Chadema yaandaa maandamano kupinga bei mpya ya umeme

Hivi busara za viongozi wa CDM ziko wapi? mseme tu mnataka umaarufu mkiandamana nchi nzima mnawakoa mafisadi? are you serious!! where is the logic besides CDM is a political party!!!!!!!!!! and not a pressure group!!!! kumbe hata CDM kuna vilaza wa siasa namna hiyo!!! waacheni chama cha watumiaji "consumers whatever they can call them selve" waandamana sana sana muwaunge mkono!!! shame on you. CDM is a powerful and very popular party to seek such a cheap popularity.

Acheni vurugugu zenu mnatuharibia nchi nyinyi na mafisadi sawa tu! tuawaambieni tofauti if you you have any all you want is chaos we are now getting tired and sick of you!!!!!!!!!!!!!. And remmember whatever goes arround comes arround. unless you are sure that you are just a pressure group, so there is no way you will become a rulling party, be prepared to face the same chaos should CDM (GOD forbid! ) come into power in that form!

CDM has greater potential to do well without being a bunch of thugs that is causing chaos every now and then. peolpe will hate it the was they hate FISADIS actully as of now the difference between the two of you is the SAME! (Sic!)
Zuzuuuuu...........................................!! Busara za CCM kutumbandishia umeme kibwege ziko wapi??
 
Sioni natija ya maandamano! Maendeleo maanake ni kujifunga mkanda. Maendeleo hayaji bila wananchi kushirikishwa. Serikali iachwe ifanye kazi yake.

Hata chama chochote kingekuwa madarakani haya yangetokea na bei ya cement ingezidi kupanda kwani hata mafuta pia yamepanda.

Sisi kama tungekuwa great thinkers tungelipendekeza serikali kurekebisha sheria ili kuwa na ushindani katika uwekezaji katika nyanja ya umeme. Pia serikali iruhusu makampuni binafsi kusambaza umeme. Tanesco wabaki ni wazalishaji tu. Nazungumzia fani na sio ushabiki wa kijinga.
 
Wana JF,
Msameheni hajui asemalo wala atendalo. Wenye uchungu na nchi hii, watafika mahali wataamua kuchukua hatua kuipigania nchi yao. Wenye kuonja, wenye kulamba, wenye hisa kwenye ufisadi kamwe hawatawaonea huruma Watanzania wenzao. Nyantela ajiulize asilimia ngapi ya Watanzania wa Vijijini wana Umeme, na wangapi wa mjini. Ni kwanini tuko hivyo wakati tuliowapa dhamana kina Mkapa walijianzishia Makampuni ya kufua Umeme kwa jasho la Watanzania Maskini ikiwemo US Dolla 7 za NSSF zilizokopwa na kuwekewa Guarantee na Serikali? Inawezekana hajui kinachoendelea, ndio maana nasema msipoteze muda na wa aina hii. Wenye nia njema na mapenzi mema na Taifa letu tusonge mbele. Tukiwa na ujasiri tutafika. Maneno hayatatufikisha mahali wala kumtukana kwenye Jamvi hapatatupeleka mbele licha ya kutengeneza hasira. Inawezekana ndio lengo lake(lao) kutuondoa kutoka kwenye "critical thinking" itakayotusaidia mikakati ya kusonga mbele.
 
hivi busara za viongozi wa cdm ziko wapi? Mseme tu mnataka umaarufu mkiandamana nchi nzima mnawakoa mafisadi? Are you serious!! Where is the logic besides cdm is a political party!!!!!!!!!! And not a pressure group!!!! Kumbe hata cdm kuna vilaza wa siasa namna hiyo!!! Waacheni chama cha watumiaji "consumers whatever they can call them selve" waandamana sana sana muwaunge mkono!!! Shame on you. Cdm is a powerful and very popular party to seek such a cheap popularity.

acheni vurugugu zenu mnatuharibia nchi nyinyi na mafisadi sawa tu! Tuawaambieni tofauti if you you have any all you want is chaos we are now getting tired and sick of you!!!!!!!!!!!!!. And remmember whatever goes arround comes arround. Unless you are sure that you are just a pressure group, so there is no way you will become a rulling party, be prepared to face the same chaos should cdm (god forbid! ) come into power in that form!

cdm has greater potential to do well without being a bunch of thugs that is causing chaos every now and then. Peolpe will hate it the was they hate fisadis actully as of now the difference between the two of you is the same! (sic!)

crap!!!
 
Wana JF,
Msameheni hajui asemalo wala atendalo. Wenye uchungu na nchi hii, watafika mahali wataamua kuchukua hatua kuipigania nchi yao. Wenye kuonja, wenye kulamba, wenye hisa kwenye ufisadi kamwe hawatawaonea huruma Watanzania wenzao. Nyantela ajiulize asilimia ngapi ya Watanzania wa Vijijini wana Umeme, na wangapi wa mjini. Ni kwanini tuko hivyo wakati tuliowapa dhamana kina Mkapa walijianzishia Makampuni ya kufua Umeme kwa jasho la Watanzania Maskini ikiwemo US Dolla 7 za NSSF zilizokopwa na kuwekewa Guarantee na Serikali? Inawezekana hajui kinachoendelea, ndio maana nasema msipoteze muda na wa aina hii. Wenye nia njema na mapenzi mema na Taifa letu tusonge mbele. Tukiwa na ujasiri tutafika. Maneno hayatatufikisha mahali wala kumtukana kwenye Jamvi hapatatupeleka mbele licha ya kutengeneza hasira. Inawezekana ndio lengo lake(lao) kutuondoa kutoka kwenye "critical thinking" itakayotusaidia mikakati ya kusonga mbele.

Unaonekana bado una hasira ya kupigwa chini kwenye uchaguzi uliopita..punguza jazba mkuu!

Asiyekubali kushindwa hana haja ya "kushindana"

Unaeleweka kwa wachache sana die hard chadema..fanya critical analysis..
 
I expect watu wote; CUF, CCM NCCR, na vyama vyote wataunga mkono hii issue. Unless wao hawaoni umuhimu wa hili issue; its comes a time when ushabiki tunauweka pembeni na tunajumuika wote kama wana jamii

I like, kwani hili linatuumiza wote, ccm,chadema, cuf, wananchi wote kwa ujumla tuamke kwa pamoja
 
Wana JF,
Msameheni hajui asemalo wala atendalo. Wenye uchungu na nchi hii, watafika mahali wataamua kuchukua hatua kuipigania nchi yao. Wenye kuonja, wenye kulamba, wenye hisa kwenye ufisadi kamwe hawatawaonea huruma Watanzania wenzao. Nyantela ajiulize asilimia ngapi ya Watanzania wa Vijijini wana Umeme, na wangapi wa mjini. Ni kwanini tuko hivyo wakati tuliowapa dhamana kina Mkapa walijianzishia Makampuni ya kufua Umeme kwa jasho la Watanzania Maskini ikiwemo US Dolla 7 za NSSF zilizokopwa na kuwekewa Guarantee na Serikali? Inawezekana hajui kinachoendelea, ndio maana nasema msipoteze muda na wa aina hii. Wenye nia njema na mapenzi mema na Taifa letu tusonge mbele. Tukiwa na ujasiri tutafika. Maneno hayatatufikisha mahali wala kumtukana kwenye Jamvi hapatatupeleka mbele licha ya kutengeneza hasira. Inawezekana ndio lengo lake(lao) kutuondoa kutoka kwenye "critical thinking" itakayotusaidia mikakati ya kusonga mbele.

Ahsante sana Dr. Slaa,
Mimi ninaomba kufahamu kama kweli maandamano haya yatakubaliwa kwani ninavyoona watu bado wako kwenye excited state kwa maana ya majeraha ya kura zao halali kuchakachuliwa, Makali ya mgawo wa umeme na hila za CCM kuendeleza kutumia nguvu kunyang'anya manispaa na halimashauri ambazo kimsingi zinatakiwa ziongozwe na CDM na wananchi kuanza kufurahia sera za CDM, kama vile Elimu bure, Afya Bure na Makazi bura na hata kushughulikia mafisadi katika ngazi ya wilaya na jiji kama ilivyo kwa Karatu 2000 kwenye sera ya Kodi, Elimu na Maji.

hofu yangu ni wataturuhusu?

Peoples Power
 
Unaonekana bado una hasira ya kupigwa chini kwenye uchaguzi uliopita..punguza jazba mkuu!

Asiyekubali kushindwa hana haja ya "kushindana"

Unaeleweka kwa wachache sana die hard chadema..fanya critical analysis..
Hivi hii issue ina uhusiano gani na kupanda kwa umeme ?; au wewe unaona hii bei ni poa?;
Je wananchi wakifanikiwa na bei kutopanda wewe hii haitakusaidia?

Kweli bado tuna safari ndefu, lakini hakuna neno ngoja sisi tukufanyie kazi ili wewe na wajukuu zako waje wale mbivu....
 
Miaka miwili iliyopita nilishirikiana na baadhi ya waachumi kutoka NYU kufanya study ya Umeme kusini mwa jangwa la Sahara. Ukweli ni kwamba tatizo sio bei ya umeme, bali tatizo ni ukiritimba ndani ya Tanesco.

Tangu Tanesco ianzishwe 1963 ni 15% ya watanzania wote ambao wamepata umeme, nao walio nao wanapata 140 days za power outages sawa na miezi 4 ya bila umeme. Serikali yoyote inategemea kodi kutoka kwenye viwanda vya uzalishaji nchini kwake, sasa kama miezi minne katika mwaka viwanda vinatumia umeme wa majenereta then hii expenses inakwenda kuwa against the revenue kwenye P&L na matokeo yake ni lower tax bracket na Tanzaia inakosa pato lake la halali.

Tatizo sio bei ndani ya Tanesco, bali tatizo ni mfumo mzima wa Tanesco. Nimategemeo yangu CDM wamefanya study na wataleta mapendekezo katika mchakato huo mzima wa maandamano. Kwamba ni muda muafaka Tanesco ivunjevunjwe kwenye vipande vitatu, yaani Uzalishaji, Usambaziji na Uuzaji. Uzalishaji uwe unashikiliwa na serikali sababu ya security reasons, usambazaji uwe ni partnership kati ya serikali na private sector na uuzaji uwe private sectors, kampuni zishindane market shares ili kudetermine price.

Hizi principle tatu zikitumika Tanesco inaweza kuwa mafanikio. Ikumbukwe Tanesco inakuwa kwa asilimia 0.3% kwa mwaka, hii ni aibu kubwa sana. Tanesco inatakiwa ikuwe at least kwa asilimia 6% kwa mwaka.

CDM lazima wajenge debate ambayo itaonyesha kweli Tanesco inabidi ibadilike, lazima waanzishe mchakato sambamba na ule wa katiba. Umeme ndio chanzo cha maendeleo cha nchi yoyote. MKUKUTA, Kilimo Kwanza, MDGs na nyinginezo zote haziwezi kufanikishwa kama umeme unakatika miezi 4 katika miezi 12.

CCM na serikali wanafumbia jicho swala la Tanesco, kila mmoja anaogopa kufanya recommendation za kubadilisha mfumo mbovu ndani ya Tanesco. Mkapa na timu yake ya wabinafsishaji walitaka kuibia nchi kwa mfumo wao mbovu ule. Tanesco inajiendesha kiasara, ina labor cost kubwa sana, sasa ni muda muafaka kubadilisha mfumo mzima ambao hauna kichwa wala miguu.
 
Unaonekana bado una hasira ya kupigwa chini kwenye uchaguzi uliopita..punguza jazba mkuu!

Asiyekubali kushindwa hana haja ya "kushindana"

Unaeleweka kwa wachache sana die hard chadema..fanya critical analysis..

Anauchungu na TZ na watu wake ninavyo mfahamu DR. Slaa si mtu mwenye Uchu wa madaraka ila ana msimamo, Kiboko ya Mafisadi na an historia ya kutong'ang'ania uongozi maana mara zote amekuwa akiombwa kugombea hilo nafikiri huna shaka nalo.
 
Hivi hii issue ina uhusiano gani na kupanda kwa umeme ?; au wewe unaona hii bei ni poa?;
Je wananchi wakifanikiwa na bei kutopanda wewe hii haitakusaidia?

Kweli bado tuna safari ndefu, lakini hakuna neno ngoja sisi tukufanyie kazi ili wewe na wajukuu zako waje wale mbivu....

Sivyo unavyofikiri..

Kuandamana ni siasa zaidi

mambo ya Tanesco ni Utaalamu zaidi, napendelea watu waheshimu wataalamu kuliko wanasiasa kama Slaa "ambao wamekasirika from day one to the end"
 
Sivyo unavyofikiri..

Kuandamana ni siasa zaidi

mambo ya Tanesco ni Utaalamu zaidi, napendelea watu waheshimu wataalamu kuliko wanasiasa kama Slaa "ambao wamekasirika from day one to the end"

Kupandisha bei kunahitaji utaalamu gani?; kujua kwamba siwezi kuafford kulipia hilo ongezeko kunahitaji utaalamu??; Mpaka sasa watu wengi majiko ya umeme ni mapambo hawayatumii tena, sasa baada ya ongezeko si hata hizo taa zinakuwa ni mapambo.

Na kama si maandamo wewe unasuggest nini la kufanya ili wananchi waweze kusikilizwa??
 
CHADEMA waache cheap popularity na sympathy za kitoto! kabla umeme hauja tangazwa kupanda...EWURA waliendesha Tashtiti nchi nzima kwa wadau kutakiwa kutoa comments zao juu ya ombi la ongezeko la asilimia 34 liliombwa na TANESCO. Sikuona kiongozi yoyote wa CHADEMA pale Karim Jee Hall kupinga ongezeko hilo, Tashtiti kama hili pia ilifanyika mikoani na CHADEMA wakaa kimya. Leo hii wanaongea utumbo gani.!?

Hivi vitisho vya maandamano ni siasa zilizopitwa na wakati na ni za kitoto zaidi..CHADEMA mnatakiwa mkue kiitikadi sio mnalila lia tu na mkipewa nafasi ya kujitetea hamtokeo.
 
Wakati huo huo IPTL izalishe isizalishe wanalipwa pesa yao. Inauma sana!!!!!!!!! Tutafika tumechoka!!
 
Hivi busara za viongozi wa CDM ziko wapi? mseme tu mnataka umaarufu mkiandamana nchi nzima mnawakoa mafisadi? are you serious!! where is the logic besides CDM is a political party!!!!!!!!!! and not a pressure group!!!! kumbe hata CDM kuna vilaza wa siasa namna hiyo!!! waacheni chama cha watumiaji "consumers whatever they can call them selve" waandamana sana sana muwaunge mkono!!! shame on you. CDM is a powerful and very popular party to seek such a cheap popularity.

Acheni vurugugu zenu mnatuharibia nchi nyinyi na mafisadi sawa tu! tuawaambieni tofauti if you you have any all you want is chaos we are now getting tired and sick of you!!!!!!!!!!!!!. And remmember whatever goes arround comes arround. unless you are sure that you are just a pressure group, so there is no way you will become a rulling party, be prepared to face the same chaos should CDM (GOD forbid! ) come into power in that form!

CDM has greater potential to do well without being a bunch of thugs that is causing chaos every now and then. peolpe will hate it the was they hate FISADIS actully as of now the difference between the two of you is the SAME! (Sic!)

ndugu ivi kweli unaishi Tanzania?unaweza ukalaumu mtu yeyote anaejitokeza kutuetea sisi watumia umeme? Au wewe unalelewa nini? Inaingia akilini sh.360 per unit? Usipinge hali mradi umepinga tu,acha uendawazimu na kama ccm imekuweka msukule kaa uko uko usiwalete watanzania utani! Hata kwa asiye na chama ata ccm wote tunatumia umeme,acha kuleta udondocha wetu. Nimechukizwa sana na mchango taka wako.
 
Umeme waiweka serikali pabaya
• CHADEMA kufanya maandamano nchi nzima kupinga bei mpya

na Mwandishi wetu

amka2.gif
KUKOSEKANA kwa umeme wa uhakika na kupandishwa kwa gharama za nishati hiyo hivi karibuni kunaiweka serikali ya Rais Jakaya Kikwete katika shinikizo kali la kupingwa na umma wa Watanzania nchi nzima ukiongozwa na chama kikuu cha upinzani – CHADEMA.
CHADEMA jana ilitangaza msimamo mkali wa kufanya maandamano nchi nzima wenye lengo la kuhamasisha na kuwaongoza wananchi wote kupinga ongezeko kubwa la gharama za umeme ikiwa serikali haitatengua haraka gharama mpya za kutumia nishati hiyo zilizotangazwa hivi karibuni.
Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Madini nchini (EWURA) juzi ilitangaza kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni mtaa wa Ufipa jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, Erasto Tumbo, alisema kiwango hicho ni kikubwa mno kwa wananchi wa kawaida.
Alisema ni vema gharama hizo za umeme zingebebwa na serikali kwa sababu yenyewe ni moja ya taasisi zinazolimbikiza madeni sugu ya TANESCO hivyo kulifanya shirika hilo kushindwa kujiendesha.
"Kulingana na kipato cha wananchi wengi wa kawaida kuwa cha chini ongezeko hilo la asilimia 18 linakuwa mzigo mwingine mzito unaokuja kuyakandamiza maisha ya wananchi wa kawaida," alisema Tumbo.
Aliitaka serikali kusitisha haraka ongezeko hilo kwani litawaongezea wananchi machungu ya maisha.
"Tunaiomba serikali isitishe ongezeko hili na kama itashindwa CHADEMA tutaitisha maandamano ya amani nchi nzima kupinga ongezeko hilo," alisema Tumbo.
Alisema kwa kuwa serikali ndiye mdaiwa sugu wa TANESCO ni vema ikaweka wazi inadaiwa kiasi gani na shirika hilo pamoja na madeni ya vigogo na taasisi nyingine badala ya kukimbilia kuutua mzigo huo kwa wananchi ambao wengi hawana uwezo wa kumudu gharama mpya za umeme zilizotangazwa.
Kupandishwa kwa gharama hizo kunaweza kuwa ni mpango wa serikali wa kulipa deni la Dowans ambalo waliamriwa kulilipa na Mahakama ya Biashara ya kimataifa hivi karibuni.
CHADEMA pia imeishutumu TANESCO kwa tabia yake ya kupenda kujitangaza kila kukicha kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari wakati bado inashindwa hata kuboresha huduma zake.
Wakati CHADEMA ikitoa msimamo huo jana hiyo hiyo serikali kupitia kwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, ilitangaza kuridhia kupanda kwa gharama zilizotangazwa na Ewura.
Ngeleja alisema kupanda kwa bei ya umeme hakuna uhusiano wowote na suala la kutafuta pesa ili kulipa deni la sh bilioni 185 ambalo TANESCO inadaiwa na kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans.
Serikali imewataka wananchi kukubali gharama hiyo ili kulifanya shirika hilo kupata pesa kwani limekuwa likijiendesha bila kutegemea ruzuku kutoka serikalini.
Ngeleja alitoa msimamo huo jana alipokuwa katika ziara ya kikazi kwenye ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura).
"….. TANESCO linajiendesha lenyewe na halitegemei ruzuku yoyote toka serikalini. Katika kupanda kwa bei ya umeme tunajua wananchi ndio wanaoumia kwa hilo, lakini hatuwezi kumfurahisha kila mtu…bei wanazotoza haziendani na gharama halisi za uendeshaji.
"Kwa hili lazima wananchi waelewe juu ya kupanda kwa gharama hizo, wote ni wa hapa hapa, suala sio kubinafsisha shirika bali kutafuta njia ya kutatua tatizo," alisema Waziri Ngeleja.
Katika maelezo yake Ngeleja alisema gharama za umeme kwa wateja hapa nchini ziko chini ikilinganishwa na nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema mwaka 2006 shirika lilipata hasara ya sh bilioni 168 na mwaka jana ilipoteza sh bilioni 5 kama hasara.
"Nchi inakosa umeme wa uhakika kwa sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu mibovu na zingine; ambapo maombi ya kupandisha gharama hizo kwa Ewura ni ya msingi ingawa wananchi wanalalamika," alimalizia Ngeleja.

Tunaishukuru sana CHADEMA kwa hili.
Hakika hii inashabihiana kabisa na Thread yangu ya jana, ambayo niliomba CHADEMA kama chama chenye dira sahihi na dhamira kulikomboa taifa hili, itoe Tamko Rasmi kwa Taifa ikiwa ni pamoja na kutangaza maandamano ya Amani kitaifa. Thread ipo chini hapa...

icon1.png
Chadema itoe Tamko kuhusu Tanesco, EWURA; Wizara ya Nishati/Madini na dira ya Taifa!

TANESCO ni nini? EWURA ni nini? na Nchi yetu inapelekwa wapi na Taasisi hizi??

Ni hali ya Masikitiko makubwa, Uchumi unavurugika, Wananchi wanazidi kudidimia ktk dimbwi la kukosa huduma, ziwe za muhimu hasa zile zinazotegemea uzalishaji mdogo mdogo kwa kutumia nishati ya umeme kama ujasiriamali, huduma za mahitaji ya vyakula na vinyaji baridi mfano maziwa, maji, samaki, nyama nk. Ajira binafsi kama saloon, uchomeleaji nk; Vyote hivi vimekuwa vikitegemea sana mahitaji ya umeme ijapokuwa umekuwa ukipatikana kimkanda-mkanda, ila watanzania wamekuwa wakivumilia tu na kujiendeshea maisha yao ya kuokoteza na kujikwamua kiujasiriamali.

Kitendo cha Tanesco kuvurunda tena ktk usimamizi wa mitambo kuwa eti baadhi kusemekana umeharibika, na kusasabisha adha kubwa kwa Taifa nzima kwa kukata umeme kila mara ni aibu na jambo ambalo limekuwa likitokea kila mwaka na kila wakati bila wahusika kuwajibika bali wao huachiwa tu kutoa 'ufafanuzi wa kisanii' ambao mara nyingi ni 'porojo tu za kujilinda nafasi zao na maslahi wa waliowaweka madarakani'. Haifai tena!

Hii ni dhuluma, na usaliti mkubwa mno kwa taifa na wananchi wanaohangaikia maisha yao kila kukicha. Wanavutwa nyuma na utendaji uliooza, na Hakuna maendeleo yoyote kwa mtindo huu. Nchi itazidi kuangamia kwa umaskini sababu ya watu wachache wanaolindana.
Watanzania wanahitaji dira na Mwelekeo wa hali hii. Na EWURA pasipo kujali maisha ya wa tanzania yanavyodhoofika, nao wamekubali msukumo wa TANESCO kuongeza bei ya huduma za Tanesco kuanzia mwakani. EWURA ni kwa maslahi ya nani? Tanesco ni kwa maslahi ya nani na ni ya nini Tanzania? EWURA ina maslahi gani kwa Watanzania?

TUNAIOMBA CHADEMA itoe TAMKO na dira kwa Taifa hili. Na hata kama inafaa itangaze rasmi maaandamani ya Amani kwa nchi nzima kupinga kuangamia kwa nchi yetu! Tanesco ivunjwe na Wahusika wa EWURA na Wizara ya Nishati na Madini wawajibike. La sivyo watanzania kwa kiwango kikubwa wanazidi kukata tamaa mno na hawatasikia la yeyote kwamba wanaye watetezi wa maisha yao.

Mungu ibariki nchi yetu. Naomba kuwasilisha.
 
Kupandisha bei kunahitaji utaalamu gani?; kujua kwamba siwezi kuafford kulipia hilo ongezeko kunahitaji utaalamu??; Mpaka sasa watu wengi majiko ya umeme ni mapambo hawayatumii tena, sasa baada ya ongezeko si hata hizo taa zinakuwa ni mapambo.

Na kama si maandamo wewe unasuggest nini la kufanya ili wananchi waweze kusikilizwa??

Huwezi kuzuia bei kupanda kwa maandamano bana!

Njia mbadala ni "kuondoa CCM" madarakani

Uchaguzi 2015
 
Huwezi kuzuia bei kupanda kwa maandamano bana!

Njia mbadala ni "kuondoa CCM" madarakani

Uchaguzi 2015
Unaweza ukapata chochote kwa njia ya maandamo...... Hii imekuwa ikitumiwa na wananchi wote dunia nzima kudai haki zao; kuonyesha kwamba wapo pamoja na wamekerwa na kitu fulani. ndio njia ya amani na inayofaa kuliko migomo....

Kuwangoa CCM madarani alafu ndio tuombe punguzo la umeme??? for the time being si moshi wa mishumaa utatuua.

Do Not Put Off Till Tomorrow That Which You Can Do Today
 
Wee kweli wa kuja.

Unataka CHADEMA wasubiri hadi mwaka 2015?

Kama baba angelikuwa kasubiri kwa njia zako, si ajabu leo hii ungelikuwa hujazaliwa.

Kwenye Ngumi huwa kuna kupiga mbavu kwanza na mtu akisikia maumivu ya INI basi anaachia mikono juu na hapo hata boxer mbovu anajua kuwa nina sekunde kadhaa uso ni wangu. Sasa weee Chadema wamepewa USO na uliokaa kama Punching Bag na wewe unasema "subirini kwanza CCM apate pumzi ndiyo muanze kummaliza........" Sijui akili zako kama kweli zinafahamu USHINDANI.

Dunia nzima huwa inatumika sana na ndiyo maana watu huwa wanasemwa kuwa "wanaogopa maamuzi makali" kwa sababu yatawamaumiza sana wananchi. Ila kama angelikuja Rais mpya leo na kusema "TUFUNGE MIKANDA" na tukaona hata wao wanafunga, watu watawaelewa. Ila wao wanapoongeza BEI huku wanazidi kujinunulia mashangingi na safari za nje haziishi, dawa yao ni MGOMO na MAANDAMAMO.

Ile walk out ya Bungeni ilishaanza kufanya kazi yake. Migomo ya UDOM na wanafunzi kwa ujumla nayo itazidi kulainisha mambo. Wakija kugoma Wafanyakazi hapo mtu atakuwa na hali mbaya zaidi. HAKI haijileti yenyewe ila HUPIGANIWA.

Warusi walitumia njia mbaya zaidi kwa kukiangamiza KIZAZI cha Sarah chote. Wale jamaa Wekundu walikuwa MAKATILI sana. Sidhani kama tutafika huko. Ninaombea tusifike na njia za kawaida za Maandamano na Migomo zitamuondoa SULTANI au walau kumfanya kuwa RAIA WA KAWAIDA na si mungu mtu.
Huwezi kuzuia bei kupanda kwa maandamano bana!

Njia mbadala ni "kuondoa CCM" madarakani

Uchaguzi 2015
 
Back
Top Bottom