Ronal Reagan
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,299
- 3,055
Kila la heri CHADEMA.
Ila ni muhimu sana mje na mkakati-kazi na sio kauli kali na nzito tu.
Ila ni muhimu sana mje na mkakati-kazi na sio kauli kali na nzito tu.
Kila la heri CHADEMA.
Ila ni muhimu sana mje na mkakati-kazi na sio kauli kali na nzito tu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesitisha operesheni yake ya M4C mkoani Iringa na kuitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu.
Kikao hicho cha Kamati kuu kitafanyika siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam chini ya viongozi wake wakuu Mkiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.
Mkuu wa operesheni M4C Benson Kigaila amesema haiwezekani kuendelea na operesheni huku polisi wakiua watu kwenye mikutano ya CDM kwa maelekezo maalum. Amesema Kamati kuu itatoa mwelekeo rasmi wa chama kuhusu hali hii ambayo haiwezi kuvumiliwa.
Pia inatarajiwa kamati kuu kujadili vitisho vya msajili wa vyama John Tendwa dhidi ya chama hicho,msajili ambaye watanzania wengi wanaamini ni kada mwaminifu wa chama tawala.
Source: Tanzania Daima/Majira.
Wasiwasi wangu ni wale waliopata ajira kutokana na hiyo mikutano! itabidi tuanzishe michango ili familia zao zisiwe omba omba!
Wamualike na huyo mwenye upara kama upande wa kalio.
Mkuu ADC kimepata usajili wa kudumu.
Si wote wavaao nguo za kaki ni cdm kuna policcm nao huvaa kaki!tunaongea kwa maslahi ya taifa hapa hakuna u-CDM wala u-CCM. Yaani watu waendelee kufa kisa kampeni.Stupid ideas
Natambua kuwa hapa si FB ule ni mtandao wa ullimwengu mzima si kama hapa JF kwa CDM. Lakini ukweli lazima tuwe tunausema. Tunajua wazi wewe ni mmoja wa wanaofaidi fedha za harambee wanazochangishwa walipa kodi wetu. Mnazitumia kupiga propaganda ambazo hazina maana yoyote, hebu jaribu kutembelea TANURU LA FIKRA kule FB ujionee hoja zinavyowasilishwa na kuchangiwa kwa uwazi. Kule FB SLAA, MBOWE na wngine wanachambuliwa kwa undani na na madudu yao kuwekwa hadaharani wakati huku JF ukimgusa SLAA unakula burn ya nguvu na naamini kwa mchango huu lazima leo nile burn , fuatilia baada ya dk 10 hutaniona tena nitakuwa nimeshakula kitanzi toka kwa MODs ambao nao wanakula za walipa kodi. Ukiona mtu anang'ang'ania humu JF ujue huyo anafanyia CDM, na mfano mzuri ni wewe ambaye hutaki kupanua uelewa wako na unabaki kunyoosha vidole juu kama unaimba taarabu.
Mimi napendekeza tuandamane dhidi ya huyu Msajili wa vyama vya siasa. Lakini maandamano yetu yawe ya ujumbe wa simu kwa siku 3 mfululizo, tukimtaka asimamie haki kwa vyama vyote. Ujumbe wetu usomeke "SOTE TUNA HAKI, KWANINI IWE YA CCM TU?". Kwa wingi wetu tukipeleka text msg kwa siku 3 mfululizo, kwanza tutaonyesha jinsi tunavyoguswa Watanzania kwa ujumla wetu, pili, tutazuia mawasiliano na yoyote kupitia namba zake za mkononi.
Tuwekewe namba zake zote za mkononi tuanze maandamano yetu. Nakumbuka hili lilifanyika kipindindi kilichopita baada ya kuanzishwa na Mwanakijiji na lilikuwa na mafanikio makubwa sana
Ni vyema wakatathmini mwendeno wa chama chao kwani kimeanza kujenga taswira mbaya kwa watanzania.
Waje na kitu ambacho kitawaonesha kuwa hatimaye wanaelewa uzito wa kile kinachowakabili. Maana tangu 2010 bado wanaonekana walikuwa wanaamini kuwa wanaweza kuishawishi serikali ya CCM to be nice to them...