WANA-JF;
Nimelazika kuwaandikia hasa ndugu mwanachama au mshabiki wa CHADEMA na watanzania wazalendo wenye mapenzi mema na nchi yetu popote mlipo ili niwafahamishe yafuatayo;
1. Hakuna binadamu mkamilifu. Katika siku za hivi karibuni Mh. Zitto Kabwe amekumbwa na mambo mengi ambayo kwa kiasi fulani yamesababisha wana-CHADEMA bila kujua kwamba ni njama za CCM za kutaka kuwaruga wao, nao wameingia mkenge na kuanza kushambulia viongozi wao hasa Zitto Kabwe. Narudia kusema kwamba kuhusu kilichotokea kigoma kati ya Zitto, Mwananchi, na Wabunge wengine haikuwa kitu kizuri na ndiyo maana sote tulilikemea. Hivyo, naamini Zitto kama kijana mwenzetu alisikia na atajirekebisha baada ya kuona kwamba kuna vitu anafanya ambavyo havijengi chama na badala yake anachangia kuchelewesha ukombozi wa Watanzania. Pamoja na hayo bado tuna imani kwamba Mh. Zitto ataweza kujifunza na kuendelea na ujenzi wa Taifa letu kupitia CHADEMA, kwani kuteleza siyo kuanguka. Hivyo nitoe wito kwa wazalendo wenzangu, TUACHE sasa kuendelea kufanya kazi ya NAPE na kitengo chake cha CCM cha Propaganda, ambacho kinafanya kazi ya kutakakuwagawa WANACHADEMA.
2. Kama kumbukumbu zetu ziko sawa tunaweza kukumbuka kauli ya Wasira kwamba CHADEMA itakufa ndani ya mwaka moja. Je, mmewahi kupata muda na kufikiria ni namna gani chama kinaweza kufa? kama hamjafanya hivyo, basi nyinyi wenyewe wanachama mmeamua kuua chama chenu na sasa mnaona kwamba wabunge wa CCM kumsafisha Lowassa ni sahihi na hamuonekani kukemea na badala yake mmeendelea kushambuliana nyinyi kwa nyinyi na kusahau ile approach ya wakoloni ya Divide and Rule.
3. Sawa, kuna wabunge wantuhumiwa kuomba rushwa TANESCO na wengi wao ni CCM, lkn sasa nyinyi bila kuchunguza na wala kuwa na uhakika mmeamua kufanya kazi ya kitengo cha Propaganda ya CCM bila kujua hilo. Hivi mnashindwa kujiuliza swali mmoja dogo tu kwamba mbona katika hizi mada za kuparuruana nyinyi kwa nyinyi wana-CHADEMA, watu kama kina Nape, Mwigulu (Burn Kurudi), na wote wanaolipwa na Nape kwa ajili ya kazi ya Propaganda hapa JF kama Zomba, Ritz, Mama Porojo, n.k, hawaonekani kuchangia chochote? Jibu ni rahisi tu, kwamba Wanachadema wanatimiza unabii wa Wasira wao kwa wao, bila hata ya kutafakari nini madhara ya hiki wanachofanya kwenye ujenzi na utengamano wa chama.
4 Je hamjiulizi hata swali moja tu kwamba, iweje leo Mh. Zitto kuhisiwa tu kwenye hilo sakta la TANESCO wakati Mh. Sendeka na wenzake wametajwa moja kwa moja lkn hakuna anayewashambulia hao wengine na badala yake ni Zitto ndiyo anashambuliwa sana? Je mmechunguza ni lini hawa wanaoanzisha mada zinazohusu Zitto na CHADEMA wamejiunga hapa JF? ukiangalia na kufuatilia wengi wao wana ID mpya, hivyo hilo inawezekana ikawa ni strategy ya watu fulani kutimiza kile walichoelekezwa na kitengo cha propaganda cha CCM chini ya Nape.
Mwisho naomba niseme kwamba, mimi ni kati ya watu wanaochukia ubadhirifu wowote na hata kauli za kiunafiki zenye malengo ya kuwadhoofisha watu katika ukombozi wao. Lkn pia naamini kwamba watu wana mapungufu, hivyo yawezekana Mh. Zitto naye ana mapungufu (ni kweli anayo), lkn wito wangu kwenu WANACHADEMA wote na WATANZANIA WAZALENDO WOTE popote mlipo, tusiingie kwenye mtego wa CCM wa divide and rule, na badala yake tuelekeze nguvu katika kujenga chama imara na kuwasidia viongozi wetu akiwemo Zitto ili tukakomboe nchi yetu kwa pamoja. Ukombozi wa Watanzania uko mkononi mwa CHADEMA, WANACHAMA WA CHADEMA, na WATANZANIA wazalendo wote. Na hili litawezekana tu iwapo hatutakuwa tayari kufanya kazi ya NAPE NA CCM. Nawaomba sana wazalendo wenzangu, tuamke sote na tuache kufanya kazi ya CCM, kwani CCM ilishajichokea lkn haiko tayari kuondoka madarakani.
Nawasilisha wadau.
TELO.