CHADEMA Yaisambaratisha CCM Kyela; ngome ya Mwakyembe yatikiswa

"CHADEMA Yaisambaratisha CCM Kyela; ngome ya Mwakyembe yatikiswa"

Hiki kichwa cha habari chasema mengi kuliko face value yake.
 
Mkuu,

Vipi zile habari zako fake za vikao vya NEC unaona hazitoshi na unaanza kuingilia na Kyela?

Sisi hatuhitaji kupiga simu kujua yanayotokea Kyela, tunayaona yakitendeka. Utashangaa sana mwaka huu na hao wapiganaji wako.

Mpigia simu huyo rafiki yako Mwakyembe na mwulize mbona anashindwa hata kusalimiana na majirani zake?

Vinginevyo ya Kyela niachie mimi engineer wa Majungu according to Masanilo (aka Ze Comedy_ niendelee kuwaletea za jikoni.

Hii inanilkumbusha mjinga mmoja pale kyela anaitwa Ima yeye kutwa ni kuongea na kumfuatilia dokta na kipikipiki chake wakati yeye majukumu yake ni zero kabisa. Sasa kama wewe huwezi kutekeleza majukumu yako hata kwa asilimia 49% unawezaje kweli kuanza kumsema mwenzio.

Kweli watu tumetofautiana sana
 
Du!! mawazo yangu MH. itabidi sasa urudi class maana tunakumiss sana huku kwani ukiwapigia goti watu hawana Elimu Mbaya sana Please come back
 
kuna wanakyela feki humu ambao wanajifanya mslahi yao ni kyela tu, hiyo ni dhambi mbaya! kwamba wanachokiona kwa Dr, ni kusahau jimbo na kuwa Mtaifa na kwao hili ni baya! HAWATUFAI

hivi unafikiri barabara itajengwa kwa kirahisi ndani ya miaka 4 wakati tuko kwenye mapambano................

Mheshimiwa Shukuru apange bajeti, Mhe. Mwakipesile atoe mazingira mazuri ya ketekelezeka....bado.

tuje kwenye source;tazama. lile la charles charles!!!!!!!!!!!
kama ndio washabiki wa kyela wanatumia source ambayo kila mtu anajua imecling na akina nani, na hao akina nani wanamsaada gani kwa taifa....basi hata akikosa ubunge next He will be right at, cause its seemz most of people are ignorance by choice, not by design as most pple be.

all in all, Dr ni kichwa, na amebadilisha mfumo wa kisiasa, majadiliano mpaka ushabiki.
within 4 years as MP, things have changed totaly. Na kwa wale wanaodhani watatudiscourage kwa kupitia humu ndani, ni ngumu, jamaa influence yake bado ni great per now, i don knw next!

bravo Dr
.

Mkuu, umefulia na points zako
 
hakuna ukweli huu wote umbea tu na hizi ni fitna za mwakalinga na nyie wake zake vimada aliowatuma humu JF kuleta majungu ya kyela njaaa tu hakuna kitu hapo
 
Kama chama cha Mwakyembe hakikubaliki nyumbani kwake na kumbuka yeye aliwapanga wapambe wake ili mambo yamwendee murua mwakani, hizo sio salamu tosha akae chonjo 2010?

na je kama chama cha makamu wa rais[aliyepo na aliyepita/omar juma]hakikubaliki nyumbani inakuwaje?[kwa kuwa majimbo yao yanaongozwa na wapinzani]
na je ikifikia siku wapinzani wanachukua jimbo analotoka rais wa nchi tutasemaje kuhusu rais?
 
Always ukiamini kazi ya Fisadi nawe ni Fisadi. Tokea lini Mtanzania likamwandika vizuri Mwakyembe? Hapo Umenowa Kommesha ya mafisadi acha kununua bidhaa au service zao
 
Always ukiamini kazi ya Fisadi nawe ni Fisadi. Tokea lini Mtanzania likamwandika vizuri Mwakyembe? Hapo Umenowa Kommesha ya mafisadi acha kununua bidhaa au service zao
.

Na magezeti ya yule fisadi nyangumi,aliyetajirika kwa kipindi cha miaka minane tu na kuifilisi NBC yetu,mbona yanampamba kila siku mwakyembe?
 
.

Na magezeti ya yule fisadi nyangumi,aliyetajirika kwa kipindi cha miaka minane tu na kuifilisi NBC yetu,mbona yanampamba kila siku mwakyembe?

Mwenzetu wewe wawapi?..............

kama unakifahanu kiswahili vile, ila sidhani kama Mtz.

mengi na azizi wapinawapi, hata mtoto anaejifunza uraia darasa la3 anajua tofauti zake..
 
Mimi nadhani wanakyela wameanzakukomaa kisiasa, hawachagui chama bali wanachagua mgombea anayewafaa tofauti na hapo ni kwamba chadema inakubalika kwa sasa wilayani kyela. Vyovyote vile Mwakyembe anabakia kuwa mtu muhimu kwa mustakabali wa taifa hili, legacy hiyo anaipata kwa kuwa mmoja wa wanaharakati waliohusika kuliondoa CHUKIZO LA UHARIBIFU MAHALI PATAKATIFU. Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni jamani, Mwakyembe bado ana nafasi yake nzuri tu ktk siasa za taifa hili.
 
huu ni unafiki tu.....Dk. mwakyembe siyo kihiyo kama akina makamba so hata ubunge ukiota mbawa bado milioni zinamsubiri pale school of law.
 
Ngome ya Siasa ya Mbunge wa Kyela (CCM) Dkt Harrison Mwakyembe imesambaratishwa vibaya na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya wapambe wake karibu wote kuangushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji!

Kuangushwa kwa wapambe wake ni dalili za wazi mbaya kwa Dkt Mwakyembe anayeonekana hodari wa kutumia vyombo vya habari kujiaminisha kuwa anapendwa.

Habari zilizopatikana kutoka Kyela zinaeleza kuwa mpambe wa Dkt Mwakyembe aliyekuwa amejitosa kuwania kitongoji cha Ikolo anakoishi mbunge huyo, ameangushwa na kitongoji hicho kwa sasa kipo chini ya CHADEMA.

Dkt Mwakyembe aliyekuwa amepanga wapambe wake waweze kutwaa vitongoji kadhaa ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya kushinda kwenye kinyang'anyiro mwakani lakini juhudi zimefikia tamati baada ya CHADEMA kuwazidi ujanja na kuibuka washindi kwenye vitongoji vya Kyela Mjini, Mikumi, Bondeni, Mpakani, Ndandalo, Mwaya, Ngyekye, Bwato B na Ipinda!

(Source: Tazama, tr 3-9/11/2009, uk. 1-2).

kama hii ilikuw ani startegy ya rafiki yangu Mwakalinga.....basi kachemsha big time..........siku zote kwenye siasa.....ushindi wa chama ni muhimu
 
Ngome ya Siasa ya Mbunge wa Kyela (CCM) Dkt Harrison Mwakyembe imesambaratishwa vibaya na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya wapambe wake karibu wote kuangushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji!

Kuangushwa kwa wapambe wake ni dalili za wazi mbaya kwa Dkt Mwakyembe anayeonekana hodari wa kutumia vyombo vya habari kujiaminisha kuwa anapendwa.

Habari zilizopatikana kutoka Kyela zinaeleza kuwa mpambe wa Dkt Mwakyembe aliyekuwa amejitosa kuwania kitongoji cha Ikolo anakoishi mbunge huyo, ameangushwa na kitongoji hicho kwa sasa kipo chini ya CHADEMA.

Dkt Mwakyembe aliyekuwa amepanga wapambe wake waweze kutwaa vitongoji kadhaa ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya kushinda kwenye kinyang'anyiro mwakani lakini juhudi zimefikia tamati baada ya CHADEMA kuwazidi ujanja na kuibuka washindi kwenye vitongoji vya Kyela Mjini, Mikumi, Bondeni, Mpakani, Ndandalo, Mwaya, Ngyekye, Bwato B na Ipinda!

(Source: Tazama, tr 3-9/11/2009, uk. 1-2).

Hao wapambe hawana majina? Uthibitisho gani kuwa hawa ni wapambe wa Mwakyembe na wala sio vinginevyo?
 
Kumbe school of law kuna mamillioni?? au kujifariji manake mtu hakiwa mbunge anavuta zaidi kuliko kula chaki bana.

Habari ni ya kishabiki zaidi manake kama ushindi ni 95% sasa kusambaratishwa kunatoka wapi kama sio kupakana matope. Na wote walio shinda wametoka CCM mwezi kabla ya uchaguzi lini wamepata itikadi za Chadema kama sio kuchezeana shere na kuonyesha kuna upinzani kumbe zuga tu.

Kali kuliko zote mganga alikuwa mwenyekiti anayeshikilia madaraka alitema uenyekiti wa kitongoji na kumwachia mshkaji wake ili agombee uenyekiti wa kijiji sasa kustuka Kyela imekuwa mamlaka ya mji mdogo na hakuna mwenyekiti wa kijiji ndio jamaa akakimbilia Chadema na kushinda manake mshkaji hauziki na ni mwandishi wa habari.

Sasa uadilifu wa viongozi wa namna hii huko wapi kama sio kupotezeana muda na wizi mtupu na kupakana matope upinzani unajimaliza wenyewe kwa kulundika makapi ya CCM na waroho wa madalaka.
 
Yale Yale....siasa za Kyela kwlei ngumu wajameni. Hivi hizi nguvu za kisiasa zipo ki hivyo au zinapewa uzito usiostahili na vyombo vyetu vya habari?

nadhani kulikuwa na proposal pia kuwa na kasub forum ka wanaKyela ili waweze kukata issue vizuri.
 
He he heeeee ....... Minyakyusa bwana!!!!! Heri sisi wa Sikonge tuna Mbunge aliyekaa kama Hitler vile. Halafu JF tupo wanne tu........
 
Buchanan,

Hii habari mbona niliileta siku ile ile ya uchaguzi?

Kilichofanyika ni kwamba mheshimiwa aliweka wapambe wake ili wachukue baadhi ya vitongoji na akafanya kampeni ya wiki nzima.

Kambi ya Mwakalinga (sina uhakika kama Mwakalinga aliidhinisha strategy hii) ilipoona hilo ikaweka mkakati wa kuwatungua hao wapambe wote wa Mwakyembe. Baadhi ya wanachama wa CCM wakaamua kugombea kupitia CHADEMA na hilo kundi likawaunga mkono.

Wao wanasema lengo lilikuwa kumpa kipigo mbunge na pia kuwatisha madiwani wachache ambao bado wanamuunga mkono Mwakyembe kwamba wajiandae kupoteza nafasi zao kama wataendelea kumshabikia huyo msanii.

Kweli strategy imefanya kazi sana maana hata kitongoji anakotoka Mwakyembe (Ikolo) nacho kikatekwa.

Pigo kubwa lilikuwa mjini ambako Kilumbu, ambaye ndiye mfuasi mkubwa wa Mwakyembe aliangushwa na mzee mmoja mganga wa kienyeji.

Ukiwa karibu na mwakyembe hapa Kyela kwasasa jua kitumbua chako kisiasa kiko hataraini.

Mimi naona alifanya makosa makubwa sana kuweka wapambe wake maana hii imeonyesha watu wengi kwamba Dr ni weak na hata waliokuwa wanamuunga mkono, taratibu wanaanza kutafuta namba za Mwakalialinga ili wamsalimie.

Hizo ndio siasa za Kyela. Ila Mwakalinga aangalia maana hao CHADEMA wasije wakapata nguvu na kuamua kuitumia dhidi yake. Pia mwenyekiti wa CCM wa wilaya ambaye ndio pekee katika uongozi wa chama bado yuko na Mwakyembe, ameshaanza kusema Mwakalinga anawasaidia CHADEMA. Lakini wapambe wa Mwakalinga wanatamba kwamba hawaogopi hilo maana kwenye vikao vya CCM wakiamua nani ni hatari kwa CCM, kati ya hawa watu wawili, itaonekana ni bora kuwa na Mwakalinga kuliko Mwakyembe.

Jambo lingine la kushangaza ni kwamba CHADEMA Kyela walikuwa karibu sana na Mwakyembe na ghafla wamebadilika sana na wanaongoza kumuita msanii.

CCM bado wameshinda Kyela kwa asilimia zaidi ya 95.[/QUOTE
Mzee Mwakalinga kaifanyia nini kyela? wenzio wakili kushindwa kwa mwakalinga na wameanza kumuandaa mama mmoja kutoka ukoo wa mkuu wa majeshi tanzania. Ninaimani naye pia bado ataangushwa chali. MWAKALINGA ameishachuja hana lolote alilofanya kwa kyela. Kwani alikuwa wapi? HIvi amewahi hata kuwa balozi wa nyumba kumi? Mwakalinga hana chake Kyela. Bado mwakyembe ni kigogo wa siasa Tanzania.
 
Ngome ya Siasa ya Mbunge wa Kyela (CCM) Dkt Harrison Mwakyembe imesambaratishwa vibaya na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya wapambe wake karibu wote kuangushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji!

Kuangushwa kwa wapambe wake ni dalili za wazi mbaya kwa Dkt Mwakyembe anayeonekana hodari wa kutumia vyombo vya habari kujiaminisha kuwa anapendwa.

Habari zilizopatikana kutoka Kyela zinaeleza kuwa mpambe wa Dkt Mwakyembe aliyekuwa amejitosa kuwania kitongoji cha Ikolo anakoishi mbunge huyo, ameangushwa na kitongoji hicho kwa sasa kipo chini ya CHADEMA.

Dkt Mwakyembe aliyekuwa amepanga wapambe wake waweze kutwaa vitongoji kadhaa ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya kushinda kwenye kinyang'anyiro mwakani lakini juhudi zimefikia tamati baada ya CHADEMA kuwazidi ujanja na kuibuka washindi kwenye vitongoji vya Kyela Mjini, Mikumi, Bondeni, Mpakani, Ndandalo, Mwaya, Ngyekye, Bwato B na Ipinda!

(Source: Tazama, tr 3-9/11/2009, uk. 1-2).
Hapa ni uzushi mtupu kwani kyela kuna vitongoji vingapi? na CCM imesambaratishwa kivipi? Unamaanisha chadema wameikamata Kyela?.Tupe jumla ya vitongoji vilivyochukuliwa na CCM na vile vilivyochukuliwa na chadema. KUshindwa kwa mpambe wa Mwakyembe katika kitongoji ndio kushindwa kwa Mwakyembe?. Hapa ni kujifariji tu. Umejaa uzushi mtupu.
 
Mzee Mwakalinga kaifanyia nini kyela? wenzio wakili kushindwa kwa mwakalinga na wameanza kumuandaa mama mmoja kutoka ukoo wa mkuu wa majeshi tanzania. Ninaimani naye pia bado ataangushwa chali. MWAKALINGA ameishachuja hana lolote alilofanya kwa kyela. Kwani alikuwa wapi? HIvi amewahi hata kuwa balozi wa nyumba kumi? Mwakalinga hana chake Kyela. Bado mwakyembe ni kigogo wa siasa Tanzania.

Kuna watu wana akili duniani!!! Wee Wacha tu.
 
Back
Top Bottom