Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Sasa chaguzi zinafutwa hovyo
=====
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefuta chaguzi tano za Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kutokana na kukiuka Katiba, Kanuni na taratibu za uchaguzi.
Hayo yamesemwa leo Jumanne Septemba 27, 2022 na Katibu wa Halimashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Hamdu Shaka baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Amesema changamoto ziko katika jumuiya zote za chama hicho na kwamba idadi kamili ya malalamiko waliyoyapokea haijajulikana kwasababu bado wanaendelea kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi.
“Mfano hadi kufikia juzi, kwa upande wa vijana (UVCCM) kuna chaguzi zaidi ya tano zimefutwa na lakini kwa upande wa wanawake kuna chaguzi zaidi ya tatu zimesimamishwa,”amesema bila kutaja maeneo ambako chaguzi hizo zimefutwa.
Amesema Jumuiya ya wazazi haina malalamiko mengi lakini kwa upande wa jumuiya nyingine bado wanaendelea kufanyia kazi malalamiko yao na wanafuatilia kwa karibu.
“Chama kinafuatilia sana mwenendo wa chaguzi hizi na pale itakapobainika kuwa haki haijatendeka pale itakapobainika kanuni na taratibu zimekiukwa basi hatua za kufuta ama kutengua matokeo hayo hazitasita kuchukuliwa,”amesema.
Ametoa wito kwa wana CCM kuheshimu Katiba ya chama hicho na kuheshimu kanuni za chama ili kupata viongozi walio bora wakuongoza nafasi mbalimbali.
Amesema hapo ndipo wanajenga msingi ambao utakuja kuwavusha kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na 2025.
Amesema chama kitahakikisha kinasimamia kuhakikisha kuwa haki inapatikana mahali ilipopindishwa.
Shaka amesema wanafuatilia sana masuala ya rushwa katika chaguzi zinazoendelea ndani ya chama na kwamba hilo ni eneo ambalo watasimamia kwa nguvu kubwa
Kuhusu kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa, Shaka amesema wamefanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wenyeviti wa ngazi za wilaya katika wilaya 168 za chama.
Amesema uchaguzi wa wenyeviti wa wilaya wa CCM utafanyika Oktoba Mosi hadi 2 mwaka huu.
Aidha, Nec imeongeza muda wa kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea wajumbe wa NEC.
Chanzo: Mwananchi