Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Ngome ya Siasa ya Mbunge wa Kyela (CCM) Dkt Harrison Mwakyembe imesambaratishwa vibaya na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya wapambe wake karibu wote kuangushwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na vitongoji!
Kuangushwa kwa wapambe wake ni dalili za wazi mbaya kwa Dkt Mwakyembe anayeonekana hodari wa kutumia vyombo vya habari kujiaminisha kuwa anapendwa.
Habari zilizopatikana kutoka Kyela zinaeleza kuwa mpambe wa Dkt Mwakyembe aliyekuwa amejitosa kuwania kitongoji cha Ikolo anakoishi mbunge huyo, ameangushwa na kitongoji hicho kwa sasa kipo chini ya CHADEMA.
Dkt Mwakyembe aliyekuwa amepanga wapambe wake waweze kutwaa vitongoji kadhaa ili aweze kujiwekea mazingira mazuri ya kushinda kwenye kinyang'anyiro mwakani lakini juhudi zimefikia tamati baada ya CHADEMA kuwazidi ujanja na kuibuka washindi kwenye vitongoji vya Kyela Mjini, Mikumi, Bondeni, Mpakani, Ndandalo, Mwaya, Ngyekye, Bwato B na Ipinda!
(Source: Tazama, tr 3-9/11/2009, uk. 1-2).