Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 68
chadema wametia saini mkataba mbovu na kutuingiza hasara, Mbowe na Dr Slaa wajiuzulu damu mpya ya vijana ichukue nafasi
Yaani hata mimi siwaelewi, nilitegemea wangevuta subira ili kuona kama serikali itapeleka mapendekezo ya kurekebisha sheria hii katika bunge lijalo. Job true true
kuna mtu kawastua naona,jk si mnajua mtoto wa mjini angewaingiza choo cha stendi kama alivyomfanyia lowassa kwenye ile "ajali" yake ya kisiasa....!wao walikua wanafurahia kugombea vikombe vya chai ya ikulu juzi kumbe mwenzao alikua anawasanifu tu!
ooh boy!!
kwa makubaliano yale na jk ambayo yalisainiwa na mnyika na nchimbi hakuna hata moja lililosema kuwa rais asisaini muswada kabla ya marekebisho. Ila nakumbuka la kwanza lilikuwa linasema "pamoja na sheria hiyo kupitishwa na bunge ipo haja ya kuendelea kuiboresha ili ikidhi mahitaji ya kujenga kuaminiana na muafaka wa kitaifa". sina hakika kama mlilielewa hili. Yawezekana mlinogewa chai ya ikulu na kushindwa kulitafakari hili kabla ya kulisaini. Kwa maana hiyo kusema kwamba rais kawauza mmeniboa.
mnyika naona unaona maoni ya watu wengi hapo juu, hata kitaani ni hivyo hivyo
all i can say to you guys please sticky to your decision, chadema ijulikane ina mlengo gani, mlengo wa kulia, kushoto au kati, amueni kuwa radicals na dunia ijue hivyo...au muwe kondoo na dunia itawajua hivyo. Mmekuwa mnabadilika badilika sana.....
Hata iwe vipi hamtakuwa na uwezo wa kumfurahisha kila mtu.....ila amueni muwe vipi na mtavuta wengine kwa vile mtakavyokuwa!!
Leo mtakasirika, kesho mtamchekea yule yule aliyewakasirisha jana, kitu gani huwa kinatokea??...hatujui
lingine, jamani ikiwezekana hiyo ruzuku ichukue nafasi ya posho zenu za bungeni...susieni vikao vya bunge na dunia ijue hivyo ccm wanajua kuwa huwa mnatisha leo....mnakuja kesho! This aint good not neither for your supporters nor for your members.
Kwenye nyekundu hapo ndiyo pointi, mimi nilikuwa nasubiri sana nondo za CDM, ingawa ni CCM damu, ningependa sana kuona malumbano yao na wabunge wa CCM na CUF, but to my and I think most Tanzanians disappointment..........Wanatuzuga tu mbona hawasemi wwalichokubaliana na jinsi kutekeleza pia yale ambayo hawakukubaliana na sababu zake labda hili ndilo hawakukubaliana kwa sababu uwezo wa kuingiza marekebisho yao kwa sasa kwenye mswada ni vigumu na wataendelea kuyafanyia kazi taratibu kadri inapo faa
CHADEMA walikosea mapema bungeni kitendo cha kutoka nje ya bunge Mawazo yao wangeyawasilisha tuu hata kama ni kwa ukali kiasi gani Wananchi wangejua nini mawazo yao na wanajengaje hoja na kuitetea
Tatizo lao wanaharaka mno wanataka kile wanachotaka kifanyike hata kama hakiwezekani " Lazima kulikubali kosa na uwe tayari kutafuta means nyingine namna ya kulirekebisha " ILA KWA AMANI
Unakoelekea siko jaribu kurejea kwenye mada Nahisi kama unaelekeana na mawazo ya nursery school au ndiko uliko mkuuwewe hao sio wapwan,,ni watu wa kaskazin watu wa kaz na pesa
Mnyika kwani ulitaka mapendekezo yote lazima Jk ayakubali? kama yalikuwa sita unajuaje labda matano yalibaki kayakubali?
Jamani toka tulivyoona yale makubaliano na namna CDM walivyokuwa wanatoa maelezo tata kuufafanua while wenzao wa CCM wakiwa kimya tuliwaonya viongozi wetu waitishe kikao haraka cha kamati kuu kujadili reaction ya watu na makosa ya wazi ya makubaliano yale.tamko hili la cdm tulilitarajia lakini tayari ni too late! jk kashinda kirahisi sana,yale makubaliano na zile picha za tabasamu huku rais akiwagawia juice ni turufu kwa serikali na itatumia kuwaonesha taasisi za kimataifa na kuwaambia "hawa ni walalamishi,mbona tumewasikiliza na makubaliano ndio haya hapa na tulielewana vizuri tu kama mnavyoona kwenye picha!" hapa hatuchomoki kwa hizi bla bla na matamko! Wananchi wameshazoea,lazima turudi nyuma tujiulize kabla hatujaangukia pua kabisa! Kumbukeni pia hizi vurumai zinawapa fursa ccm kujipanga na uchaguzi 2015! Muda unakwisha hatujawaandaa wananchi vya kutosha kuelekea kwenye mabadiliko! Kibaya zaidi uchaguzi utafanyika ktk mazingira haya haya hata kama ni katiba mpya! Tunaelekea kushindwa kama hatuoni! Mawazo yangu tu jamani kama mzalendo!They never seem to have plan B before taking plan A.
Nakupa guarantee hawawezi kususa hadi mwisho wa huo mchakato.
Watakuja kubadili maneno tu baadae kuwa hatukuwaelewa kama madai yao ya kutomtambua rais