CHADEMA yaleta AMANI MBEYA baada ya risasi na Mabomu kushindwa

Hili la mbeya ni ushindi mkubwa kwa peoples power. Kwamba jeshi, vifalu , polisi na mabomu yao hawawezi kuishinda nguvu ya umma. Mwisho wa siku wamerudi wenyewe mezani na kimdondokea sugu mbunge waliyekuwa wansmdharau ili atulize hasira za wananchi. Kwa hili ccm wameonyesha hawawezi kuongoza nchi hiina nawashauri waachie chadema chama chaguo la mungu washike nchi hii.
 
Hongereni Mbeya, hongera sugu. Hongera CCM hongera CDM. Siku zote naasisitiza BUSARA itumike.
 
Magwanda bana, zamu ya sugu sasa. Hivi nyie mnafikiri hizi siasa za sifa zitawafikisha kokote kweli? Mgoje zamu ya wenje. Tanzania kweli tumekwisha, yani leo hii kuna watu na akili zao wanamuona mr.2 aka 2 PLOUD aka sugu aka muheshimiwa aka mbilinyi aka supestar aka kamanda ndio mwanasiasa.
Omar...hebu niambie Mwanasiasa ni nani basi, kama sugu siye? Naomba msaada kwenye tuta please
 
Siasa maana yake ni kulipeleka jambo lolote sawasawa na hichi ndicho kilichofanyika Mbeya. Kilichokusudiwa ni vurugu kutulia na vurugu zimetulia sio muhimu nani amezituliza na vipi.

Kwa kawaida ya siasa ushindani unakua ktk uchaguzi na chama kinashinda kutokana na uwezo wa kuwakinaisha raia na sera zao na baada ya chama kushinda vyama vyote vilivyoshindwa vinatakiwa vishirikiane na chama kilichopo madarakani kwa mafanikio ya nchi. Hilo ndilo lililofanyika Mbeya. Nimemsifu sana sugu na zaidi nimewasifu wale waliofikiria kumuita sugu kwani hawa ndio walifanya kazi kubwa na walionyesha hasa quality ya leadership.

Inaleta moyo na inaonekana ni mwanzo mzuri wa baadhi ya watu kufahamu hasa nini maana ya upinzani wa kisiasa ingawaje hili halikanushi idea ya chama kingine kukosolewa kama kikionekana kua kina udhaifu ktk baadhi ya mambo.
 
kuna msemo katika biblia usemao hivi
mamlaka na watawala wote watoka kwa mungu
sasa kama mamlaka mmejichukulia kwa mabavu mtayaona
ARUSHA MBEYA NI MIFANO
MUNGU hasemi uongo mtayaona kwa macho na vitendo vyao waporaji
 
Hongera Mh. Mbilinyi kwa kusaidia kurudisha amani Mbeya!!! Mungu atakulipa kwa kazi hii nzuri!!!

Tiba
 
Hakika pumba zimeanza kuonekana naona kila mwenye umuhimu anaanza kuonekana aliyekuwa anakamatwa na kuwekwa ndani kwa amri ya viongozi na polisi , leo ndie anawaepusha viongozi na Polisi na Kolokoloni la Ocampo.Big UP Sugu polepole tunakaribia kuona watenda haki wanapata jukwaaa la kuonyesha ukweli wa maisha yetu na misingi ya haki inaimarishwa kwa faida ya vizazi na vizazi.
 
Mpelekeni na Arusha akalete amani.

Crap!!!, Crap!!!!, Crap!!!!!. Can you at least once in a week, use your head properly to think? What has Hon. Sugu to do with Arusha Constituency? Who told you that Hon. Lema is incapable of doing the same as Hon. Sugu did? Pole sana mkuu!
 
Watawala wajifunze wajifunze kupitia historia. Kwamba maguvu hayana nafasi tena ya kuleta amani popote
 
Sugu kweli rais wa mbeya,dola legelege imeshindwa kuwatuliza na kuwatendea haki watu na serikali yao legelege ya CCM! Shame on you magamba na serikali ya mkoloni mweusi CCM!
 
Watawala wajifunze wajifunze kupitia historia. Kwamba maguvu hayana nafasi tena ya kuleta amani popote

Wenye akili tulikwisha waonya watawala kwamba matumizi ya mabavu siyo endelevu yatashindwa,na kweli wananchi wa Mbeya wametoa somo zuri sana kwa watawala. Msiwalazimishe wananchi kufikia hatua ya kuanza kuchoma moto nyumba zenu na mali zenu. Na mkiendelea na ubishi na ubabe tutafika huko. Huu siyo unabii ama utabiri,ni historia pale wananchi wanapowachoka watawala wao.
 
Back
Top Bottom