CHADEMA wajiandaa kutupa bomu kubwa kuhusu SIOI kuwa na PASI mbili

hivi nyie mna akili kweli sasa waingereza wawe na passport mbili bila wao kuchukua hatua walikuwa wanawasubiri nyinyi CDM siyo??!!

Suala la kuwa ana passport mbili haliwahusu wenyewe, maana nchi nyingi zina taratibu kuwa hivyo Dickson!
 
Ni kwa nini nakala hizi hazikuwa attached kwenye rufaa ya CHADEMA kwenda tume ya uchaguzi ili uteuzi wake utenguliwe? mimi habari za namna hii huwa naziona ni za kutupotezea muda wetu wa kujadili vitu vya msingi.

Yup uko sahihi mkuu
Wanatakiwa kuambatanisha ushahidi kwenye rufani yao ..sasa muamuzi atajuaje
 
Mkuu kwa hiyo Uingereza watashirikiana na Chadema katika sakata la urai wa Siyoi?

Hivi unajua sheria za Uingereza katika matumizi ya pasipoti kwa wageni? Au umeamua kujifurahisha tu?



Mkuu Ritz
Kwanini mpaka Uingereza ishirikiane na Chadema? Kwani bila ushirikiano wao ukweli utabadilika kuwa uongo?

Hizo story za Uingereza na kanuni zao baki nazo wewe ulebahatika kusoma. Ila ufahamu asilimia kubwa ya sisi wapiga kura tumeishia kidato cha nne, na kwa mitaala hii ya Mkapa lengo lenu ilikuwa ni kutufumba macho tusijue mengi mbeleni, ili mje mtutenge na mtutishe na maneno yenu ya kingereza na kitaalam. Ilibaki kidogo mfanikiwe lakini tumefunguka macho sasa.

Nyie semeni kanuni na kila kitu ila sisi tulioko Meru tunajua kuwa Jamaa ni raia wa Kenya na hajaukana mahakamani bado, Na Tunajua Tanzania hairuhusu Uraia wa nchi mbili. Ni kinyume cha sheria na tunangoja tuone mabavu yenu CCM na serikali kulificha hili.

Je chama kilipompitisha hakikuliona hilo? Au ubabe tu.
Tume ya Uchaguzi kupokea jina haikufaham kuhusu uraia wa Sioi? Au haikuchunguza? Si ni moja ya kazi zake?


Ritz kaka, usiongelee ukiwa mbali, Karibu Arumeru ujionee mwenyewe, ukija usifikie Kibo Palace wala Ngurdoto. Njoo mtaani ukae na sisi ujionee
 
Back
Top Bottom