CHADEMA yaleta AMANI MBEYA baada ya risasi na Mabomu kushindwa

Chintu

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
5,437
3,457
Imethibitika kwa mara nyingine tena ndani ya jiji la Mbeya kuwa kumbe Magamba na polisi ndo chanzo cha vurugu nchini. Baada ya risasi na mabomu kushindwa, Magamba wakagundua njia pekee ni kutumia mamlaka halali(CDM) kutuliza vurugu, wakamwita Sugu, wakampigia magoti, wakamlilia chondechonde!!, sura zetu hazitakiwi huko nje, ni wewe tu na yule Dr wenu wa ukweli ambao mkionekana wanambeya watatabasamu, watacheka na kushusha hasira zao na kurejesha amani.

Na kweli kamanda Sugu alipowasili, hasira za wanambeya zikapotea, vigeregere na shangwe vikarindima, kumbe wanambeya wanamjua kiongozi wao ni nani na MTAWALA wao ni nani. Kiongozi hutumia hoja zenye ushawishi na mtawala hutumia risasi na mabomu dhidi ya anaowatwala.
 
waendelee na ukandamizaji wa haki wakitegemea viongozi wa cdm watawatuliza watanganyika...
 
Ebwana umenigusa sana na analysis yako.

Nafikiri busara kama hizi zitumike kuzimisha kila vurugu zinapotokea kwa kuwashirikisha wapinzani na watu mashuhuri. Nchi hii ni yetu wote, hakuna udhaifu wowote utakaoonyeshwa na serikali kama wapinzani na watiu mashuhuri wengine (viongozi wa dini, wana muziki etc) watahusishwa kutuliza vurugu. Nakumbuka wakati fulani huko Temeke ukimsimamisha Sheikh Mtopea wa NCCR watu wote kimya wanamsuikiliza.Bravo uongozi wa Mbeya kwa kuliwaza na kulitenda hilo kama kweli ni wazo lenu original aui mmedandia baada ya SUGU kuanza kutuliza mambo!!!!
 
Katika kuiongoza nchi, CHADEMA wana uhalali wa watu {legitimacy of the people}, lakini ccm wanatawala kwa uhalali wa kisheria {legitimacy of the law}. Sasa imedhihilika wazi, katika uchaguzi wa mwaka jana chadema ilishinda na ndio maana inaongoza nchi nje ya ikulu. ccm haiwezi tena kuongoza nchi hii na hivi karibunii wananchi wataamua wakakizike wapi chama hiki, jangwani au baharini?, wao wataamua.
 
Zilikuwa ni vurugu za masaa 30 nonstop kuanzia Mbalizi - Mwanjelwa - Uyole,

Baada ya SUGU kuongea mji kimya amani tupu imetawala hadi asubuhi hii
 
Zilikuwa ni vurugu za masaa 30 nonstop kuanzia Mbalizi - Mwanjelwa - Uyole,
Baada ya SUGU kuongea mji kimya amani tupu imetawala hadi asubuhi hii
sijajua sambwe shitambala anaficha wapi sura yake. Huyu aliwasaliti wana mbalizi, na sasa MBILINYI anatwanga kotekote hadi mbalizi! Viva SUGU
 
Unajua alidhani mbeya ni kama dsm ambako wengi ni wahamiaji!
Watu wako kwao uku alafu unawatimua waende wapi
Labda yeye ndo arudi iringa kule kalenga walikomtosa kura za ubunge
 
Zilikuwa ni vurugu za masaa 30 nonstop kuanzia Mbalizi - Mwanjelwa - Uyole,

Baada ya SUGU kuongea mji kimya amani tupu imetawala hadi asubuhi hii

Hii nchi ni yetu wote, hivyo kazi aliyofanya Mh Sugu ni nzuri. Hili ni fundisho kwa Mzee Kandoro kuwa siyo lazima kila kitu utumie mabavu, mbona Mwanza mabavu yaameshindwa kutuliza watui hadi anahamishwa. Mimi naona kuwa katika haya majiji matatu (Mwanza, Mbeya, Arusha) kunahitajika kila mara busara kutumika badala ya nguvu za dola. Angalia hapa chini picha toka Mbeya wakati wa ujio wa Mh Sugu kwa mujibu wa Mbeya Yetu Blog!!! Moderator / Invicible nisaidieni kuzikuza hizi picha, tekinohama yangu wasiwasi huku Kibondo!!! Kuna mtu anaweza kunipa tuition ya jinsi ya ku upload na kukuza picha haja JF????

Umati Mbeya.JPG Sugu 1 Mbeya.JPG Umati Mbeya2.JPG Sugu 2 Mbeya.JPG
 
Kwakweli nilipoangalia ya Mbeya, natamani show ya Arusha irudiwe!
Ila nadhani tunairudia soon.
 
Inatoa fundisho kubwa sana kwa viongozi wetu wa chama tawala kuwa 'wao ni viongozi wa wananchi, na wako pale kutumikia wananchi na siyo vinginevyo'. Ni mhimu sana kuelekezana mambo mhimu kwa faida ya jamii nzima, siyo kutumia nguvu wakitarajia kwa vyeo walivyo navyo wananchi watakaa kimya milele huku wakiuguza maumivu yao hadi uzeeni.

Ninachoona mimi ni kuwa kufikia 2015, tutakuwa tunazungumzia taifa lenye watu wasio waoga tena karibu kila kona ya nchi. Watu watakuwa wako tayari kwa lolote lile, pamoja na kuwa vyombo vya habari haviitendei haki jamii ya mtanzania kwa kuwanyima haki yao ya msingi ya kupata habari, lakini watu wanapata hizi kupitia njia zingine tofauti.
 
Hii nchi ni yetu wote, hivyo kazi aliyofanya Mh Sugu ni nzuri. Hili ni fundisho kwa Mzee Kandoro kuwa siyo lazima kila kitu utumie mabavu, mbona Mwanza mabavu yaameshindwa kutuliza watui hadi anahamishwa. Mimi naona kuwa katika haya majiji matatu (Mwanza, Mbeya, Arusha) kunahitajika kila mara busara kutumika badala ya nguvu za dola. Angalia hapa chini picha toka Mbeya wakati wa ujio wa Mh Sugu kwa mujibu wa Mbeya Yetu Blog!!! Moderator / Invicible nisaidieni kuzikuza hizi picha, tekinohama yangu wasiwasi huku Kibondo!!! Kuna mtu anaweza kunipa tuition ya jinsi ya ku upload na kukuza picha haja JF????

View attachment 41178View attachment 41179View attachment 41180View attachment 41181

nimekusoma. Namashangaa Kandoro kuamua kutumia maguvu Mbeya wakati Mwanza akiwa na Sirro walitumia busara zaidi na mazungumzo yaliepusha vurugu za machinga na kabwe japokuwa kabwe hawezi kukatiza mtaani.

Kumbe yawezekana Sirro ndo alikuwa na busara zaidi kwani pia hata FFU/ASKARI walikuwa chini ya maelekezo yake. Kandoro hakupata msaada kutekeleza matakwa yake kupitia jeshi. Kama ni hivyo, Sirro Mungu akujalie zaidi.
 
Back
Top Bottom