Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,950
- 711
Kama CHADEMA hawamtambui Rais:
1. Watashiriki kupiga kura za kumpitisha/kutompitisha waziri mkuu? Waziri mkuu hupendekezwa na Rais, kushiriki katika kumpigia kura ni kutambua huyo aliyemleta ni Rais halali.
2. Baada ya waziri mkuu kupitishwa, wataweza kumuuliza mwaswali yeye pamoja na mawaziri wengine, ambao wote wameteuliwa na Rais wasiyemtambua?
Ndugu zangu wana JF, tamko hili la CHADEMA ni la kisiasa tu na halitekelezeki. Sababu kubwa ni kwamba wabunge wa CHADEMA hawawezi kugive-up ubunge wao - kwa katiba ya Tanzania kama humtambui Rais huwezi kuwa mbunge.
Mkuu hapa kweli tunahitaji kupata elimu kuhusu katiba yetu. Nina hakika Rais anachaguliwa na wananchi kama vile wabunge kwa kupigiwa kura. Sasa iweje upoteze ubunge kisa humtambui Rais kwa sababu ya wizi wa kura uliompeleka ikulu?? Mimi ni mbumbumbu wa katiba but vitu vingine havihitaji kwenda darasani, wote tumepigiwa kura.
Katika mfumo wa chama kimoja mtu uliweza kufukuzwa uanachama na ukapoteza ubunge. Sasa nitoke chama kingine ni vipi chama kingine kije kinivue uanachama!! Kama kweli katiba yasema hivyo, basi ndiyo utaona umuhimu wa kurekebisha katiba yetu.
Ni kifungu gani kwenye katiba kinasema hivyo, eti husimbomtambua Rais basi nawe si mbunge tena? Sorry, napendwa kuelimishwa tafadhali.