Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme

Sawa mkuu andamaneni kwakuwa:-
1. Shillingi imeshuka dhamani
2. Nyumba za kupanga bei zimepanda
3. Maji hakuna huku kimara, etc
4. Foleni zimezidi barabara

Lini tutafanya kazi maana naona mtaandama kwa kila kero katika nchi hii...
nchi kero ni nyingi umeme ni "cha mtoto"
 
CHADEMA waache cheap popularity na sympathy za kitoto! kabla umeme hauja tangazwa kupanda...EWURA waliendesha Tashtiti nchi nzima kwa wadau kutakiwa kutoa comments zao juu ya ombi la ongezeko la asilimia 34 liliombwa na TANESCO. Sikuona kiongozi yoyote wa CHADEMA pale Karim Jee Hall kupinga ongezeko hilo, Tashtiti kama hili pia ilifanyika mikoani na CHADEMA wakaa kimya. Leo hii wanaongea utumbo gani.!?

Hivi vitisho vya maandamano ni siasa zilizopitwa na wakati na ni za kitoto zaidi..CHADEMA mnatakiwa mkue kiitikadi sio mnalila lia tu na mkipewa nafasi ya kujitetea hamtokeo.

Huwezi kuzuia bei kupanda kwa maandamano bana!

Njia mbadala ni "kuondoa CCM" madarakani

Uchaguzi 2015

Wewe unsema nini mkuu?? Hujasikia watu waandamana kwa ajili ya kupanda kwa bei ya mkate?? Sasa wewe hujui kupanda kwa umeme kutaadhiri vipi maisha yako?? Au unafikiria tu bill yako ya mwezi??

Kwa taarifa yako kupanda kwa gharama za umeme zitaongeza gharama za uzalishaji viwandani hivyo kuadhiri gharama za bidhaa mtaani. Sasa siyo CDM wanaotafuta cheap popularuty hapa bali ni nyinyi ndiyo mnatafuta cheap popularity kwa kuonekana kuwa mnajibu hoja za Dr. Slaa hapa JF bila kutumia akili.
 
Wee kweli wa kuja.

Unataka CHADEMA wasubiri hadi mwaka 2015?

Kama baba angelikuwa kasubiri kwa njia zako, si ajabu leo hii ungelikuwa hujazaliwa.

Kwenye Ngumi huwa kuna kupiga mbavu kwanza na mtu akisikia maumivu ya INI basi anaachia mikono juu na hapo hata boxer mbovu anajua kuwa nina sekunde kadhaa uso ni wangu. Sasa weee Chadema wamepewa USO na uliokaa kama Punching Bag na wewe unasema "subirini kwanza CCM apate pumzi ndiyo muanze kummaliza........" Sijui akili zako kama kweli zinafahamu USHINDANI.

Dunia nzima huwa inatumika sana na ndiyo maana watu huwa wanasemwa kuwa "wanaogopa maamuzi makali" kwa sababu yatawamaumiza sana wananchi. Ila kama angelikuja Rais mpya leo na kusema "TUFUNGE MIKANDA" na tukaona hata wao wanafunga, watu watawaelewa. Ila wao wanapoongeza BEI huku wanazidi kujinunulia mashangingi na safari za nje haziishi, dawa yao ni MGOMO na MAANDAMAMO.

Ile walk out ya Bungeni ilishaanza kufanya kazi yake. Migomo ya UDOM na wanafunzi kwa ujumla nayo itazidi kulainisha mambo. Wakija kugoma Wafanyakazi hapo mtu atakuwa na hali mbaya zaidi. HAKI haijileti yenyewe ila HUPIGANIWA.

Warusi walitumia njia mbaya zaidi kwa kukiangamiza KIZAZI cha Sarah chote. Wale jamaa Wekundu walikuwa MAKATILI sana. Sidhani kama tutafika huko. Ninaombea tusifike na njia za kawaida za Maandamano na Migomo zitamuondoa SULTANI au walau kumfanya kuwa RAIA WA KAWAIDA na si mungu mtu.

Maelezo mengi ya kibiblia mimi si msomaji wa biblia!

Mtaandamana kwa kila kero mkuu?

Kero zenyewe lukuki, maandamano yenyewe kero pia!

Mambo ya kitaalamu mnaendekeza siasa...mimi wakuja wewe wakwenda!
 
Kama utaalamu TUNAKUZIDI, na tena utaalamu wa Uhandisi.

Kama ni Uchumi tunakuzidi. Kama ni sheria tunakuzidi. kama ni Uchumi pia tunakuzidi.

Sisi tunasema MAANDAMANO ni lazima. Haya leta kingine sisi tukibiruebirue pia.
Sivyo unavyofikiri..

Kuandamana ni siasa zaidi

mambo ya Tanesco ni Utaalamu zaidi, napendelea watu waheshimu wataalamu kuliko wanasiasa kama Slaa "ambao wamekasirika from day one to the end"
 
CHADEMA waache cheap popularity na sympathy za kitoto! kabla umeme hauja tangazwa kupanda...EWURA waliendesha Tashtiti nchi nzima kwa wadau kutakiwa kutoa comments zao juu ya ombi la ongezeko la asilimia 34 liliombwa na TANESCO. Sikuona kiongozi yoyote wa CHADEMA pale Karim Jee Hall kupinga ongezeko hilo, Tashtiti kama hili pia ilifanyika mikoani na CHADEMA wakaa kimya. Leo hii wanaongea utumbo gani.!?

Hivi vitisho vya maandamano ni siasa zilizopitwa na wakati na ni za kitoto zaidi..CHADEMA mnatakiwa mkue kiitikadi sio mnalila lia tu na mkipewa nafasi ya kujitetea hamtokeo.

mkuu sijui unaongea nini,yan unataka Dr.SLAA au Zitto aende kuhudhuria mdahalo uchwara wa kukaa karimjehe kujenga hoja badala ya kwenda kwenye mitambo,vyanzo vya nishati kama mtera,kiwira wewe unasema waende ukumbini kupanga bei? Unataka kusema kuna Watanzania kutoka mwanza,kagera ,kigoma walikuja pale karimjehe kudebate bei?kwanza bei inakuwa bidded upon?umeme unauzwa kwa mnada ili watakaosuggest ndo wameshinda? U can't be in your senses,there is something ridiculous in your brain! Ni theory zipi za uchumi za pricing zinazosugget round table pricing? Badala ya kuendesha research na kufanya economic pricing,wanamtuma mkurugenzi karimjehe akaulize bei iwe ipi?wakurugenzi ndo planners au researchers? Yani unategemea watanzania takriban mil.10 watumia umeme waende karimjehe kila mtu na bei yake? Dr.SLAA anasema upuuzi huu hatuutaki,sauti ya Dr.wa Ukweli si sauti yake pekee,ni muunganiko wa vilio vyetu sie maskini. Sala zetu ndo zinamfanya Dr.slaa awe msemaji wetu tena mwenye afya tele wala yeye si mnywa maji pia si muangukaji kwenye majukwaa,anakuja na problem akiwa full informed with facts. Haitaji 'kwa msaada wa watu wa Marekani'. Waccm walimsema sana eti kawataja first eleven kisiasa,leo Weakleaks inaanza kufunua maneno ya dr.slaa, pia inaonekana wazi Radar scandal unaona,na sasa wahuni wanaitaka kila shilingi ya mtanzania,hawa watu si wa kupuuzia. Hapa ata angetamka shetani kuwa bei ya umeme haiko sahihi ,simtaki shetani ila kwa ili ningeandamana nae. Waache waliojitoa kutetea umma na wautetee. Mh.Dr. Slaa hata ukitaka wa kubebea mkoba wakati wa maandamo mi nko tayari. Wakati umefika kuikomboa Tz kutoka kwa mkoloni mweusi!
 
Kama hiyo juu unaita Biblia, sijui hata KATIBA ya Nchi umeshasoma.

Sasa kama mtu hata huwa husomi, utaingiaje humu kujadili? Unasubiri ulishwe matapishi ya CCN na TBC?
Maelezo mengi ya kibiblia mimi si msomaji wa biblia!

Mtaandamana kwa kila kero mkuu?

Kero zenyewe lukuki, maandamano yenyewe kero pia!

Mambo ya kitaalamu mnaendekeza siasa...mimi wakuja wewe wakwenda!
 
Kama hiyo juu unaita Biblia, sijui hata KATIBA ya Nchi umeshasoma.

Sasa kama mtu hata huwa husomi, utaingiaje humu kujadili? Unasubiri ulishwe matapishi ya CCN na TBC?

Endeleeni kuandamana kwa kila kitu ambacho ni kero...Tanzania.

Kusoma unafikiri ni kusoma biblia tu..nyinyi wasoma biblia naona mlishwe matapishi kweli...kila mahali kila kitu biblia..ugonjwa huo!

Maandamano ambayo "niliyasubiri kwa hamu ni kuibiwa kura" sasa mmebadilisha mnadai bei ya umeme, umeme ni mambo ya utaalamu siyo siasa mkuu!

Kuibiwa mshakubali yaishe tuelezeni? tunataka hayo maandamano..hiyo ndio siasa mkuu.
 
Kama utaalamu TUNAKUZIDI, na tena utaalamu wa Uhandisi.

Kama ni Uchumi tunakuzidi. Kama ni sheria tunakuzidi. kama ni Uchumi pia tunakuzidi.

Sisi tunasema MAANDAMANO ni lazima. Haya leta kingine sisi tukibiruebirue pia.

Humzidi chochote wewe..unawazidi wanyamwezi wenzako tena kutoka sikonge...nasikia ulisomeshwa na kijiji.
 
Topical,
Ningekushauri urudi shule kwanza maana inaelekea kuwa hufahamu maana ya siasa. Siku utakapoelewa siasa ni nini na uhusiano katika ya siasa na maamuzi ya kitaalamu siku hiyo tunaweza kujadiliana vizuri, bila jazba wala matusi. Ni watu wa aina yako wanaodhani kuwa " siasa" na viongozi wa kisiasa ni "mizuka" ndio waliotufikisha hapa tulipofika. Nitakubaliana nawe iwapo ungelizungumzia Siasa as a science na viongozi wanaoheshimu misingi ya kisayansi na Wanasiasi wenye kuongozwa na ufisadi. Lakini kusema "Maandamano" ni siasa tu sikuelewi!
 
Endeleeni kuandamana kwa kila kitu ambacho ni kero...Tanzania.

Kusoma unafikiri ni kusoma biblia tu..nyinyi wasoma biblia naona mlishwe matapishi kweli...kila mahali kila kitu biblia..ugonjwa huo!

Maandamano ambayo "niliyasubiri kwa hamu ni kuibiwa kura" sasa mmebadilisha mnadai bei ya umeme, umeme ni mambo ya utaalamu siyo siasa mkuu!

Kuibiwa mshakubali yaishe tuelezeni? tunataka hayo maandamano..hiyo ndio siasa mkuu.

tropical, kwani tz kuwe na akina kikwete na mawaziri wabunge kama elimu/taaluma tu inasaidia? Kumbe hujui hata ni kwa nini ulipiga kura? Dah kazi kwelikweli! Politcs and profesional should be in a balance
 
Topical,
Ningekushauri urudi shule kwanza maana inaelekea kuwa hufahamu maana ya siasa. Siku utakapoelewa siasa ni nini na uhusiano katika ya siasa na maamuzi ya kitaalamu siku hiyo tunaweza kujadiliana vizuri, bila jazba wala matusi. Ni watu wa aina yako wanaodhani kuwa " siasa" na viongozi wa kisiasa ni "mizuka" ndio waliotufikisha hapa tulipofika. Nitakubaliana nawe iwapo ungelizungumzia Siasa as a science na viongozi wanaoheshimu misingi ya kisayansi na Wanasiasi wenye kuongozwa na ufisadi. Lakini kusema "Maandamano" ni siasa tu sikuelewi!

Mkuu kila mtu atarudi shule atakaye kuwa tofauti na wewe, shule zenyewe zitoke wapi mkuu CCM walishaziua

Maoni yangu ni kwamba kuna kero nyingi sana nimezoorezesha hapo juu...tutaandamana zote? maana kwangu mimi umeme ni cha mtoto..tuandamanane kwa kero za maji kwanza!

Besides, Vipi kuhusu kuibiwa kura zetu tutaandamana lini? mkuu mnatuchanganya sana...
 
tropical, kwani tz kuwe na akina kikwete na mawaziri wabunge kama elimu/taaluma tu inasaidia? Kumbe hujui hata ni kwa nini ulipiga kura? Dah kazi kwelikweli! Politcs and profesional should be in a balance

Kuandamana kwa ajili ya kero 1 kati ya kero 1000! akili yangu inakataa mkuu..sijawasoma kabisa!
 
I expect watu wote; CUF, CCM NCCR, na vyama vyote wataunga mkono hii issue. Unless wao hawaoni umuhimu wa hili issue; its comes a time when ushabiki tunauweka pembeni na tunajumuika wote kama wana jamii

Mkuu,

Mara nyingi mimi husema kuwa vyama vya upinzani vinaweza kufanya kazi pamoja katika baadhi ya mambo ambayo yanawaunganisha wananchi wote, wenye vyama na wasio na vyama.

Huu mtindo wa chama kimoja kukurupuka na idea nzuri na kuitangaza moja kwa moja sioni kama nimfumo unaowasaidia sana kama upinzani.

Kila chama cha upinzani wanapoona kitu, jambo ambalo linawaunganisha wananchi wote basi wangeliwasiliana na vyama vyengine kuwapa dokezo wa idea yao na kupata feedback.hapa ni kuwa wana-establish lines of communication.

Sio kila chama kitakubali kushiriki au kuunga mkono kila idea. Lakini kwa chama kimoja kuweza kukishawishi chengine na kukishirikisha ni kujipa hadhi mbele ya jamii.Ile dhana ya kujipa ujiko itafutika na itakuwa chenyewe kinaonesha kwa vitendo kuwa kinafanya kazi kwa maslahi ya wananchi wote.

Kwa kutegemea kuwa chama kije kwenye vyombo vya habari kiseme kinafanya maandamano na kinaomba vyama vyengine viunge mkono ni (utoto wa kisiasa) political immaturity kwa sababu lengo sio hasa kuwasilisha vilio vya wananchi bali ni mtaji wa kisiasa wa kukipa ujiko chama fulani.

Na kwa njia hii basi vyama vya upinzani ,vitabaki kuwa wasindikizaji kwa muda mrefu.

CHADEMA kama kina dhamira ya kuungwa mkono na wananchi wote katika hili basi iwasiliane na Uongozi wa vyama vyengine. Maandamano yatafanikiwa sana.Wananchi wakiona kuwa Upinzani unafanya kazi kama united force,wananchi wanajenga matumaini kuwa mbadala wa mfumo uliopo upo, tena ni imara.
 
Hivi busara za viongozi wa CDM ziko wapi? mseme tu mnataka umaarufu mkiandamana nchi nzima mnawakoa mafisadi? are you serious!! where is the logic besides CDM is a political party!!!!!!!!!! and not a pressure group!!!! kumbe hata CDM kuna vilaza wa siasa namna hiyo!!! waacheni chama cha watumiaji "consumers whatever they can call them selve" waandamana sana sana muwaunge mkono!!! shame on you. CDM is a powerful and very popular party to seek such a cheap popularity.

Acheni vurugugu zenu mnatuharibia nchi nyinyi na mafisadi sawa tu! tuawaambieni tofauti if you you have any all you want is chaos we are now getting tired and sick of you!!!!!!!!!!!!!. And remmember whatever goes arround comes arround. unless you are sure that you are just a pressure group, so there is no way you will become a rulling party, be prepared to face the same chaos should CDM (GOD forbid! ) come into power in that form!

CDM has greater potential to do well without being a bunch of thugs that is causing chaos every now and then. peolpe will hate it the was they hate FISADIS actully as of now the difference between the two of you is the SAME! (Sic!)

Gee! Stupidity can be contagious!

Hii ni issue inayotugusa wote.... naomba tuifanyie kazi Dr. Slaa Je mikakati ya kuomba kibali cha maandamo mapema imeshafanyika; sababu niwajuavyo hawa watu wataweka kila pingamizi ili hili jambo lisifanikiwe.... tukipata kibali hata wale waoga nao watajumuika nasi.
 
Miaka miwili iliyopita nilishirikiana na baadhi ya waachumi kutoka NYU kufanya study ya Umeme kusini mwa jangwa la Sahara. Ukweli ni kwamba tatizo sio bei ya umeme, bali tatizo ni ukiritimba ndani ya Tanesco.

Tangu Tanesco ianzishwe 1963 ni 15% ya watanzania wote ambao wamepata umeme, nao walio nao wanapata 140 days za power outages sawa na miezi 4 ya bila umeme. Serikali yoyote inategemea kodi kutoka kwenye viwanda vya uzalishaji nchini kwake, sasa kama miezi minne katika mwaka viwanda vinatumia umeme wa majenereta then hii expenses inakwenda kuwa against the revenue kwenye P&L na matokeo yake ni lower tax bracket na Tanzaia inakosa pato lake la halali.

Tatizo sio bei ndani ya Tanesco, bali tatizo ni mfumo mzima wa Tanesco. Nimategemeo yangu CDM wamefanya study na wataleta mapendekezo katika mchakato huo mzima wa maandamano. Kwamba ni muda muafaka Tanesco ivunjevunjwe kwenye vipande vitatu, yaani Uzalishaji, Usambaziji na Uuzaji. Uzalishaji uwe unashikiliwa na serikali sababu ya security reasons, usambazaji uwe ni partnership kati ya serikali na private sector na uuzaji uwe private sectors, kampuni zishindane market shares ili kudetermine price.

Hizi principle tatu zikitumika Tanesco inaweza kuwa mafanikio. Ikumbukwe Tanesco inakuwa kwa asilimia 0.3% kwa mwaka, hii ni aibu kubwa sana. Tanesco inatakiwa ikuwe at least kwa asilimia 6% kwa mwaka.

CDM lazima wajenge debate ambayo itaonyesha kweli Tanesco inabidi ibadilike, lazima waanzishe mchakato sambamba na ule wa katiba. Umeme ndio chanzo cha maendeleo cha nchi yoyote. MKUKUTA, Kilimo Kwanza, MDGs na nyinginezo zote haziwezi kufanikishwa kama umeme unakatika miezi 4 katika miezi 12.

CCM na serikali wanafumbia jicho swala la Tanesco, kila mmoja anaogopa kufanya recommendation za kubadilisha mfumo mbovu ndani ya Tanesco. Mkapa na timu yake ya wabinafsishaji walitaka kuibia nchi kwa mfumo wao mbovu ule. Tanesco inajiendesha kiasara, ina labor cost kubwa sana, sasa ni muda muafaka kubadilisha mfumo mzima ambao hauna kichwa wala miguu.

...Mtanganyika, umeongea ya maana sana. Tanesco inapata hasara kwa ajili ya uendeshaji wenye upungufu mkubwa wa ufanisi na tija. Wanaibiwa sana umeme, miundombinu mibovu kabisa, mahitaji ya umeme kuzidi uwezo na wafanyakazi wasioleta tija katika kazi wanazofanya.

...Umeme usipotoka wanapoteza mapato mengi kwa taifa, viwanda na wananchi wazalishaji mali. Hatimae wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

...Tanesco inahitaji kupewa uhuru wa utendaji wenye mwingilio mdogo kabisa wa kisiasa [only on effecting policy issues], kupata kiongozi atakaye ibadili kuwa ya kisasa na hatimae kuindesha bila hasara. Hili linawezekana, kama tuko serious kujenga uchumi wetu. Willpower is all that is needed.
 
Dowans inatuathiri wengi.Hiii nchi jamani..On few wana benefit na hili Sakata.Hakika Tanzania ni nchi ya amani,tunaibiwa wazi wazi tunakaa tunaangalia tu...
 
Topical,
Ningekushauri urudi shule kwanza maana inaelekea kuwa hufahamu maana ya siasa. Siku utakapoelewa siasa ni nini na uhusiano katika ya siasa na maamuzi ya kitaalamu siku hiyo tunaweza kujadiliana vizuri, bila jazba wala matusi. Ni watu wa aina yako wanaodhani kuwa " siasa" na viongozi wa kisiasa ni "mizuka" ndio waliotufikisha hapa tulipofika. Nitakubaliana nawe iwapo ungelizungumzia Siasa as a science na viongozi wanaoheshimu misingi ya kisayansi na Wanasiasi wenye kuongozwa na ufisadi. Lakini kusema "Maandamano" ni siasa tu sikuelewi!

Dr. Slaa kwanza nikupe tena pongezi ya kurudi hapa dimbani na kuchangia kwenye midahalo muhimu inayoihusu Tanzania na maendeleo yake. Ni wazi kabisa swala la umeme ni nyeti kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yoyote.

Nadhani mimi na wewe tutakubaliana kabisa kwamba Wanasiasa hawana njia yoyote mbadala ya kuendesha kampuni kwa faida. Hii iwe Marekani au Tanzania, wanasiasa inabidi wajikite kwenye kutengeza sera ambazo zitalinda maslahi ya wananchi.

Kuandama kupinga ongezeko la bei ya umeme wa Tanesco ni njia moja lakini swali linakuja jee tutaandamana mara ngapi? Jee ni nini tatizo ndani ya Tanesco? Nadhani mimi na wewe na wengine tutakubaliana tatizo ndani ya Tanesco sio ongezeko la bei, bali tatizo ni gharama za juu za uendeshaji Tanesco (High Operating Cost). Sasa jee ni nini kifanyike ili kupunguza gharama hizi za uendeshaji ambazo ndizo chanzo cha kupungua kwa bei. Ni lazima Tanesco ivunjwe vunjwe vipande na kuongeza ushindani. Hii ndio long term solution. Maandamano yanaweza kushusha bei, lakini 2 years badae Tanesco italazimu kupandisha bei tuu.

Kwa maono yangu nadhani CDM inatakiwa ije na njia mbadala ya nini kifanyike ndani ya Tanesco. Badala ya kusema hatutaki bei mpya na kisha kukaa kimya, ni muhimu mkapendekeza nini kifanyike ili kuweka bei katika constant rate.

CCM wanaogopa swala zima la Tanesco, hawana idea, Mkapa alileta baba na mwana kuja kununua Tanesco watanzania wakashituka kilichobaki ni adisi. CDM lazima mje na different approach nazo ni long term recommendation ambazo hazibase kwenye political gain, bali long term economical gain kwa Tanzania. Maandamano inaweza kuwa njia moja ya kuamsha debate kuhusu swala la Tanesco, na katika debate hizo tunaweza kupata long term solution. Tanesco ni ya WATANZANI, ilianzishwa kwa pesa za walipa kodi, ikaendeshwa miaka nenda uje na pesa za walipa kodi, hivyo ni mali ya walipa kodi. Basi ni muhimu viongozi ambao mnawakilisha walipa kodi mkaandaa mchakato ambao utapelekea matokeo ambayo yatampa favor mlipa kodi.

Mwisho.... Kwanza tuanze na kuvunja ile bodi ya Tanesco, haifanyi kazi, wanakula mishara na kuchangia special group kuwin tender.
 
Back
Top Bottom