja ambae sie JF member nitaambatana nae.
 
Wazo la kutuma Pesa in Advance ni Zuri na Jema kwa waandaaji inatoa peace of mind.Mkuu Kanyagio tunaomba means za kukutumia confirmation by M-Pesa or Tigo or Zap.
 
Mgombezi, wale ambao hawapo katika orodha yako uliyobandika hapo juu ni kuwa walinitumia PM mf. elnino, babalao etc. Kwa kuwa idadi ni 50 so itabidi tuweke limit ya watu 50 (hili ni pendekezo)- otherwise watu watakosa sehemu ya kukaa.
aidha nakubaliana na wazo la Mgombezi kuwa ni vema tuweke utaratibu wa malipo kabla (in case kuna uwezekano)
 
jamani nasikitika kwamba sitaweza kuwepo pamoja nanyi,natamani sana kama ningeweza kuhudhuria sababu najua ningefaidika na mengi.
Kwa sasa siko Dar ndio maana sitaweza kuhudhuria.
KWA VILE NINA AMINI KTK NGUVU YA MAOMBI,BASI NITAKUWA PAMOJA NANYI KWA NJIA YA KULIOMBEA ZOEZI ZIMA LIFANIKIWE NA KUTUNUFAISHA SOTE.
 
Naam,

Jamaa yetu Tito amenihakikishia kuwa jenerator lipo standby na hakuna malipo ya nyongeza. Kwa hiyo naomba tumpe kibali alipie kabisa. Nasubiri majibu toka kwenu wakuu.
 
kimsingi tukubaliane kwamba akalipie hapo ili tuwe na uhakika wa ukumbi!! bila shaka ukitoa hiyo hela ukumbi unakuwa wako siku nzima!!
 
Kanyagio, Malila na wajasiriamali wote mliochangia hapa MUBARIKIWE sana mmekuwa kiungo kikubwa sana kwetu na naomba muendelee hivyo!

Namshukuru Mungu kwa kutuanzishia mwaka kwa kuazimia jambo jema namna hii! Hii hakika ni baraka kwetu!

Nimeku PM mkuu Kanyagio kukubali mwaliko pamoja na mchango wangu!

Mwaka jana sikubahatika kutimiza lengo langu; lakini hawa wakuu walinisaidia kuweka misingi amabyo kwayo ni rahisi kwangu safari hii kuiendeleza.

Haya shime tutaarifiane kuhusu mchango na nai atumiwe ili tutimize lengo letu la kwanza kwa mwak 2011!
 
Labda niongeze angalizo..........ni vyema yeyote aliye na fununu juu ya SAGCOT ambayo kwa kiasi kikubwa inaangukia eneo ambalo tayari tumeweka mizizi akazileta na tukajifunza ni kwa namna gani tutanufaika nayo!
 
wanajamvi
Nachukua nafasi hii kuwafahamisha kwamba kamati ndogo ya maandalizi ya mkutano wa "CHAI Day:fursa katika Kilimo na ufugaji" inapendekeza kwamba mkutano huu ufanyike JUMAMOSI tarehe 5 Februari 2011 kuanzia saa 8.00 mchana (narudia saa 8.00 kamilI MCHANA). pale Lunch Time Hotel iliyopo Mandela Road karibu na kituo cha Hostel na pia karibu na Ubungo External jijini Dar es salaam. Mwenye mawazo tofauti naomba aseme.

Mkutano utachukua takribani masaa 4. naambatanisha rasimu ya ratiba ili muweze kutoa mapendekezo yenu!!
 
Attachments

  • agenda.doc
    43 KB · Views: 91
Ikifika mpaka saa nane hakuna jibu tofauti itabidi nimwambie Tito akalipie ili tujue tuna kazi moja tu.
 
kimsingi tukubaliane kwamba akalipie hapo ili tuwe na uhakika wa ukumbi!! bila shaka ukitoa hiyo hela ukumbi unakuwa wako siku nzima!!

05 FEB 2011 - CHAI DAY (zimebaki siku 10)

Nakubaliana na hoja ya kulipia ukumbi huu, malipo ya awali yafanyike.

Mkuu KANYAGIO, kuna jinsi ambayo tunaweza kukuwakilishia michango yetu in advance as our final confirmation.

Kuhusu agenda; kuna wadau walitoa mapendekezo kama ifuatavyo:

Mkuu MALILA:
Naomba nichangie baadhi ya maada tutakazo jadiliana nazo.

1. Je kilimo,ni shughuli ambayo mwajiriwa anaweza kuifanya bila kuathiri ajira yake?
2. Je eneo lipi la kilimo linaweza kuwa na tija siku za usoni?
3. Matatizo makubwa ktk kukusanya mtaji wetu ni yapi?

Mkuu REALTOR

Mkuu Kanyagio nashukuru kwa hii taarifa, mimi pia nitaudhuria. Mchango kidogo kwenye agenda, baada ya kufahamiana:

1. Kujadili muundo wa kuanzisha hii farm; Company limited, company imited by guarantee and having no share capital? Saccos? NGO?... Mamuzi ya muundo utatokana baada ya kujadili lengo kuu la kuanzisha farm, dira yetu na malengo kwa ujumla.
2. Kuchagua uongozi
3. Mpango kazi

Nafikiri katika kikao hiki tunaweza kujadiliana zaidi agenda ambazo Mkuu REALTOR ame – propose na nyinginezo, bali itategemea na muda tutakaokubaliana.
 
mgombezi
naomba uangalie hiyo ratiba ambayo nimeiambatanisha (attachment) katika email ya awali!!!
 
wanajamvi
Nachukua nafasi hii kuwafahamisha kwamba kamati ndogo ya maandalizi ya mkutano wa "CHAI Day:fursa katika Kilimo na ufugaji" inapendekeza kwamba mkutano huu ufanyike JUMAMOSI tarehe 5 Februari 2011 kuanzia saa 8.00 mchana (narudia saa 8.00 kamilI MCHANA). pale Lunch Time Hotel iliyopo Mandela Road karibu na kituo cha Hostel na pia karibu na Ubungo External jijini Dar es salaam. Mwenye mawazo tofauti naomba aseme.

Mkutano utachukua takribani masaa 4. naambatanisha rasimu ya ratiba ili muweze kutoa mapendekezo yenu!!

Asante Mkuu Kanyagio:

Naunga mkono agenda ulizoambatanisha, naamini kushirikiana na Mkuu MALILA mtaweza kuwapata wawezeshaji katika kila agenda.

"PAMOJA TUNAWEZA"
 
Asante mkuu Kanyagio; lakini nahisi muda hautoshi ila ningeshauri walau uuwekee 2 extra hours za ziada!

Pia naomba tuijadili fursa ya SAGCOT narudia...........wadau mlio karibu na jiko kama mna fununu!
 
Asante Mkuu Kanyagio:

Naunga mkono agenda ulizoambatanisha, naamini kushirikiana na Mkuu MALILA mtaweza kuwapata wawezeshaji katika kila agenda.

"PAMOJA TUNAWEZA"

Ili mjadala uwe mtamu, tusiwe na wawezeshaji toka nje ya timu yetu,watokane na sisi wenyewe ili tupate maana kamili ya kukutana kwetu. Nashauri kila mmoja awe huru kutoa maoni ni wapi anaweza kuchangia kwa kiasi anachojua ili tukiunganisha tupate jambo letu.
 
Back
Top Bottom