winner forever
JF-Expert Member
- Mar 6, 2012
- 1,095
- 269
Kila kheri makamanda,
Na ZITTO naye atahudhuria hicho kikao?
Idiot!
Ningependa kuishauri CDM waachane kabisa na M4C kwani kama ni vita basi haina tofauti na vita ya MAJIMAJI.Imebeba dhana na mbinu dhaifu.
Hamna lolote la maana kwenye mkutano huo ni ulaji tu wa posho
Tumeshapata solution ya kuidhibiti CDM kumbe tukitaka kuizuia kabisa M4C isiendelee ni kuua wananchi wanao shiriki hiyo mikutano, BHAAAASI!!!!!!!Waje na kitu ambacho kitawaonesha kuwa hatimaye wanaelewa uzito wa kile kinachowakabili. Maana tangu 2010 bado wanaonekana walikuwa wanaamini kuwa wanaweza kuishawishi serikali ya CCM to be nice to them...
Kwa hiyo CCM wamefanikiwa ???
Acha unafiki, hujawahi kushiriki maandamano hata mara moja. Wewe bingwa wa kuchochea tu. Upo Kigoma, wakija huko tutakupima, kwa sasa endelea kuvua samaki.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha operesheni yake ya M4C mkoani Iringa na kuitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu.
Kikao hicho cha Kamati kuu kitafanyika siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam chini ya viongozi wake wakuu Mkiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.
Mkuu wa operesheni M4C Benson Kigaila amesema haiwezekani kuendelea na operesheni huku polisi wakiua watu kwenye mikutano ya CDM kwa maelekezo maalum. Amesema Kamati kuu itatoa mwelekeo rasmi wa chama kuhusu hali hii ambayo haiwezi kuvumiliwa.
Pia inatarajiwa kamati kuu kujadili vitisho vya msajili wa vyama John Tendwa dhidi ya chama hicho,msajili ambaye watanzania wengi wanaamini ni kada mwaminifu wa chama tawala.
Source: Tanzania Daima/Majira.
Uchaguzi haupiti ,upo na unakuja ,jiandae kuwaondoa wahuni,wanyang'anyi,wezi,majangili wahujumu uchumi wafanyabiashara wa ikulu mdarakani. Wanaojenga au wanaohitajika kujenga nchi ni waliok serikalini sio vyama vya upinzani.
Kujenga shule wananchi wachangie ,kujenga vituo vya afya wananchi wachangie ,kujenga balabala wananchi wachangie ,kujenga soko wananchi wachangie ,kujenga vituo vya polisi wananchi wachangie ,hivi serikali iliyopo madarakani kazi yake ni kitu gani ?
Aloo huu si wakati wa kuturudisha katika siasa za kichina ,serikali mbali ya kodi inakusanya mapato kutoka nyanja mbalimbali ,yakiwemo kutoka kwenye madini ,misitu ,utalii ,vitalu vya kuwinda mbali ya pato la gesi ,hela yote inakwenda wapi ,huu msemo wa kusema wananchi wajitolee ni kuwafanya WaTz wote wapumbavu na wenye akili taahira ,isipokuwa wachche nyie mliozidiwa na akili.
Zanzibar ikiwa watafanikiwa kujipapatua na kuweza kufukua mafuta na kuchimba gesi basi uhakika wa kila raia kulipwa upo ,tena sio chini ya dola sitini kwa mwezi ,kwa maana ule msemo wa wananchi wanatakiwa wjitolee hautakiwi ,kwani Nchi haiendi vitani.