CHADEMA yabakiza karata moja ya kucheza na mabadiliko kupatikana

mmemkwa

Member
Nov 9, 2011
54
11
Imeonekana Zitto Kabwe kuwa brain nyuma ya chama hiki kikubwa cha siasa ambacho ndicho kinacho unda upinzani halali katika nchi ya Tanzania. Hii ikitanabaisha ni tofauti na chama cha CUF ambao wao wamefunga ndoa ya kudumu na CCM ili hali katika utashi wa kuvukia barabara wanaitwa CCM B kadhalika na CCM C ambao ni NCCR- Mageuzi.

Katika matukio yanayoendelea kukikumba chama hasa kwa migomo na maandamano yasiyo na mantiki katika utashi wa kizawa na kizalendo katika Tanzania ndugu Zitto Zuberi Kabwe anaonekana kuwa ni ubongo ndani ya chama hicho kwa kuwa kutokuwepo kwake kuna ashiria madudu kutendeka.

Zitto ambaye ni mgonjwa kwa siku kadhaa sasa hali si hali tena kwenye chama chake, Mwenyekiti akana kushiriki kwenye maandamano ya Arusha na kusema hakuwepo uwanjani huu ni USALITI mkubwa kwa vijana wa Arusha na kingine ni kitendo cha Dr Slaa kujificha kwenye gari wakati polisi wakija kuwakamata maana yake haamini anachodai huu tena ni wehu, ili hali sintofahamu zinazidi kuendelea chamani humo Mkoa wa Dar es Salaam kuitisha maandamano ambayo hata wehu wameshindwa kuhuzuria huu ni uthibtisho dhahiri kuwa jamii ya wenye akili timamu na wasomi wetu Wamechoshwa na maandamano yanayo hujumu maendeleo na mustakbali wa taifa.

Zitto kabwe ambaye ndio anaonekana kuwa na ushawishi mkubwa huenda yeye tu ndio atakaye weza kuzua hali inayoelekea kukifanya chadema kama chama cha Arusha mjini na Karatu ikiwa ni sawa na UDP ya ndugu cheyo.

Chadema imebakiwa na Karata moja ya kucheza nayo ni zito kabwe tu, zaidi ya hapo anguko tayari.
 
Hii nchi ina vilaza wengi sijawahi ona...huyu naye ni kilaza wa karne
 
Duu eti huyu nae anaishii?

unajua kuna watu wanaishi kwa sababu kuwaua ni kosa la jianai na ni dhambi kwa waamini!
 
Mapendekezo yangu chuo kilichompatia Willbroad slaa udokta kimnyanganye kwani ana dhalilisha hadhi ya hicho chuo nawasilisha
 
ZITO HEZI KUA ZAIDI YA CHADEMA ,Leonel mesi hawezi kua ndio kila kitu baselona,hakuna mtu awaye yeyote kua ndio kilakitu kwenye chama makini kama CHADEMA,hilo ni wazo lako binafsi ndugu au kwa maana nyingine ni kua hilo linawezekana kwa watu wenye mtazamo hasi kwa jamii kama ilivyo kwa sisiemu,alakini kwa Chadema usitegemee upumbavu kama huo kwani watanzania wameamua mabadiliko hivyo wanajuaa ukweli ni upi na mnafiki ni nani na mwenye dhamira ya kweli ni nani.hivyo nia mbaya zote kwa umma wa wapenda mabadiliko hautaweza kwani MUNGU yupo upande wenye nia njema.shame on u magamba
 
"watoto wa mafisadi mnajitahidi kweli kupotosha dhima ya harakati za ukombozi tunaoutafuta. Mtake msitake ukombozi utapatikana tu! Hahahahaaaaaa! Imekula kwenu na hao babazenu wa kufikia mafisadi mabasha wa mama zenu."
 
Kwani uongo jamani mwe si kweeeli je mmeandamana Dar??? Je Mbowe alisema alikuwepo NMC??? Je polisi walimkuta wapi slaaa??????
Wote hao walionekana uwanjani hapo. Mboye kwa madai yake alikuwa ametoka kidogo kushughulikia maswala ya chama. Naomba ulete hoja yenye kujenga nchi sio hoja yenye dharau.
Swala la nzito nalo si hoja. Zito ni mtu aliyeandaliwa na CDM na ni kada mwaminifu sana kwa cdm. Kama akiamua kundoka ni haki yake kama ambavyo tumeona makada wa ccm walivyoondoka na kuiponda. Pia ujue kwamba siasa ndivyo ilivyo.
 
Weweee!
Udokta wa Slaa haunyang'anyiki maana ni wa kitaaluma si wa kupewa kama huyo ****** wenu; usikurupukie mambo!
 
Mmemkwa umefanya utafiti wa hayo mambo au unasukumwa na hisia zako kuyatamka?
 
Jaribu jingine hili la kumfanya Zitto kuwa juu ya chama umepotea. CDM sio sawa na CCM. CCM kilidai mwaka jana kuwa JK ni mtaji wao, yaani kiwao wao JK yuko juu ya chama. Kwa CDM sivyo, ataondoka Mbowe, ataondoka Zitto chama kitabaki imara. It is too late kusambaratisha CDM
 
Njia ya mafanikio huwa ngumu sikuzote, na hili ni gumu kueleweka kwa mwana-CCM wa kawaida (mwenye akili za kushikiwa) kama wewe.

Zitto angeshiriki vipi maandamano akiwa India?

Slaa kukimbilia garini ni kusalimisha uhai wake, ambao nyinyi mmeufanya 'kipusa'.
Ili uelewe, chunguza viumbe vyote utabaini vina namna asilia ya kujihami.

Mbowe kukana kuwepo NMC (kama ni kweli) ni changamoto kwa jeshi la CCM (polisi) ambalo nyinyi mmeligeuza adui wa UMMA; na msishangae maana hiyo ndio namna ya kumchukulia adui.
Usiongozwe na hisia kuliko sababu!
 
Back
Top Bottom