CHADEMA yaibwaga CCM Arumeru Mashariki; CCM Yakubali kushindwa (Zaidi ya kura 6,000)

jamani haya yanayosemwa ni kweli.,!?
kuna yeyote mwenye kujua idadi ya matokeo ya jumla toka kata zote 17.
 
2 + 2 jawabu lake ni 4 haijalishi anayetangaza ni Mchina, Mjerumani au Mndengereko. Kinachogombana sasahivi ni jumla ya mwisho tu... lakini HAWATOTANGAZA CCM IMESHINDA. Mnawapa sana credit na hii ni hatari kweli.
nimekuelewa mkuu, im not an easy believer thats why!!! afu moyo wangu ni delicate, especially nikijua nashinda afu isiwe hivyo!!
 
jamani mbona nyie wazushi sana, aya matokeo ya AKHERI haya hapa, tuambie chadema inaongozaje
[h=6]Matokeo ya kata ya akheri.
Nkoanrua1 cdm 192 ccm 60
Nkoanrua 2 cdm 166 ccm 56
Ushirika akheri 1 cdm 70 ccm 115
Ushirika akheri 2 cdm 46 ccm 250
... ushirika akheri 3 cdm 33 ccm 268
kimundo cdm 63 ccm 181
kimundo 2 cdm 61 ccm 150[/h]

Let's grant you your own results! Sasa tuambie, magamba mtashinda kwa hayo matokeo yako?
 
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.

Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.

My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015:
Hongera sana jamii forum kwa kutuletea matokeo. Pia hongera CDM kwa ushindi!
 
Mwanakijiji mbona leo Mods hawaweki record ya idadi ya watu walioko online inakuwaje?Hatufiki member wote wenye registration ya kudumu kweli?
 
Kama matokeo yakiendelea kuwa CDM ni majority, basi CCm walikosea sana kumweka Siyoi Solomon Sumari kuwa mgombea wao.

Jaji Damiani Lubuva amesema wamepewa computer 8 zisaidie kukusanya matokeo na sio kuchakachua.
 
Mbona Kagenzi kupitia ITV anasema wamepata matokeo ya kata saba pekee!

Kagenzi alisema ndani yalikuwapo matokeo ya kata 7 na nje magari matatu yalikuwa yameshaingia, hii ni kusema wakati ule, zaidi ya saa moja ndani ya viwanja vya halmashauri walaikuwa wana matokeo ya kata 10. Kwa kawaida, kila chama kina mawakala katika vituo vyote, na chama makini kina contact za mawakala wake wote katika kata zote. Ina maana mara baada ya kubandikwa matokeo katika vituo vyote, inachukua dakika 30 hadi saa moja kukusanya matokeo katika vituo vyote na kata zote 17. Kwa maana hiyo basi, kwa sasa vyombo vya Usalama na viongozi wa vyama vyote wanayo matokeo halisi ya kata zote na kama tofauti inaweza kuwa ndogo sana kutokana labda na ujumlishaji.
 
Wadau, mtakumbuka ktk thread yangu ya awali hapa jamvini! Nilisema toka kuwa ..."ukeshaanza kuona chama tawala kinashindwa na chama pinzani na hasa ktk ngazi ya kijiji, kata au vitongoji...ni ishara mpya ya kufa na kufutwa kwa udhalimu na chama kuondolewa madarakani!", Chadema imeshashinda ktk Udiwani Songea, na narudia kauli yangu ya awali kuwa "Taifa linakombolewa", watawala wanaanza kufutika ktk historia, CCM itakuwa kama chama alichokuwa anaongoza Chiluba cha MMD ambacho kimefilisika kisiasa hadi kifedha na hata kushindwa kulipa ada za uwepo wake hadi kimefutwa!

HONGERA TENA CHADEMA, CCM walishaiona laana yao ktk jimbo la Arusha, na wasilogwe wacheze mchezo wao wa maji-taka ktk jimbo la Arumeru Mash....wataona kilichomnyoa kenge magamba, kama wao yamewakwama!
 
wakuu je matokeo yatatangazwa saa ngapi?
Kuna matokeo yanangojwa toka pembeni ingawa nahisi wanataka kuyachakachua ila wanachi wako makini sana na hakuna kulala kama walivyokubaliana....hadi Nasari atangazwe
 
Back
Top Bottom