CHADEMA yaibwaga CCM Arumeru Mashariki; CCM Yakubali kushindwa (Zaidi ya kura 6,000)

Bora. Bado urais, kwani uchaguzi lini? Tufanye mpange ufanyike kabla ya 2015
 
Eeh mwenyezi mungu baba wa mbingu mwenye nguvu na mamlaka ya kila ulichokiumba tunakuomba uongoze mioyo ya wahusika wote wa tume ya taifa watangaze matokeo yaliyosahihi kwa haki na usawa.
 
Mtandao wa JamiiForums waweza kutangaza kwa uhakika kabisa kutokana na vyanzo makao makuu ya Jimbo huko Arumeru Mashariki kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo ambapo mgombea wake Bw. Joshua Nassari ameibuka kidedea baada ya kumbwaga vibaya mgombea wa CCM Bw. Siyoi Sumari. Matokeo yanaonesha hadi hivi sasa baada ya zaidi ya asilimia 80 ya vituo vyote kuripoti CDM imeshinda kata 14 dhidi ya 3 za CCM.

Chama cha Mapinduzi tayari kimekuballi kushindwa na kutoa pongezi kwa mgombea wa CDM.

My Take:
Bila ya shaka Uongozi wa taifa wa CDM hauna sababu ya kujiuzulu kwa wakati huu! Upepo umevuma upande wao na mtumbwi unaelekea kwenye ushindi 2015:

Sasa ni muda wa kuhamishia mbinu za Arumeru Mashariki sehemu nyingine nchini kwetu. Hakuna kulala hadi kieleweke. Mungu ibariki na uilinde nchi yetu Tanzania!
 
CDM fujo zenu zitawaponzwa mmediriki kulipiga mawe gari la polisi, mwataka mlindwe na nani?
 
Najaribu kuwaza hawa wazee wa magamba waloenda arumeru kumpigia debe SIOI, sijui watajificha wapi na sura zao zilizoshupaaa.........................

Mkapa,wasira,lowasa,medeye,mukama,lusinde,ole sendeka,mwigulu,nape wote ngozi zinawabana........
 
CDM kushinda Arumeru Mashariki ilikuwa wazi tu wananchi wa Kaskazini wameamka huwezi kuinganisha na Igunga ambapo Chama Cha Kijani kilishinda.Demokrasia ya Tanzania ni ngumu HONGERENI CDM.:high5::smile-big:
 
it is not over until it's over .... some people somewhere can always turn the tables in their favour
 
jamani mbona nyie wazushi sana, aya matokeo ya AKHERI haya hapa, tuambie chadema inaongozaje
[h=6]Matokeo ya kata ya akheri.
Nkoanrua1 cdm 192 ccm 60
Nkoanrua 2 cdm 166 ccm 56
Ushirika akheri 1 cdm 70 ccm 115
Ushirika akheri 2 cdm 46 ccm 250
... ushirika akheri 3 cdm 33 ccm 268
kimundo cdm 63 ccm 181
kimundo 2 cdm 61 ccm 150[/h]

tatizo huelewi maana ya kata na vituo..vituo vipo 327..kata zipo 17
 
Waiterrrr funga baa. Sogeza meza zote hapa. Lete wahudumu wenzio, supervisor na jamaa wa chips.

Njoo haraka na castle.
Mimi nipe Serengeti baridi kupata zoote, na ntaanza kulipa Mimi ktk raundi hii
 
Back
Top Bottom