Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,678
- 4,350
dah mungu mkubwa. wezi tumewapiga chini
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.
Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.
CDM imeshinda kwa zaidi ya kura 6000
MATOKEO SEMI-OFFICIAL:
CHADEMA 32,543
CCM 26,452
My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015!
Kutoka kwa Zitto (FB)
Sizitaki mbichi hizi.Huu ni ushindi mkubwa sana kwa CCM.
Kuwawacha mfurahi ili "stability" iwepo ndani ya nchi, na hakuna atakaefungua mdomo baada ya leo kusema hakuna demokrasia.
Asa sioi itakuwaje maana familia inamtegemea? aligombea ili alishe familia
Wakuu, mpaka sasa tumebakiza kukusanya matokeo ya vituo vinne tu, narudi vituo si kata, vituo vya kupigia kura katika kata nne tofauti. Matokeo mpaka sasa yanasomeka hivi;
CHADEMA 32, 535
CCM 26, 296
AFP 131
DP 72
NRA 32
SAU 22
TLP 16
UPDP 22
Tumeanza na Mungu tunamaliza na Mungu