CHADEMA yakamata ngome ya CCM Kyaka

CDM kimeshinda uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Burifani, Kata ya Kyaka, wilaya ya Misenyi, ambacho ni makazi ya Mbunge wa Nkenge, Asumpter Mshana. Mgombea wa CDM, Deogratias Laurian, alipata kura 401 dhidi ya kura 129 za Mathias Kibarwiga wa CCM. Placid Vedasto wa TLP alipata kura 2.

Habari zaidi soma Mwananchi la leo uk.9. HONGERA CHADEMA

idd amin, hii ilikuwepo jana
 
Toeni ujinga hapa kila ukisema kamji kamekakamaa useme kwenu wapi usikute we wa Singida alafu unachonga.
Hahahahaaa......
Mkuu, lakini issue hapa ni M4C
Zoa zoa imepamba moto.
Achaneni na mambo ya mji mdogo au mkubwa!
 
Wahaya bana majigambo mengi nlipofika bukoba sikuamini macho yangu kamji kamekakamaaaa,na usomi wao wa kinafki wengi ni wabinafsi .

Kejeli kama hizi hazitusaidii kujenga umoja na nchi yetu kwa ujumla. La msingi ni kujiuliza kwa nini miji mingi ikiwepo Bukoba na mingine mingi haikui kwa kasi? Ukweli ni kwamba suala la msingi zaidi kujiuliza ni kwa nini uchumi wa Tanzania umedumaa na kukakamaa baada ya miaka 50 ya uhuru huku kukiwa na maliasili nyingi sana? Jibu la swali kama hili ni chimbuko la umaskini wetu. Ni muhimu wanajamvi tuwe na vision ya kujenga.
 
Kudadadadeki.., yaani sasa hivi zaidi ya asilimia 70 ya chaguzi zote za vijijini nazosikia CCM wanaangukia pua. Kwa mwendo huu CCM ishamwagiwa Polium asee..
Mwendo mdundo :target:
 
Toeni ujinga hapa kila ukisema kamji kamekakamaa useme kwenu wapi usikute we wa Singida alafu unachonga.

Wengine wa tabora, tanga, rukwa, songea, lindi, mtwara alafu wanachonga! ukiwauliza kwenu wapi wanadanganya eti wamezaliwa dsm! hacheni upuuzi british kingdom au bk ni pazuri, au kwan lazima wote tuwe chadema?
 
Wahaya bana majigambo mengi nlipofika bukoba sikuamini macho yangu kamji kamekakamaaaa,na usomi wao wa kinafki wengi ni wabinafsi .

Hapo umenena!! Wahaya wana kitu wanaita "OLWANGO" okutendelana ndio maana wahaendelei kujenga mji wao. Majigambo mengi, hawabadiliki, nyie wahaya, tubadilike jamani. Okutendelana, olwango logo!!!!
 
2015 nanye nintaa owitu Muleba. Iwe Tibaijuka oyeandae ninkutela entule nogwa ahansi. Yoo ebyawe tibiliyo 2015
 
Toeni ujinga hapa kila ukisema kamji kamekakamaa useme kwenu wapi usikute we wa Singida alafu unachonga.

ta muganyizi, achana nao hao utakuta wengine wanatokea Sirorisimba, huko msm vijijini, ila huyu mbunge wa Nkenge anatakiwa atoke hana inshu.
 
Kila nisomapo namna CDM inavyojikita na kufanikiwa vijijini inanipa faraja kubwa sana. Mara nyingi ni habari njema pekee ktk siasa chafu za nchi hii.

Hongera CHADEMA. Hongera makamanda!
 
Hongera CDM kwa ushindi Watanzania tunawasubiri mtawale wakati wowote CCM wameshindwa wakabidhi nchi kwenu.

Natangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Nkenge kupitia CDM, wapenda maendeleo naombeni ushirikiano wenu.
 
Mkombozi wetu kashaija Butege ataeneza Sumu hiyo ya Ukombozi hadi nyumbani kwa kwa wale ambao bado wamelala usingizi kila kitu kinakwenda hatua kwa hatua ni kweli baadhi ya maeneo bado ya malala lakini wataamka tu kwa maana saa ya ukombozi ni huu.
 
Good to hear about that, naaminia wanamageuzi. DED alijaribu kubadilisha tarehe za uchaguzi lakini wapi... Ngoja magamba wapate fundisho... tunasubiri 2015 tupate Mbunge kutoka CDM.
 
Back
Top Bottom