CHADEMA yasitisha oparesheni M4C na kuitisha kikao cha Kamati Kuu

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha operesheni yake ya M4C mkoani Iringa na kuitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu.

Kikao hicho cha Kamati kuu kitafanyika siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam chini ya viongozi wake wakuu Mkiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.

Mkuu wa operesheni M4C Benson Kigaila amesema haiwezekani kuendelea na operesheni huku polisi wakiua watu kwenye mikutano ya CDM kwa maelekezo maalum. Amesema Kamati kuu itatoa mwelekeo rasmi wa chama kuhusu hali hii ambayo haiwezi kuvumiliwa.

Pia inatarajiwa kamati kuu kujadili vitisho vya msajili wa vyama John Tendwa dhidi ya chama hicho,msajili ambaye watanzania wengi wanaamini ni kada mwaminifu wa chama tawala.

Source: Tanzania Daima/Majira.
 
Hivi huyu Tendwa alivyoumbuka kule Arumeru na hadithi zake za Washiri bado tu hajakoma?
 
Uchaguzi haupiti ,upo na unakuja ,jiandae kuwaondoa wahuni,wanyang'anyi,wezi,majangili wahujumu uchumi wafanyabiashara wa ikulu mdarakani. Wanaojenga au wanaohitajika kujenga nchi ni waliok serikalini sio vyama vya upinzani.

Kujenga shule wananchi wachangie ,kujenga vituo vya afya wananchi wachangie ,kujenga balabala wananchi wachangie ,kujenga soko wananchi wachangie ,kujenga vituo vya polisi wananchi wachangie ,hivi serikali iliyopo madarakani kazi yake ni kitu gani ?

Aloo huu si wakati wa kuturudisha katika siasa za kichina ,serikali mbali ya kodi inakusanya mapato kutoka nyanja mbalimbali ,yakiwemo kutoka kwenye madini ,misitu ,utalii ,vitalu vya kuwinda mbali ya pato la gesi ,hela yote inakwenda wapi ,huu msemo wa kusema wananchi wajitolee ni kuwafanya WaTz wote wapumbavu na wenye akili taahira ,isipokuwa wachche nyie mliozidiwa na akili.

Zanzibar ikiwa watafanikiwa kujipapatua na kuweza kufukua mafuta na kuchimba gesi basi uhakika wa kila raia kulipwa upo ,tena sio chini ya dola sitini kwa mwezi ,kwa maana ule msemo wa wananchi wanatakiwa wjitolee hautakiwi ,kwani Nchi haiendi vitani.
 
Mimi napendekeza tuandamane dhidi ya huyu Msajili wa vyama vya siasa. Lakini maandamano yetu yawe ya ujumbe wa simu kwa siku 3 mfululizo, tukimtaka asimamie haki kwa vyama vyote. Ujumbe wetu usomeke "SOTE TUNA HAKI, KWANINI IWE YA CCM TU?". Kwa wingi wetu tukipeleka text msg kwa siku 3 mfululizo, kwanza tutaonyesha jinsi tunavyoguswa Watanzania kwa ujumla wetu, pili, tutazuia mawasiliano na yoyote kupitia namba zake za mkononi.

Tuwekewe namba zake zote za mkononi tuanze maandamano yetu. Nakumbuka hili lilifanyika kipindindi kilichopita baada ya kuanzishwa na Mwanakijiji na lilikuwa na mafanikio makubwa sana
 
nchi hii imefika hapa pabaya sababu ya professional kuchanganywa na siasa. Mungu awe nanyi CDM
 
CUF walipakwa matope ya rangi zote, na hata umauti, lakini hadi leo hii na hata kesho, CCM hawana chao Pemba. Tupo smart sana, kuliko wanavodhani. Tumetulia kama wajinga, kama ma-****, lakini uhakika ni kwamba ccm na wapambe wao have to find save heaven.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Uchaguzi haupiti ,upo na unakuja ,jiandae kuwaondoa wahuni,wanyang'anyi,wezi,majangili wahujumu uchumi wafanyabiashara wa ikulu mdarakani. Wanaojenga au wanaohitajika kujenga nchi ni waliok serikalini sio vyama vya upinzani.

Kujenga shule wananchi wachangie ,kujenga vituo vya afya wananchi wachangie ,kujenga balabala wananchi wachangie ,kujenga soko wananchi wachangie ,kujenga vituo vya polisi wananchi wachangie ,hivi serikali iliyopo madarakani kazi yake ni kitu gani ?

Aloo huu si wakati wa kuturudisha katika siasa za kichina ,serikali mbali ya kodi inakusanya mapato kutoka nyanja mbalimbali ,yakiwemo kutoka kwenye madini ,misitu ,utalii ,vitalu vya kuwinda mbali ya pato la gesi ,hela yote inakwenda wapi ,huu msemo wa kusema wananchi wajitolee ni kuwafanya WaTz wote wapumbavu na wenye akili taahira ,isipokuwa wachche nyie mliozidiwa na akili.

Zanzibar ikiwa watafanikiwa kujipapatua na kuweza kufukua mafuta na kuchimba gesi basi uhakika wa kila raia kulipwa upo ,tena sio chini ya dola sitini kwa mwezi ,kwa maana ule msemo wa wananchi wanatakiwa wjitolee hautakiwi ,kwani Nchi haiendi vitani.

mkuu hongera... naona siku hizi siasa zako zimebadilika.... pamoja tutamshinda mkoloni mweusi ccm!
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Back
Top Bottom